Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 550
- 786
Nchimbi ni akili kubwa sana aliposema Watumishi wa Umma siyo maadui wa chama tafsiri yake ametumia hekima ya wazee wanaosema Mkeo akikosea anasemwa chumbani siyo hadharani,Kuku wako Manati ya nini wakati jioni anaingia Bandani.
Anachokifanya Makonda kwasababu ni populist kinawezekana kikampa umaarufu ila kina gharama pia kwa chama cha Mapinduzi kwasababu kinachonganisha Chama chake na Watumishi wa Umma ambalo ni kundi lenye wapiga kura linalohitajika kwao.
Ninafahamu zipo Sheria,Kanuni na Miongozo ya Watumishi wa Umma ikiwemo ya kuwawajibisha hawa Watumishi wanapokosea najiuliza kwanini havitumiki kinaanzishwa kitu kingine cha kudhalilishana kwenye majukwaa ya kisiasa tena mbele ya vyombo vya habari Dunia nzima inaona.
Makonda anachotaka kuwaaminisha watu ni kwamba Matatizo yote ya Wananchi yamesababishwa na Watumishi wa Umma pekee Wanasiasa hawahusiki kabisa,je hii ni kweli?
Ninafahamu hata yeye alipokuwa Kinondoni baadae Jiji zima la Dar es salaam hakuweza kumaliza Kero sasa kwanini leo aone wenzake wote hawana wanachokifanya wala wanachokijua ndiyo maana kero zipo,kwanini asikiri mfumo una shida itafutwe namna bora ya kutatua kero hizo hata kama yeye hayupo.
Inavyoonekana Watumishi wa Umma wakifanya Mema ni ya Wanasiasa wakifanya Mabaya ni ya kwao,sasa kwanini asishauriwe kutenda haki akapiga Back to Back nyingine ya kupongeza Mema yaliyofanyika?
Ni Mtazamo tu,mawazo tu masela msijenge chuki,Naruhusu POVU.