aretaskimario
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 527
- 248
Mm kuna time nafanya kitu ambacho ni mara ya kwanza kukifanya maishani mfano kusafiri, au mtu ananipa story tu hata kabla hajamalizia naona hadi move yake yote yan hadi najishangaa mwenyewe. Au naweza kutulia mahali nikiwa nimeinamisha kichwa nafikiria tu mambo yangu ghafla najisahau naona kitu kingine mfano namwona mtu fulani anakuja kwenye mawazo alafu nikinyanyua kichwa tu namwona huyo mtu anakuja kweli na jinsi niluvyomwona anakuwa ivoivo.unajua brains zetu zinatunza sana kumbukumbu......personally kuna vitu vingi sana vimeshawahi kujirudia au nimehisi kama nilishafanya kabla ila unashindwa kukumbuka ni lini na ilikuwajekuwaje and kuna times huwa nahisi kama vile siku imejirudia ila yote tisa. ...kumi ni imani zetu zinatujenga tofauti sana so kiukweli siri ya baada ya kifo wanaujua ni waliotangulia katika haki.........maada tata sana hii
Mm kuna time nafanya kitu ambacho ni mara ya kwanza kukifanya maishani mfano kusafiri, au mtu ananipa story tu hata kabla hajamalizia naona hadi move yake yote yan hadi najishangaa mwenyewe. Au naweza kutulia mahali nikiwa nimeinamisha kichwa nafikiria tu mambo yangu ghafla najisahau naona kitu kingine mfano namwona mtu fulani anakuja kwenye mawazo alafu nikinyanyua kichwa tu namwona huyo mtu anakuja kweli na jinsi niluvyomwona anakuwa ivoivo.
kwanza kwa maelezo uliyogusa kuhusu yesu na eliya uko mbali sana na ukweli. Na ulipomalizia kwa kusema nitakumbuka nikifa, kwanza nianze kwa kupinga hilo kutoka katika biblia ambayo hata wewe umejaribu kuitumia kama muongozo, soma mhubiri 9:5-6 uone biblia inavyozungumzia kuhusu wafu. Pia hata mimi sina kumbukumbu kama nilipozaliwa ilikuwa mara yangu ya kwanza au nilishawahi kuzaliwa hapo kabla na nikafa. Au jiulize mwenyewe, je ulishawahi kuishi kabla? Na kama bado, je unataka kusema watu waliokuwepo kipindi hicho hawakuwa wametosha mpaka kuwe na ulazima wa wengine kuzaliwa? Ilihali kwa maelezo yako, ingewezekana hao hao wa zamani, ndio wangekuwa wanazaliwa, wanakufa kisha wanazaliwa tena.
jamani tubishe ama tukubali ila hili jambo lina ukweli fulan maana hii hali si kawaida japokuwa nimegundua hii hali ya kuhisi vitu kujirudia kuna muda inaapotea kabisa na haitokei kila siku. .........binafsi nasapoti kwa mikono miwili kwamba kuna something fishy kuhusu hii maada inawezekana kabisa ikawa true maana kama mpo mnaobisha then hebu nielezeeni ni nini haswa...........kuna siku nilishuhudia ajali pale manzese ila cha ajabu nilipoiona tu kabla hata sijaambiwa wameumia wangap mimi tayari nilikuwa najua wameumia wangap na nani aliekufa na cha ajabu zaidi eti nakumbuka hadi hiyo ajali iliilivyotangazwa kwenye tv mtangazaji alifanya nini kwenye hicho kipindi........kiukweli niliamua tu kuacha kufuatilia haya mambo baada ya kuona sipati majibu ama maelezo ya kueleweka kuhusu hali inayonitokea ila ni wazi hili jambo lina ukweli fulani
Ni sawa bills kwan hapo ina maanisha hilo tukio lilifanyika kabla.... Au roho iltumwa mbele kujua kilichopo?
Hayo ni majinni maovu yanacheza na akili yako.
hivi ile hali ya kuwa usingizini na kuota ndoto usiku nayo ni majini?