Ushauri: Harusi na mimba ya miezi 7

Ushauri: Harusi na mimba ya miezi 7

Wild fauna

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
461
Reaction score
189
Habari wadau,

Naombeni kupewa ushauri,

Nina mchumba wangu ambaye ninategemea kufunga ndoa siku za usoni. Bahati nzuri au mbaya ana ujauzito na kwa mipango na taratibu nilizoziweka katika kukamilisha zoezi la harusi mimba itakuwa na miezi 7. Naomba kushauriwa, inawezekana kufunga hiyo ndoa akiwa na mimba ya umri huo? Au niahirishe mpaka ajifungue then ndio tufanye hilo zoezi.

Naomba ushauri wenu.
 
Kwanini hamkufunga ndoa kabla hamjapeana mimba?
Subiri sasa ajifungue apumzike vya kutosha ndio muanze purukushani za sherehe ya ndoa. Kwa kukadiria ni kama miaka miwili ijayo.
Au tumieni njia fupi (mkiwa nyie ni wakatoliki) nendeni misa ya asubuhi mfunge ndoa. Hapo ataweza kumudu purukushani.
 
Mmh bwana muache tuu kwanza ajifungue..... Kwanza mimba ya umri huo atakua amechoka sana na pia huko mbeleni anaweza asifurahie pia kkuangalia picha za harusi yake maana watu wengine wakati wa ujauzito swanakua tofauti uso mara umevimba pua cjui imekaaje..... ptuuuu muache tu ajifungue kwanza then apumzike kidogo mambo yaendelee
 
Ngoja kwanza upepo huu uishe atakuwa kashajifungua tayari.

Sa hizi wahuni wana roho mbaya sana wanaweza tuma picha tena ikawa hatari.
 
Asanten kwa ushauri wadau. Cha msingi nipeleke tuu mahar na kuweka mambo sawa kwa wazaz wake
 
Mmh bwana muache tuu kwanza ajifungue..... Kwanza mimba ya umri huo atakua amechoka sana na pia huko mbeleni anaweza asifurahie pia kkuangalia picha za harusi yake maana watu wengine wakati wa ujauzito swanakua tofauti uso mara umevimba pua cjui imekaaje..... ptuuuu muache tu ajifungue kwanza then apumzike kidogo mambo yaendelee

Lakin hiv kuna ndoa za stahili hyo znafanyika? Kwamba ndoa zenye mdada mwenye mimba kubwa kiasi hicho au mie ndie itakuwa ya kwanza?
 
Subiri ajifungue. Hata kama unamuamini siku hizi lolote linawezekana. Wasichana wanakuwa na wachumba zaidi ya mmoja in case.mmoja akizengua. Si busara kujiaminisha sasa hivi kwamba alikuwa wa kwako peke yako.
 
Habari wadau,

Naombeni kupewa ushauri,

Nina mchumba wangu ambaye ninategemea kufunga ndoa siku za usoni. Bahati nzuri au mbaya ana ujauzito na kwa mipango na taratibu nilizoziweka katika kukamilisha zoezi la harusi mimba itakuwa na miezi 7. Naomba kushauriwa, inawezekana kufunga hiyo ndoa akiwa na mimba ya umri huo? Au niahirishe mpaka ajifungue then ndio tufanye hilo zoezi.

Naomba ushauri wenu.
akitoka honeymoon, likizo ya uzazi timing nzuri mkuu
 
Fungeni.
Mkihairosha mtajikuta mnaishi miaka 16 hamajafunga.

Achague nguo nzuri itakayositiri tumbo vizuri.
Asivae hills atafute sandals nzuri unique

Asisimame saaana
 
Shida Ni kwamba akisha jifungua process za kufunga ndoa zina kosaga hamasa..

my bro alisemaga ivo mke akitoka Tu uzazi tunafunga ndoa hadi Leo mtoto Ana mwaka hamna cha ndoa .km inawezekana fungeni Tu bila kufanya sharehe..mje mfanye party badae km inaumuhimu kivile
 
Bariki sa hivi au funga sa hivi la sivyo subiri ajifungue ndionufunge ila haitaniga....mlikuwa na haraka ah hakukuwa na plan.....inapendeza after ndoa ndio mimba......so far you got to choose
 
Hapo tatizo sio kufunga/kubariki ndoa. Shida ni sherehe ndio tatizo kwako mkuu. Kama ni ndoa funga tu.
 
Shida Ni kwamba akisha jifungua process za kufunga ndoa zina kosaga hamasa..

my bro alisemaga ivo mke akitoka Tu uzazi tunafunga ndoa hadi Leo mtoto Ana mwaka hamna cha ndoa .km inawezekana fungeni Tu bila kufanya sharehe..mje mfanye party badae km inaumuhimu kivile

Asante sana kwa ushauri
 
Back
Top Bottom