Ushairi: Taswira

Fikra Angavu

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
301
105
Taswira
Alimkuta amelala,
Akamziba masikio,
Kisha akamwambia,
"Amka Huu mchana wewe".

Hakua kiziwi,
Ila alikua fofofo,
Kwa mnong'ono wa jazba,
"Shauri yako na maisha yako"

Watu walikuwepo,
kwa mbali na mwingi upepo,
Walishuhudia kwa vitendo,
"Hata ufanyeje watu hawa hawaelewi"

Vitendo vya ria,
Taswira hasi ya wenye kusikia,
Kwa majivuno huwaambia,
"Jamani nawapenda ila mjipende pia"

Aliamka na kiza machoni,
Kazibwa na kitambaa usoni,
Akauliza Jamani vipi kulikoni?
Akajibiwa "tuliza macho utaona"

Kwakua alitoka ndotoni,
Macho kenu mithili ya mwanaugoni,
"Jamani ni nini hiki usoni?"
"Tuliza munkari, ni kinga ya wajihi"

"Jamani kwani niliomba?"
Sogora kwa kujigamba,
Mdomo ulioanuka kama Mamba,
"Si unaniamini?, najua kizuri kwako"

Anajua wanachotaka,
Wanajua anajua mipaka,
Ila moyo watia mashaka,
"Hivi ni asali au sharubati ya ukwaju?"

Baba, mama, dada na kaka,
"Upi ni uzuri wa shimo la taka?
Lijae au liwe tupu? Napata mashaka,
Kwa ukali, "Fata yanayokuhusu"

Muuliza swali hajui jibu,
Ili hali anajua yanayo msibu,
Lakini ana picha ya mtabibu,
"Tatizo nini? Mbona kila kona kona"

Usiniulize maana,
Haitafsiriwi tafsiri,
Ni fikra za asiyefikiri,
Mtaarifu ana arifu kwa arafa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom