Ushabiki wa vyama wawapofusha wabunge wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushabiki wa vyama wawapofusha wabunge wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 28, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akibadilishana mawazo
  na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, bungeni.

  WABUNGE amesahau wajibu wao?
  Inawezekana wamesahau wajibu wao kutokana na ushabiki kwa vyama vyao vilivyowaingiza bungeni; hivyo kuifanya Serikali ishindwe kupata ushauri wa kina kutoka kwa chombo hicho. Malumbano ya wabunge sasa yameacha kuegemea maslahi ya Taifa badala yake yanaenda kwenye ushabiki wa vyama. Hali hii inafanya hata kama ni jambo zuri limetolewa na upande mmoja wa wabunge wale wa upande wa pili wanashindwa kuunga mkono.

  Tumeshuhudia wakati wa mjadala wa kupitishwa kwa Sheria ya Fedha ya mwaka 2011. Kuna mambo mengi ambayo yaliwasilishwa na wabunge lakini kutokana na mivutano yao ya kikambi mapendekezo ya Serikali yalipita kirahisi bila ugumu wowote. Kwa mfano pendekezo la kufuta misamaha ya kodi ambalo lililetwa na Serikali bungeni, awali wabunge wa pande zote mbili walilipinga kwa nguvu zote, lakini wakati wa kupitisha vifungu vya muswada huo wabunge wa CCM walionekana kunywea na kuyakubali mapendekezo ya Serikali. Walinywea kwa sababu mapendekezo ya marekebisho ya muswada huo mengi yalifanywa na wabunge wa Kambi ya Upinzani, John Mnyika wa Ubungo ; na Tundu Lissu wa Singida Mashariki. Hoja zao nyingi zilipingwa na Serikali.

  Wabunge hao walitaka misamaha hiyo, iondolewe kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza kwenye Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZ); pamoja na misamaha kwa wawekezaji wa madini na mafuta, kwa maelezo kuwa misamaha hiyo ndio ambayo imeliangamiza Taifa. Wakati kwenye mjadala wabunge wakiwemo wa CCM, walipinga misamaha hiyo. Lakini, wakati wa kupitisha vifungu hivyo, kwa vile tu marekebisho hayo yaliletwa na Mnyika na Lissu wa upinzani na kukataliwa na Serikali, wabunge wa CCM hawakuthubutu kuhoji zaidi.

  Eneo moja tu ambalo wabunge wa CCM walihoji ni kuziondolea uwezo halmashauri za wilaya, kukusanya kodi kwa kipindi cha miaka 10, jambo ambalo lilikataliwa na Wabunge wa CCM na kuungwa mkono na wapinzani. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, wakati akijibu hoja za wabunge wa upinzani alionekana kuzijibu kwa kejeli, lakini baadaye akawaambia wabunge wa CCM “niwahakikishieni wabunge wa CCM ambao wanapinga misamaha hii isitolewe kuwa Serikali yao ina nia nzuri ya kuiweka hivyo wakubaliane na mapendekezo hayo ya Serikali.”

  Hata pale aliposimama Mnyika na kuwasilisha mapendekezo kuwa kama Serikali inang’ang’ania kutoa misamaha hiyo kwa wawekezaji, basi iwepo miaka mitano na sio 10 na baadhi ya wabunge wa CCM kuunga mkono hoja hiyo, lakini Serikali ilisimamia mapendekezo yake. Ndipo Mnyika akasimama na kuwaambia wabunge kuwa “ufike wakati wabunge wengi kwa kuwa tumependekeza iwe miaka mitano, basi tufanye kazi yetu ya kutunga sheria ; na sio kutumiwa kama rubber stamp (mhuri) na Serikali. Kwamba Serikali inaleta mapendekezo yao, lakini wabunge wanashindwa kutunga sheria wanayoona ina maslahi kwa Taifa.”

  Baada ya maneno hayo ya Mnyika, kama kawaida ya kanuni, Spika wa Bunge akawauliza wabunge wanaokubaliana na marekebisho hayo ya Mnyika ya miaka mitano badala ya 10, waseme ‘ndio’, wakasema wachache wa Kambi ya Upinzani ; na alipouliza wale ambao hawakubaliani na mapendekezo hayo ya Mnyika na wanakubaliana na yale ya Serikali, wabunge wote wa CCM wakasema ‘ndio’ kwa Serikali. Ni katika hali hiyo, nasema kwamba wabunge wa CCM kwenye michango yao, walionesha wazi kuwa wanapinga uamuzi wa Serikali wa kutoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji hao. Lakini, baada ya Serikali kung’ang’ania uamuzi wake, wakanywea na wakakubaliana na mapendekezo yote ya Serikali. Katika hali ya namna hii, tunaona kuwa wabunge wenye wajibu wa kutunga sheria nzuri zenye maslahi kwa wananchi, wanaweza kujikuta wanakuwa mihuri ya kubariki mapendekezo ya Serikali, kwa sababu tu ya ushabiki wa vyama vyao. Wanaona kwamba wakikubali watakuwa wamewapa ‘ujiko’ wabunge wa upinzani. Kazi ya Serikali ni kuleta mapendekezo mbele ya Bunge, lakini kazi ya kutunga sheria ni kazi ya Bunge. Iwapo wabunge wataendeleza ushabiki wa vyama vyao, kuna hatari kuwa na sheria mbaya ambazo baadaye tutazijutia.

