USHAURI: 63" Hisense Vs 55" Samsung

Ungeweka model number za hiyo Hisense na Samsung ndio tukushauri,hapa hatuangalii jina tu kutoa ushauri.
 
Type elimu kidogo Mkuu umefanikiwaje kukaa nazo muda mrefu hvyo. Tunaomba darasa la jinsi ya kuzitunza me mwenyewe nilikua nataka kubadili TV nichukue hiyo brand lakini naona humu ndani inapondwa sana
 
Type elimu kidogo Mkuu umefanikiwaje kukaa nazo muda mrefu hvyo. Tunaomba darasa la jinsi ya kuzitunza me mwenyewe nilikua nataka kubadili TV nichukue hiyo brand lakini naona humu ndani inapondwa sana
Mkuu mimi binafsi sioni kama kuna matunzo ya ziada ninayoyafanya, nikiitundika ukutani imetoka hiyo sansana huwa inafutwa vumbi tu kama tunavyofanyaga kwenye Tv ya aina yoyote.
 
Dah, sijui mtakuja kuacha lini huu ushamba wa brand!! Usibabaishwe na brand unapoenda kununua vitu na vifaa vya umeme kwa nchi ya Tanzania!!!
 
Watu kama Nyie wafanyabiashara wanawapenda sana. Only huku kwetu hizi brand za ajabu ajabu zinafanikiwa.
Umejibu kwa kutumia mhemko na siyo mantiki.Kwa hizi brand fake zilizojazana Tanzania, linganisha na uelewa wao kuhusu ubora wa vifaa vya umeme unahisi wanaweza kutoboa?? Hizo bei zake wanaweza kumudu??Unakubali wauziwe brand fake kwa bei halisi??

LG, Samsung,Sony,Tcl,Hisense n.k kutofautisha hii ni fake au halisi kwa watanzania wengi hawana huo ufahamu zaidi ya ujuaji na ushamba.Hizo halisi bei zake(wengi wao) kwa Authorized agents watazimudu??
 
Tatizo lako hujui na hutaki kujua na unakatisha tamaa wenzako wasijue ili wote msijue.

Kujua Display fake ama ya low quality si kazi ni kitu cha sekunde kadhaa tu ama dakika mfano.
1. Kioo kama ni ips ama low quality vya tft unaangalia tu viewing angle, nenda kulia, kushoto katikati ikiwa haioneshi kwa quality nzuri sio panel nzuri ya display, panel mbaya siku zote inakuwa na view angle mbovu.
2. Plasma siku zote ni kama Glass haina weusi wa LED inakuwa kama kijivu same kwa panel za zamani unazozikuta kwenye chogo.
3. Oled ukionesha Picha nyeusi ukiwa umezima taa inakuwa kama tv imezimwa, ama kwa mzoefu akiangalia tu kwa macho wakati inaonesha rangi nyeusi anajua hii oled, led/lcd haiwezi onesha nyeusi tii. Etc

Pia kila brand inakuja na Unique features
-Samsung smart zina Tizen
-LG smart zina Web os
-TCL smart zina Certified Google TV (Android TV) ama Roku ama opera TV
-Hisense zina Vidaa os etc.

Wachina wa kawaida ama TV fake zina android ambayo sio certified ni aosp ya kawaida kama kwenye simu ama tablet na wanaweka tu Launcher ku imitate, app zake ni za simu hazipo optimized kwa TV kwa macho tu unaona utofauti na Brand za juu.


Na Bei za TV ni within laki mpaka laki 2 Kibongo bongo, baina ya Wachina na brand kubwa

Mfano Tcl ni laki 4 mpaka 5, mchina choka mbaya ni ariund laki 2 na something mpaka 3, kama unaweza Afford toa laki 3 ukanunua TV isio na jina huwezi shindwa kuongeza kidogo ukanunua TCL ama Hisense.

Ukienda Inch 40, 43 ni hivyo hivyo unakuta LG na star x utofauti ni chini ya laki 2, unatoa laki 6 unanunua no name chinese unaacha laki 7 OG.
 

Wewe Sasa ndio umeongea jambo la muhimu.
Raia aangalie kama anaridhia na kiwango Cha muonekano wa picha abebe kifaa. Wengi hatuwezi kumudu Bei za vitu original licha ya kutamani features zake. Ndio maana vifaa vingi vya electronics hata mavazi pia yanayoletwa huku kwetu ni viwango duni ili tuweze kumudu Bei, zile zenyewe watanunua wachache sana ambao wanaweza kuagiza hata nje ya nchi kutokana na kuzingatia ubora.
 
TV bora kwa sasa ni:

-SONY
-LG
-SAMSUNG
-TCL
-HISENSE
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…