ushaur wenu naomba

ushaur wenu naomba

Tuna sahau kuwa hili jukwaa lina angaliwa/tazamwa/changiwa na watu tofauti tofauti, uandishi huo kwenye blue una kera sana.
Sidhani kama ataweza kukuelewa kama wewe mwenyewe unashindwa kuandika ili watu wote waelewe.
Samahan mi skujua ilo, mi ni mgeni humu
 
Pole sana binti kwa changamoto hiyo inayokukabili, maisha ni maamuzi na pia ni chaguzi. Namna unavyoishi leo inaweza kukuonesha utakavyoishi kesho, uchaguzi mzuri/mbaya unaoufanya leo ndio utakao kuletea maisha mazuri/mabaya utakayo ishi kesho. Wewe bado mtoto mdogo ndiyo maana unataja mambo mengi sana ya mpenzi wako yanayokukera lakini cha ajabu bado unasisitiza kuwa nampenda sana, tena kwa kung'ang'ana.
Kwakua umeomba ushauri basi nisikilize mtoto mzuri ili nikushauri nawe ufanye maamuzi.
1. Kaa nae seriously kwa mazungumzo, mweleze kinagaubaga hatari ya kile anachokifanya kwa mustakabali wa maisha yenu ya sasa na ya badaye. Mweleze unapenda kuishi maisha ya namna gani (kumcha Mungu, ulevi etc)
2. Jiwekee deadline, namaanisha panga muda wa matazamio. Unampa muda gani awe amebadilika?
3. Chukua hatua either kuachana naye au kukaa vyovyote atakavyokua.
Angalizo:
Kama unataka uingie naye kwenye ndoa kuwa makini katika kufanya maamuzi, ndoa siyo mapenzi ya miaka 2/3/4 au 5. Hapa tunaongelea maisha dada, vitu ambavyo unaona anakufurahisha vingine ni vya kupita, anafanya tu ili ukamatike. Ukiingia kwenye ndoa na kukaa vya kutosha, kuzoeana vya kutosha, kujuana vya kutosha utakuja gundua kuwa maisha ni zaidi ya matamanio na hapo ndipo utakapo jilaumu kwa uchaguzi ulioufanya au utamshukuru Mungu kwa uchaguzi ulioufanya.
Wanandoa wengi sana wanalalamika, wanaume wakiwalaumu wanawake na wanawake wakiwalaumu wanaume kuwa ndio wabawa bila kujua kuwa huyo aliyenae (personally) ndiye mbaya na hii ni kutokana na uchaguzi alioufanya kwa hiyari yake. Kuwa makini wakati wa uchaguzi ili ufurahie matokeo.
Asante kwa ushauri ntajita
id kufanyia kazi
 
kwa umri huo kupambana na mvuta bangi.sigara sijui makitu gani mapema sana nenda skuli atakuzeesha bure
 
Mpeleke akaombewe ili hayo makitu ayaache. Hivi hivi haiwezekani binti yangu
 
Unajua nini? Haniker wala hanifanyi vitu vibaya, but sipendi because haina faida, na its not good for health

kama hukereki basi haijalishi
hizo ndio starehe zake,siku
akiona hazifai ataacha mwenyewe!!
 
Back
Top Bottom