  Yawezekana wabunge wa CCM, walipinga mapendekezo ya upinzani, kwa vile kambi hiyo pia iliingiza tambo wakati ikiwasilisha mapendekezo yao kwenye muswada huo. Naibu Msemaji wa Kambi hiyo katika masuala ya Fedha, Christina Mughwai, alitamba kuwa yale mambo ambayo Serikali iliyarekebisha kwenye bajeti ya Serikali, yalitokana na kelele za wapinzani pekee, hivyo akasema kambi hiyo imedhihirisha kuwa inaweza. “Tumedhihirisha kuwa tunaweza,” alisema Christina na kutaja mambo kadhaa, ambayo Serikali imesalimu amri na kuyarekebisha kwenye bajeti, kwa sababu yalitolewa na Kambi ya Upinzani. Hivyo, kauli hii inadhihirisha kuwa wabunge hawa wana ushabiki wa vyama vyao na wamesahau majukumu yao, kuwa wanatakiwa waangalie maslahi ya Taifa na ya wananchi wa Tanzania katika kutunga sheria zao.

  Labda, niwakumbushe tu kuwa wakati wakichangia muswada huo, wabunge hao walisema misamaha ya kodi, inayotolewa na Serikali kwa wawekezaji wa madini, mafuta na maeneo huru ya uwekezaji yanaliangamiza Taifa. hao wakasema wema wa kuzipatia kampuni tajiri za nchi za Magharibi misamaha ya kodi, unatajirisha kampuni hizo na kuiacha Tanzania ikiogelea kwenye umasikini. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) katika mchango wake kwenye Muswada huo wa Sheria ya Fedha, alishangaa kuwa pamoja na misamaha kwenye sekta ya madini kuiangamiza Tanzania, bado Serikali haijajifunza badala yake inatangaza kutoa misamaha mingine ya kodi.

  Alisema tume mbalimbali zilizoundwa na Serikali katika kutafakari namna sekta ya madini, inavyochangia kwenye pato la Taifa na wakapendekeza misamaha hiyo ya kodi kufutwa, lakini bado Serikali sio sikivu inaendelea kuwakumbatia wawekezaji. “Nchi hii inaangamizwa na misamaha ya kodi kutokana na wema tunaozifanyia kampuni tajiri, dhahabu imeshindwa kutunufaisha kwa misamaha hii iweje leo tena tutangaze kutoa misamaha kwa madini na maeneo huru ya uwekezaji? Alihoji. Alisema badala ya kuondoa misamaha hiyo, Serikali inaongeza misamaha. “Inabidi sisi wabunge tupinge ili tumtii Mungu…kwa nini hatujifunzi kutokana na makosa yetu? Alihoji. Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), alisema mataifa makubwa sio kwamba yanaipenda Tanzania bali yanapenda rasilimali zetu hivyo kutoa misamaha kwa kampuni za kigeni ni kuinyima Serikali mapato.

  “Iweje kila kitu tunatoa misamaha ya kodi, huruma hii inatuponza,” alisema Zambi na kutaka misamaha hiyo ya kodi ifutwe kwani kampuni hizo zinafanya biashara na kupata faida kubwa. Serikali iache kutoa misamaha hiyo na mwekezaji anayetaka aje kuwekeza asiyetaka na asije. Alisema umefika wakati wa Tanzania kufaidika na rasilimali zake na sio kuwanufaisha wawekezaji pekee. Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), alisema naye alipinga misamaha kwa wawekezaji hao na akataka mpango huo usitishwe mara moja. Hatua hiyo ya wabunge ilitokana na hotuba ya Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima wakati akiwasilisha Muswada wa Fedha wa 2011 kutangaza uamuzi wa Serikali wa kusamehe ushuru wa stempu wakati wa uhamisho wa mali ndani ya maeneo ya uwekezaji, kwa ajili ya mauzo ya nje ya nchi na maeneo maalumu ya uwekezaji kwa ajili ya mauzo ya nje.

