Ushahidi wa Jerry Silaa Utata Mahakamani Leo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imekwama kufikia uamuzi kutokana na ushahidi wa Jerry Silaa kuwa na utata, anaandika Faki Sosi.

Dk. Onesmo Kyuka, Wakili wa Serikali ameieleza mahakama kuwa, kwa mujibu wa kanuni 21A(2) ya ushahidi, Silaa hana sifa ya kuwa shahidi wa kesi aliyofungua mwenyewe.

Silaa, aliyekuwa mgombea ubunge kwenye Jimbo la Ukonga, jijini Dar es Salaam kupitia CCM alifungua kesi hiyo kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Mwita Waitara (Chadema).

Kesi hiyo imesikilizwa katika mahakama hiyo mbele ya Fatuma Mseng ambapo Silaa alifika kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Dk. Kyuka ameieleza mahakama kuwa, utoaji ushahidi mahakamani lazima kuzingatiwe sheria na kwamba, Silaa hakuenda kwa msajili wa mahakama kwa hatua za awali za ushahidi.

Akitoa utetezi wake Masumbuko Lamwai, Wakili wa Silaa amesema kuwa, bado kuna haja ya mahakama kukubali ushidi huo kutokana na Silaa kuhusika kwake.

Madai ya Silaa katika shauri hilo ni kuwa, matokeo ya uchaguzi yalitangazwa tarehe 28 Oktaba saa 10 alfajiri mwaka jana ambapo yeye alipewa hati tofauti ya matokeo halisi.

Uamuzi kuhusu nafasi ya Silaa kuwa shahidi kwenye kesi hiyo utatolewa kesho.
 
rufaa akishinda wa CCM mahakama zinapendelea, ila akishinda wa CHADEMA hakuna malalamiko, duuh kazi ipo tz.
Kweli wewe umepiga Kitwanga Lager! Hujaelewa hata kinachozungumzwa unakimbilia kukomenti!
 
Slaa dogodogo wa mbeleko naona familia ya kwanza haikusaidia kukupa ushindi kama sehemu zingine walizochakachua ikiwemo wa Tumbili!.....
 
Yamemlemea sana Jerry

Mwanahabari Huru, ninafahamu unamacho ya kuona picha hata kama kusoma umesahau kwa sababu ha kujua lugha nyingi. Hizi kesi zote ni sarakasi tu. Hakuna cha proceedings, hakuna cha ushahidi/mashahidi wala cha nani sijui hakufanya submission na nini. Hizi ni sanaa tu.

KESI ZOTE ZA UCHAGUZI ZINAAMULIWA KWA MATAKWA YA CCM!. KINACHOZINGATIWA NI MADHARA YA MSHINDI WA CHADEMA KWA CCM AKIWA BUNGENI, MAHTAJI YA CCM KATIKA JIMBO LILNALOGOMBEWA NA UMUHIMU WA MGOMBEA WA CCM KAMA CCM WATAKAVYO.

Hawa wanaoendesha kwa uahirisha, sijui kukataa ushahidi, sijui kufanya nni ni mbwembwe tu za kuonyesha kwamba kulikuwa na kataratibu, LAKINI KESI ZOTE ZA UCHAGUZI ZIMESHAHUKUMIWA.
 
Back
Top Bottom