Ushauri: Je, nilipe hili deni la benki?

swagy

Senior Member
Jan 23, 2018
131
201
Hamjambo waungwana?

Mimi ni muajiriwa serikalini, mwezi wa kwanza nilikopa pesa katika taasisi fulani kiasi cha milioni sita na pointi kadhaa, ambapo riba/ marejesho kwa miaka mitano ni milioni kumi na mbili na pointi kadhaa.

Hoja iliyonifanya niombe ushauri ni kuwa mwezi wa pili sikuchukua hati ya mshara(salary slip), ili kuangalia makato yangu lakini mwezi wa tatu nimechukua na kukuta kuna makosa yalifanyika katika kujaza deni.

Hapa nimekuta nadaiwa milioni moja na point fulani ambapo nategemea kumaliza deni ndani ya miezi takribani saba, ambapo deni halisi ni milioni kumi na mbili na point, ambapo ninapaswa kumaliza kulipa deni kwa muda wa miaka mitano.

Nilichogundua ni kuwa deni liliingizwa vibaya badala ya kuiandika milioni kumi na mbili na point wahusika waliandika milioni moja na laki mbili na point kadhaa, hivo kunipa unafuu wa kumaliza deni kwa muda wa miezi takribani saba.

Nimejaribu kuongea na watu wangu wangi wameniambia nisiende kuwajulisha benki kwani sio mimi ndo nilisababisha hiyo hali.

Swali langu hapa/ msaada ninaotaka ni je wahusika ambao ndo benki wanaweza gundua hili? Na je ni namna gani wanaweza kugundua na je wakigundua kuwa marejesho yamesitishwa ilihali wanajua kuwa wananidai milioni 12 wataniadhibu, au je niende nikajisalimishe ili kuepuka usumbufu?

Naomba msaada wenu wapendwa
 
Unakopa milion 6 na ushehee baada ya miaka 5 unarudisha milion 12. Watu mnafanya mzaha na maisha
ok! Anyway piga kimya watarekebisha wenyewe. Kwangu lbd unipe miaka 25 ndiyo nitaweza kukopa milion 6 nikarudisha milion 12.
 
Unakopa milion 6 na ushehee baada ya miaka 5 unarudisha milion 12. Watu mnafanya mzaha na maisha
ok! Anyway piga kimya watarekebisha wenyewe. Kwangu lbd unipe miaka 25 ndiyo nitaweza kukopa milion 6 nikarudisha milion 12.
Serikali inadaiwa kaka ije kuwa Mimi,?
 
Serikali inadaiwa kaka ije kuwa Mimi,?
Ukitaka kufanikiwa ktk jambo lolote usijifunze kwa walioshindwa. Kwahiyo serikali kudaiwa na ww kudaiwa unachukulia poa tu?
Kwahiyo mke wa jirani yako akigongwa nje na wako pia utachukulia simple tu kisa na wa jirani kagongwa?
Ok! Tuyaache hayo. Kaa kimya watarekebisha wao ila nakushauri acha kukopa pesa kwa riba kubwa bali uwe mtu wa kuzalisha hela.
 
Back
Top Bottom