  Silima alitangaza pia kusamehe ushuru wa stempu wakati umiliki wa mali, unapohamishiwa katika chombo maalumu cha kutekeleza na kusimamia uzalishaji wa kipato kwa madhumuni ya kutoa dhamana zinazotegemea mali husika ambayo umiliki wake umehamishwa. Alisema lengo la kutoa misamaha hiyo ni kuhamasisha miradi ya uwekezaji inayohitaji fedha nyingi kama miradi ya barabara, madaraja, nishati na maji. Eneo lingine ambalo Naibu Waziri huyo alitaja ni kusamehe ushuru wa mafuta ya petroli unaotozwa kwenye mafuta yanayotumika kuendesha meli, na vifaa vingine vinavyotumika katika utafiti wa mafuta na gesi. Alisema maombi hayo ya msamaha, yatatolewa kupitia tangazo la Serikali kwenye Gazeti la Serikali. Alisema maombi ya msamaha yatahakikiwa na kupitishwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kabla ya kuwasilishwa Wizara ya Fedha.

  Silima alisema hatua hiyo, inalenga katika kutoa unafuu wa gharama kwa kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta na gesi. Pia alisema wataruhusu kampuni za madini kununua mafuta, ambayo hayajalipiwa kodi. Lakini ni wabunge hawa ambao hoja zao zilikataliwa na Serikali, hawakuweza kuhoji zaidi, badala yake walikubaliana na mapendekezo yote ya Serikali. Kwa hiyo ile misimamo yao, kuwa misamaha ya kodi inaliangamiza Taifa, waliiweka pembeni na kufuata upepo wa Serikali ya chama chao.

  Hilo ndilo Bunge letu la sasa.

  Habari Leo
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wa article hiyo labda watakusikia manake wabunge wa CCM wameziba masikio wanajiwakilisha wenyewe
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  wabunge wa ccm wameathiriwa na bange, naam moshi wa bange kwenye operation uchomaji mashamba ya bange ambayo huongozwa na polisi ambao wamedata.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nimeshangaa kuona hata gazeti la serikali limeona kasoro hiyo kwa wabunge wa CCM, nadhani ndio maana semina elekezi zinavyoelekeza
   
 5. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hakuna wabunge wanaongoza kwa kuwa na vitambi km wa magamba, hakuna wabunge wanaongoza kwa vipara kama magamba, hakuna wabunge wanaongoza kwa mawazo mgando kama magamba, hakuna wabunge wanaongoza kuwa vilaza kama magamba, hakuna bunge la kijinga kama hili la tanzania, they are but a rubber stamp. Magamba MPs' are DOGS in the MANGER,
   
 6. MANI

  MANI Platinum Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Tatizo na la wabunge wa CCM wamesahau wajibu wa bunge ni kusimamia serekali wao badala ya kusimamia serakali wameamua kuwa serekali na kwa mtaji wao wa wengi hapo bungeni bunge haliwezi kamwe kuisimamia serekali mpaka hawa CCM wapungue hapo bungeni.
   
 7. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  hapo bungeni ni pamba tu masikioni kama mbunge si wachama kinachokuhusu, na ushauri ukifanikiwa kuingia sikioni basi mbunge anahakikisha unatokea sikio la upande wa pili hata kama ushauri utasaidia na wananchi waliomtuma. kazi ipo
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni hao na kuwa na wabunge wengi wa CCM ni dhambi sana katika taifa letu na pia ni hasara sana kwa manufaa ya taifa hili!! Saa inakuja na wala sio Mbali sana
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe 100% wabunge wa CCM ni golikipa wa serikali
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Wabunge wa CCM wapo kimaslahi yao zaidi.
  Wanahofia endapo hawatoenda sawa na misimamo ya chama chao huenda wakakosa nafasi ya kugombea temu ijayo na hivyo kukosa ulaji na posho kede kede.
   
 11. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  To be honest zaidi ya asilimia 98 ya wabunge wa CCM hawajui wajibu wao Bungeni...matokeo ndio mikataba mibovu ktk maeneo ya umeme na madini etc.

  Wabunge wa CCM hawa-question issue that matters most...utasikia wananchi wangu wamenituma kuipongeza serikali...kisha anaanza kusoma list ndefu ya matatizo jimbo kwake.

  Ukiacha hilo kuna hiki kitendo cha cha kinafiki..eti kumshukuru Mungu, wanajimbo na kuwapongeza viongozi wa serikali. Kwa hili ni poor leadership ya Bunge ndio inali-entertain. Nafikiri thinking ya Spika ni kwamba she is doing some good thing for the government. Wrong infact anachangia kuiweka serikali pabaya zaidi mbele ya watanzania

  Mwisho wa siku hoja hazifanyiwi improvements zinapita kwa kelele za ndio...ni kutokana na uppuzi kama huo wabunge wanajikuta wamepitisha mikataba ya Ki-Karl Peters. Imagine juzi wanalazisha taxi holdays kwa wawekezaji kuwa 10yrs..stupid.
   
Loading...