Ushauri: Anataka kusomea upadri ila wazazi hawataki

LAMBOFGOD

JF-Expert Member
Aug 12, 2016
1,561
1,317
Kuna kijana jirani yangu anataka akasomee mambo ya upadri lakini wazazi wake wamemkataza kwa kila sababu wanazojua wao na wanamwambia atafute kazi ili akaajiriwe.

Sasa jamaa kaja kwangu, me of course “nimemshauri aendelee na lengo lake ili shauku ya moyo wake itimie kwa sababa swala la kazi si la mzazi ila mhusika mwenyewe” am I wrong katika ushauri huo?

Karibu kwa maoni na ushauri based on biblical evidences ili wazazi wake wasione kama jamaa anawadharau.


Update kidogo wanajamvi

Majirani tumeitwa na mama mtu ili kushauri kijana lakini mama kasema hataki mambo ya upadre ni akheri akope pesa amsomeshe masters kuliko kuwa padre na akaanza kububujikwa na machozi akisisitiza kutoridhia na swala hilo na hatimaye katamka maneno mazito kabisa kwamba akienda upadre hatamaliza na atachanganyikiwa, kwa sababu haiwezekani amsomeshe mda wote huo hadi chuo then achukuliwe juu juu kama wao ndo waliohangaika naye na kumwuita mwanaye mjinga kwa sababu hamsikilizi anachomtaka akitekeleze yaani asitishe wazo lake hilo. mama katia jazba hata hatujafikia muafaka kabisa

Samahani lakini kwa yule nitakaye mwudhi wanajamvi
 
Kuna kijana jirani yangu anataka akasomee mambo ya upadre lakini wazazi wake wamemkataza kwa kila sababu wanazojua wao na wanamwambia atafute kazi ili akaajiriwe, sasa jamaa kaja kwangu, me of course “nimemshauri aendelee na lengo lake ili shauku ya moyo wake itimie kwa sababa swala la kazi si la mzazi ila mhusika mwenyewe” am I wrong katika ushauri huo?

Karibu kwa maoni na ushauri based on biblical evidences ili wazazi wake wasione kama jamaa anawadharau
Kwanza kabisa je hao wazazi wake ni watu wa dini au la??
Ukute wazee wa watu wanataka wajukuu halafu kijana anataka kuwakatili
 
Kuna muda mwingine wazazi, wanakosea sana!
Hapo ukiwapinga tu! unaonekana kiburi.. kisa wao ndio wanaokusomesha!
Mwambie akae nao azungumze nao kwa nidhamu na busara sana kuhusu msimamo wake..
Akishindwa atafute watu wenye busara ambao wataongea na wazazi wake, huenda itasaidia..
Ikishindikana kabisa basi, awasikilize wazazi wake..
 
Wazazi ndo wamemzaa,wakamlea,wameishi maisha muda mrefu, wana experience and always wanamtangulizaga mwanao mbele.. afate wanavomshauri.. maana huko mbeleni mambo yakiharibika,ww ulompa huo ushauri utakuwa wa kwanza kujikataa..
 
Hivi huyo kijana ana heshima kweli?? Amri ya 4 inasemaje?? Afuate maelekezo ya wazazi wake. Wazazi wameona yanayo tokea makanisani. Kilaini na fweza ya Escrow, Mokiwa na mikataba feki, Jima na mke wa Mbasha, Luse na bapa lake we unataka nini tena?? Kijana, usibishane na wazazi wako wao waliiona dunia ile wakilinganisha na hii ya leo, wanaona akheri upagani kabisaaa
 
Safari ya Upadre si ndogo, ajitafakali kama kweli yupo tayari kwa hilo. Pia nadhani panashida maana kama kweli yupo serous, kuna jumuia huko anakoishi, na pia viongozi wa kanisa amabao wanaweza washauri wazazi wake na sio wewe, usichukue kila jambo kirahisi namna hiyo na kulileta hapa JF
 
Kila la kheri kwa huyo kijana aende tu hata kimya kimya sio lazima ajioneshe, au ni lazima usomee? But Jesus hakupiga theology kua Padre
 
Kuna kijana jirani yangu anataka akasomee mambo ya upadri lakini wazazi wake wamemkataza kwa kila sababu wanazojua wao na wanamwambia atafute kazi ili akaajiriwe.

Sasa jamaa kaja kwangu, me of course “nimemshauri aendelee na lengo lake ili shauku ya moyo wake itimie kwa sababa swala la kazi si la mzazi ila mhusika mwenyewe” am I wrong katika ushauri huo?

Karibu kwa maoni na ushauri based on biblical evidences ili wazazi wake wasione kama jamaa anawadharau.
Wanamjua ni choma choma
 
Afuate moyo na dhamira yake inavyomsukuma hasa ukizingatia anataka kufanya kazi ya Yesu Kristu, sioni ubaya.

Wazazi waache tamaa ya mali kwani hapa duniani ni wapita njia tu, na kijana ajue kuwa siku ya kufa atakufa peke yake na si na wazazi, hivyo suala la kuchagua njia ya Mungu ni muhimu kuliko hayo maoni ya wazazi wake.
 
Back
Top Bottom