Ushauri: Idea 5 za biashara

Stability

Senior Member
Jan 30, 2020
171
332
Habari wana Ndugu,

Tunatofautiana ufahamu, ulipoishia wewe kufikiri ndio mwanzo wa mwingine. Hizi idea tano nimezifanyia zote uchunguzi kwa kiasi na nimepata ufahamu wa hizi ideas kwa kadri ya uwezo wangu.

Nina Tsh 14 million (hapo nishatoa gharama za kodi ya frem, urekebishaji wa frem, usafiri wa mzigo, Tax clearance, akiba ya kuishi siku kazaa, n.k), Location ni jijini Mwanza urban.

Kwa kutumia uzoefu wenu na uchambuzi wa biashara mgenishauri niinvest katika idea ipi kati ya hizo hapo chini. Biashara itakayo nipa return ya uhakika wa kuendesha life yangu.

IDEAS ZILIZOPATA:
1: Aina zote za Vipodozi na Urembo tofauti tofauti (wigs, weavings, saa za mkononi, etc)

2: Duka maalum linalo deal na aina zote za Vitasa, Komeo na Bawaba tu za milango.

3: Vifaa vya umeme (installation, wiring)

4: Appliances za umeme za majumbani nianze na items kama TV, Radio, Pasi, Blenders, jagi la umeme...

5: Maduka mawili katika location tofauti yanayo deal na uwakala wa pesa mitandao ya simu (V'COM, A'TEL, TIGO...) na banks za CRDB, NMB.

6: Pazia za kisasa, sheers, mazulia ya sakafu, mazulia ya mlangoni (door rugs), bomba za pazia na fittings zake, mashuka special (set), nets, blankets

Pia kama unayo idea nyingine inayoendana na huo mtaji wangu, nitashukuru ukinisaidia hiyo idea.
 
Hiyo namba 4 kwa hela yako ni ndogo sana labda ufanye hiyo ma 3 na 2 kidogo mzunguko wa hela utakuwepo ila ukiingia hiyo namba 5 na 1 hutofika mahali maana kwenye mzunguko itakwama kwenye mali.

Labda uingize hela yako kwenye aluminium na glass na mapazia ya kisasa ndio biashara inayokimbiza kwa sasa.
 
ahsante boss kwa mchanganuo wakao, nisaidie una maanisha nini kusema kwenye mzunguko itakwama kwenye mali?

na pia hyo ya mapazia unakuwa una deal pazia peke yake au na unaweka bidhaa gani ya kwenda na hizo pazia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6.Spare za pikipiki na bajaj. Weka mafundi iwe gereji.
7. Biashara ya vitu vya jumla kama chumvi,mafuta ya kula, viberiti,unga,mchele,soda,maji,juisi,sabuni za unga, sabuni za kipande, stiliwaya,sigara,condom n.k
Fanya utafiti ukiangalia eneo ulipo,wingi wa watu ,hali ya kipato cha watu katika eneo lako, wingi wa maduka katika eneo lako na umbali toka barabara ya lami.

NB: kwenye mpesa na tigopesa kuwa makini sana wafanyakazi wanaiba balaaa, sikutishi ila ndio ukweli.
 
Utakaa dukani wewe au utatafuta mtu akuuzie duka? Pia wewe binafsi una ujuzi na nini? Naona kuna cosmetics (no. 1), hardware (2,3, & 4), na finance services (no. 5). Ni vizuri kuanza na biashara ambayo una ujuzi nayo.
 
6.Spare za pikipiki na bajaj. Weka mafundi iwe gereji.
7. Biashara ya vitu vya jumla kama chumvi,mafuta ya kula, viberiti,unga,mchele,soda,maji,juisi,sabuni za unga, sabuni za kipande, stiliwaya,sigara,condom n.k
Fanya utafiti ukiangalia eneo ulipo,wingi wa watu ,hali ya kipato cha watu katika eneo lako, wingi wa maduka katika eneo lako na umbali toka barabara ya lami.

NB: kwenye mpesa na tigopesa kuwa makini sana wafanyakazi wanaiba balaaa, sikutishi ila ndio ukweli.
ahsante kwa hizo ideas,

ahsante kwa ushari juu ya business ya uwakala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi yangu mm naona ufanye biashara ya vyakula hakika itoka na kilipa kwa sababu kula ndio kunamfanya binadamu aendeleee kuishi, unaweza ukafungua duka la kuuza vitu vichache kama sukari,sembe, mafuta ya kula,ngano,mchele maharagwe,njugu mawe,choroko, mbaazi na kunde tafuta duka zuli linalouza vitu bei ya rahisi kama mafuta ya kula, unaweza fuata mahindi Shamba na ukayaleta ukatafuta MASHINE ukasaga sembe kisha ukapeleka kuuza dukani kwako, biashara ya vyakula ni nzuli

ahsante boss kwa upeo wako, hili nalo nitaliangalia kwa ukaribu zaidi..kwa sababu ni fursa nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom