The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 381
Mimi ni msichana wa miaka 28. Nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana mwenye umri sawa na wangu. Tulidumu kwa muda wa miezi nane.
Mwanzoni mwa mahusiano yetu, tulipendana sana. Baadae mwenzangu akaamua tu kunibadilikia na kusitisha mahusiano. Pamoja na kuachana huko, bado tuliendelea kuwa karibu, tulionana ingawa ugomvi wa mara kwa mara ulikuwepo.
Nilidhani alikuwa amepata msichana mwingine hivyo nikaamua kuthibitisha fikra zangu kwa kuchunguza nyendo zake kwa kutazama simu, barua pepe zake na hata mitandaoni (Nazijua password zake). Hakuna nilichoambulia mpaka sasa.
Yeye binafsi amekuja na pendekezo la kuachana lakini tuendelee kuwa karibu. Ukaribu tulionao hauna tofauti sana na kipindi tukiwa kwenye mahusiano.
Kutokuwa wapenzi ndio tofauti pekee iliyopo. Mimi binafsi nimeshangazwa na hali hii. Sijui kama inawezekana wapenzi wakabaki kuwa best friends, ndugu wana jamii forum, naombeni ushauri juu ya haya:
1). Huyu mwanaume bado ananipenda kweli?
2). Inawezekana kuwa marafiki baada ya kubreak up?
3). Itakuwa ni busara mimi kuendelea kuwa nae kama rafiki wa karibu?
Msaada tafadhali.