Ushauri: Benki gani naweza kupata mkopo wa haraka?

my king

Member
Jan 22, 2014
48
9
Nina Contract ya kazi as independent Consultant katika sekta ya ujenzi, nimepata changamoto ya fedha kuendelea na hii kazi kwa kiasi fulani nimekwama, nafikiria kuomba mkopo bank wa mda mfupi unisaidie kuendelea na hii kazi.
Naomba mawazo yenu wadau bank gani naweza kupata mkopo kwa haraka na yenye masharti nafuu.
Nakaribisha mawazo yenu wadau.
 
Nenda Benki kuu,ila lazima uwe umesajiliwa kama Kampuni nauna uzoefu wa kazi husika kwa references ya kazi umezowahi kufanya,dhamana lazima,na sio blaa blaaa
Benki kuu ndugu yangu naanzaje! Sina Kampuni ndo kazi yangu ya kwanza ninafanya as individual Consultant kama kuna alternative nyingine mbali na benki kuu nitashukuru pamoja na maelezo ya dhamana zitakazohitajika.
 
Sikukatishi tamaa,kama huna kampuni hakuna bank hata moja itayokupa mkopo wala kufikiria kukupa Mkopo.
Mkopo sio rahisi kama tunavyofikiria.
Na hapo kama ndio kazi yako ya kwanza ni kwamba unaifanya bila kuwa Licensed,sasa ni kwamba bado inatia mashaka nani anakupa kazi bila kuwa na license.

Wengi mliomaliza chuo cha Ardhi mnapata tabu sana kwenye kuanza,na tatizo ni kwamba hamna umoja.Mgejiunga kikundi na kuunga unga pesa zenu kisha mkanzisha kampuni basi mngepata tenders za uhakika.
We angalia mfano kampuni za wana sheria Advocates,unaweza kukua imeandikwa Rwechungura and Jonas Advocates,au Juma and Michel advocates,lengo ni kutafuta nguvu
 
Mh! Sawa mkuu
 
Mkuu king nilichomuelewa usitaje namba tu za simu labda utaje na benki kwa faida ya wachangiaji wote
 
License..

Tax clearance form..

Business Location..

Collateral..

Kama huna hizo usisumbuke kwenda bank kuomba mkopo labda upate nduguyo tajiri akukopeshe
 
Kama sio muajiriwa kupata mkopo inakuwa ishu sana kama auna mali isiyoamishika ndugu yangu. Benki nyingi azikubali hata kama ni kampuni lazima uweke mali ya kampuni husika
 
Nenda Bayport! Ukienda asubuhi, jioni umepata. Hawana longo longo ila riba yao ni kibwa ki mtindo
 
Ahsante masharti yao yapoje mkuu
Uwe na salary slip mbili za miezi miwili ya karibuni, uwe na barua kutoka kwa mwajiri na ujaze fomu ya maombi ya mkopo. Kwa maelezo zaidi tembelea tawi lao lililopo karibu kwa ufafanuzi zaidi.
 
Ni jambo lililo wazi na bayana kuwa benki "si rafiki wa watu maskini". Jitahidini uunge unge siku ukiwa na pesa benki zitakufuata ili wakupe mkono.

Kwa hali uliyonayo njia lahisi na ya haraka ni kutafuta mtu wa kuingia nae ubia katika hiyo kazi. Yeye awekeze fedha na wewe utaalamu. Mwisho wa siku wote mpate hela ya maji.
 
Back
Top Bottom