Ushauri makini sana.Hili suala usilichukulie poa sana. Tuliza akili zako kabisa. Usije ukabadili taswira ya malezi yako kutoka kwa baba yako mlezi. Utamvunja moyo baba yako aliyekulea toka utotoni mwako, usipokuwa makini.
Fikiria, baba mlezi alimkubali mama yako bila kujali ni single mother, tena aliyekuwa tayari ameshaolewa akaachika na bado akakubali kukulea hadi sasa 24 yrs! Na bado hakuweza kukutenga wala kwa chochote.
Utakapojitegemea utaanza hizo harakati zako kijana.
Fikiri kabla ya kutenda.
Kweli kabisaWanasemaga mtoto wa mwenzio mbebe akiwa kalala akiamka atamtafuta mzazi wake....
Kwa busara ongea na baba kaa nae mzungumze kiume, ila sijui hata atalipokeaje pole sana.
naanza kuelewa kwanini kina mama wengine huwa hawataki kusema ukweli kwa situation kama hii naona inaleta vurugu tu na kuondoa amani iliotawala kipindi chote cha kupiga kimya.