Ushahidi wa Wabunge utaendelea kufichua mengi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushahidi wa Wabunge utaendelea kufichua mengi...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Emils, Jul 6, 2011.

 1. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  USHAHIDI ni ithibati ya kuona kitu au tendo ama kusikia maneno na kuhakikisha kwa kueleza mambo yaliyokuwa yakitendeka; uthibitisho, ushuhuda. Suala la wabunge kutakiwa kutoa ushahidi wa madai yao limepamba moto katika vikao vya Bunge linaloendelea sasa. Mara zote wanaotakiwa kutoa ushahidi ni wabunge wa upinzani. Kwanza alikuwa mbunge wa Moshi mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philemon Ndesamburo (Ndesapesa) alipotakiwa kutoa ushahidi dhidi ya Frederick Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati wa utawala wa Ben Mkapa. Mbunge Zitto Kabwe wa CHADEMA alipata kusimamishwa kuhudhuria vikao kadhaa baada ya kumtuhumu Nazir Karamagi aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini kwa kusaini mkataba wa Richmond, ingawa baadaye iligundulika kuwa kweli alitia saini. Mara hii tena Zitto ametakiwa kutoa ushahidi kuwa baraza la mawaziri lilishawishiwa kubadili msimamo na kubariki azimio la kuongeza muda wa uhai kwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa miaka mitatu kinyume cha mapendekezo ya Bunge. Baada ya malumbano ya hapa na pale, hatimaye Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo alilazimika kurekebisha azimio hilo. Kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha sheria ya benki, Bunge linaazimia kuongeza muda wa CHC kwa miaka mitatu kuanzia Julai mosi mwaka huu hadi Juni 30, 2014. Hii itatoa fursa kwa shirika hilo kukamilisha taratibu za kiutendaji na kisheria na baada ya hapo serikali itafanya tathmini ya CHC na kupeleka taarifa bungeni ili kuona namna litakavyoshughulikiwa. Mapema mwaka huu Jeshi la Polisi lilitumia nguvu za ziada kuzuia na kutawanya maandamano ya amani yaliyofanywa na CHADEMA kupinga uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha. Katika vurugu hizo, watu watatu, mmoja akiwa raia wa Kenya waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa huku baadhi yao na viongozi/wabunge wa CHADEMA kufunguliwa mashitaka mahakamani. Katika kujitetea, Jeshi la Polisi lilionesha picha zilizohaririwa kitaalamu kuficha ukatili wa askari na kuonyesha pale wananchi walipojibu mashambulizi tu. Picha hizo zilionyeshwa kwenye vituo karibu vyote vya runinga kwa siku tofauti. CHADEMA kilitangaza kuonesha tukio zima bila kuhariri picha zile, lakini wenye vituo vya runinga walinyooshewa kidole wasikubali kuonyesha picha zile. Walijua wangeumbuka! Baadaye m-bunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) alitaka kujua mwongozo wa Bunge kama Waziri Mkuu analidanganya Bunge ni hatua zipi zichukuliwe dhidi yake, akakatizwa haraka na Spika Anne Makinda akimtaka (Lema) atoe ushahidi. Lema alipotaka kutoa ushahidi, akaambiwa autoe kimaandishi. Alifanya hivyo, lakini mpaka leo Spika ameukalia ushahidi huo. Kwa nini? Sikiliza. Wakati vurumai zile zikitokea mjini Arusha, Godbless Lema alikuwa miongoni mwa waliokumbwa na mzaizai ule. Waziri Mkuu Mizengo Petter Pinda (mwana wa mkulima) hakuwapo; alikuwa ofisini kwake pale Magogoni jijini Dar es Salaam. Hata hivyo akitoa taarifa yake bungeni, alikilaumu CHADEMA kuwa chanzo cha vurugu zile na kwamba Jeshi la Polisi lilikuwa sahihi kutumia nguvu za ziada ili kudumisha amani. Husemwa penye wengi hapa haribiki jambo. Kuna kila sababu ya kuamini kuwa uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa ushahidi wa Godbless Lema ni sahihi na ule aliotoa Waziri Mkuu ni wa ‘kupikwa’. Sasa