Ushauri fao la kujitoa NSSF

Msaranga

JF-Expert Member
Feb 10, 2009
956
227
Wadau,

Mimi nimefanya kazi miaka 12 nikaamua kuacha kazi nikiwa na biashara zangu ndogo ndogo nikajua kiasia nilichonacho NSSF around 60milioni ingeniwezesha kupanua biashara zangu na kwenda mkoani kuwekeza kwenye kilimo.

Cha ajabu nimekaa miezi sita nilivyofuatilia FAO lakujitoa NSSF wakaniambia eti kwa kuwa nimeacha kazi mwenyewe sistahili kupewa fedha zangu nikashangaa sana eti wanaopewa ni walioachishwa kazi tuu.

Sasa wadau naombeni msaada wa ushauri nifanyaje niweze kupata fedha zangu niweze kujiandalia maisha ya uzeeni mwenyewe maana sana nina miaka 38 ninanguvu za kupigania maisha yangu ya baadae mwenyewe.

Nawasilisha
 
afadhali hata nssf wanatoa fao la kujitoa kama umeachishwa kazi, au contract kuisha, sasa mimi niliachishwa kazi nmb yapata miezi 9 sasa, nilikuwa PSPF nilivoenda kujitoa nkaambiwa nikae miezi 6 ndo ntapata haki yangu na fomu za kujitoa nikajaza kabisa, lkn ajabu nlivorudi baada ya six month naambiwa cwezi pata mpaka ntimize 55yrs, wakata kazi ilikuwa ya muda na nimefanya mwaka 1.5 tu mafao hayafiki hata 2mlns. ila wenzangu walokuwa lapf tulioachishwa kazi wote walishaoata chao, me naambiwa et serikali umezuia, sasa najiuliza umezuia kwa PSPF tu, pesa yangu inanuma sana nkiwaza kuwa nimenyimwa haki yangu wakati mimi cna hata mtaji wa ujasiliamali.
 
Hii issue ya fao la kujitoa bado ni janga. Nakushauri kwa sasa angangalia namna nyingine kuweza kuendeleza miradi yako na maisha yako. Ukiiwazia sana hii kitu itakutoa kwenye mstari kaka.
 
Hii issue ya fao la kujitoa bado ni janga. Nakushauri kwa sasa angangalia namna nyingine kuweza kuendeleza miradi yako na maisha yako. Ukiiwazia sana hii kitu itakutoa kwenye mstari kaka.
Duh yaani wee acha tuu tunatiana umasikini hivi hivi
 
rudi kwa HR akuandikie barua ya kuachishwa kazi.

umeandika kama ni rahisi sana.. unafikiri nssf ni wajinga??

na hata huyo h.r nae unafikiri ni mjinga hajui kitachomkuta akigundulika ameongopa... na barua ya kuachishwa kazi lazima iwe na sign ya managing director kama mkataba vile... je managing director gani atasaini barua ya magumashi...
 
huo ndio mtaji wake alioutegemea.. hana pengine

Hii issue ya fao la kujitoa bado ni janga. Nakushauri kwa sasa angangalia namna nyingine kuweza kuendeleza miradi yako na maisha yako. Ukiiwazia sana hii kitu itakutoa kwenye mstari kaka.
 
Kama Una Baba yako, Mama Yako, Bibi Babu, Dada Na Hata wewe Mwenyewe na Wanyonge Wote Serikali ya Awamu ya Tano Imekaribia kuleta Mkong'oto Huu Huu hapa (Kilio na kusaga Meno)

Kuna mswada unakuja na kwa Bunge letu la Wangapi wanakubali Waseme Ndiyooooo "Ndiyoooooo" waliosema ndiyo wameshinda "Utapita"

MSWADA HUO Unaenda kuua wastaafu Na sisi Tunao karibia kustafu

Ni hivi Mafao ya wastafuu yatakuwa hivi Tega sikio, utalazimika kulipwa 38% tu na 62% utakuwa unalipwa kila Mwezi (monthly) hapa ili unielewe nikupe mfano. kama ilikuwa ulipwe milioni 100 kama hela yako ya kustafia maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi.

Ukistafu na umri wa miaka 61 utakula hicho kiasi cha million 38 kigingine utalipwa kidogo kidogo kila mwezi

Ubaya wa hili siku ukifa tu kila kitu kimekufa malipo kila mwezi nayo yanakufa. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma wakati ungepewa yote ungewaachia miradi familia wakaishi hata kama haupo

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu. Yaani LPF, NSSF PPF sijui nani sijui nani itafungwa na kubaki mifuko miwili tu (Vibarua vinaenda kuota nyasi)

4. April 2018 sheria itaanza kutumika Yaani Mwakani Kuna kilio kikuu kwa watumishi wa mifugo na wastafuu

My Take

Kwa ufupi bila kupindisha muswada huu utaumiza watumishi wote ,Bunge Mkafanye kazi yenu, sasa Hiki ni kipimo chenu cha kudhibitisha Mpo huru na kwamba ni muhimili unajitegemea ,Wabunge wetu msipoliona hili kuwasemea watumishi basi Mtawasononesha watumishi

Yaani Ufanye kazi miaka 61 ukitumikia umma uzeeni uporwe haki itasikitisha

Alloyce Nyanda
Mtozi
 
Back
Top Bottom