baada ya mambo kuwa kama yalivyo, Spika Makinda anafikiri afanye nini. Akieleza ukweli, Waziri Mkuu ataumbuka na yeye (Spika) kuonekana hafai! Waziri Mkuu Pinda alipewa taarifa ya maandishi ya vurugu za Arusha. Waliompa ni polisi na wasaidizi wa ofisi yake. Kwa vyovyote vile, waliandika taarifa iliyoegemea upande mmoja, yaani ya kukitia hatiani CHADEMA na wabunge/viongozi wake. Kama ndivyo, Waziri Mkuu alilieleza Bunge kutokana na taarifa ya kuandikiwa kwa kuhakikishiwa na wasaidizi wake ambao hakuwa na sababu ya kuwatilia shaka. Kwa hiyo kuna kila dalili ya kuonyesha kuwa ushahidi wa M-bunge Godbless Lema wa Arusha Mjini (aliyekuwapo kwenye mzaizai ule), ni wa kweli. Huyu anazo picha zote zinazoonyesha tukio lile tangu mwanzo mpaka mwisho. Sasa kirumbizi/kiumbizi (ngoma inayochezwa na watu wawili wawili kwa kupigana fimbo) kinabaki kwa Spika Anne Makinda na Wazirii havistahiki sifa hizo. Wakati mwingine inachusha kuona wabunge wa CCM wakiwatupia vijembe wapinzani wakati wasemayo ni kwa manufaa ya wananchi wote. Ushabiki wa aina hii hauwezi kuwasaidia wananchi kwani maendeleo hayana itikadi wala mipaka na haichagui wanachama na wasio wanachama. Kero nyingine ni ya wabunge kutokuwapo bungeni wakati wa mijadala. Kwa kadiri ya picha zinazoonyeshwa kwenye vituo vya runinga, karibu robo tatu ya viti huwa wazi wakati wa vikao. Hao wengine huwa wapi? Hawa ndio wanaodai kwa nguvu posho zinazokataliwa na wabunge wa upinzani. Inakera kuona jinsi wabunge wanavyolala usingizi wakati mijadala mizito ikiendelea. Wanapopigwa picha na kutokea kwenye magazeti, wengine hujitetea kwa kusema eti walikuwa ‘wakikemea mashetani!’ Wengine huonekana dhahiri kutokwa na udenda (mate mazito yanayoteleza yamtokayo mtu anapolala). Huko ndiko ‘kutafakari?’ Wabunge kama hawa wanawasaidiaje wapiga kura wao? Ndani ya Bunge lenye vijana wasomi na machachari kama hili, hawafai chembe! Lile suala la baadhi ya wabunge kuingia kwenye shutuma ya kuomba rushwa mbona halijadiliwi haraka na kupata ukweli? Je, kama itabainika kuwa kweli, watachukuliwa hatua gani? Au kwa kuwa wao ndio watunga sheria suala hilo litafichwa ili life kifo cha mende? Kwa kuwa sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma, madai hayo yakibainika kuwa kweli, waondolewe kwenye ubunge na kufikishwa mahakamani sawia. Hivi sasa njia rahisi ya kuwa na maisha mazuri ni kuwa m-bunge. Ndiyo maana wanataaluma mbalimbali huacha taaluma zao na kupigania ubunge kwa hali yoyote iwayo, iwe kwa kuwanunua wapiga kura au kwa kutumia nguvu za giza. Bunge limejaa wanasheria, walimu, madaktari, mainjinia n.k. kwa kujua huko ndiko kunakolipa vizuri kwani kwenye taaluma zao hawapati mishahara mizuri na marupurupu wapatayo wabunge. Wasiokuwa na bahati ya kuwa wabunge wamekimbilia nchi za n-nje wanakolipwa vizuri kuliko hapa nyumbani ingawa wanaambiwa ’hawana uzalendo!’ Ni nani asiyetaka malisho mazuri na maendeleo ya baadaye? Mbona wao wameacha taaluma zao na kukimbilia kwenye ubunge?
   
 2. B

  BondJamesBond Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  space hamna siwezi kusoma
   
 3. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Acha uvivu nyie ndo wale wabunge wa ccm mnaounga mkono hoja bila kuisoma
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  du!
  naomba unisomee kwani mimi nimeshindwa pamoja na kwamba naona kama ni nzuri.
   
 5. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  No space, no paras. Tiring to read
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimemkumbuka maneno ya mwl wangu wa darsa la kwanza hapa Sunni manzil vikokotoni.
  Comma, full stop, space, paragraph etc ni muhimu sana
   
Loading...