Ushabiki wa timu ya taifa vs ushabiki wa klabu

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Wakuu leo tuongee kuhusu mambo ya mpira na ushabiki, kwa kweli kwa maoni yangu hivi club huwa inamuwakilisha nani, tumekua na washabiki wengi sana wa club kuliko washabiki wa timu ya taifa.

Club kama club ni timu za kibiashara ambapo mtu yeyote kutoka sehemu yoyote duniani anaweza kuja kuchezea club japokua kuna namba ndogo ya wazawa ipo ndani.

Watu wanachukulia poa sana timu ya taifa, lakini timu ya taifa ndo inakuwakilisha, kisaikolojia mtu anatakiwa awe connected na timu ya taifa kuliko club, hata ushabiki na nguvu ya uboreshaji unatakiwa uelekezewe kwenye timu ya taifa, club haina identity, kwenye club anaweza kuchezea mtu kutoka marekani, Senegal, England, brazil, na club ikipata mafanikio kunakua hakuna positive psychological impact kwa wazawa, kwann serikali isielekeze nguvu kwenye timu ya taifa hasa.

Timu ya taifa ni identity moja kubwa sana, watu hawajui umuhimu wa psychological impact timu inayokuwakilisha kupata ushindi. club kama club ni timu ya kibiashara, club ikishinda inamnufaisha mmiliki, lakini timu ya taifa ikishinda inampa mwananchi ujasiri na sifa ambayo at the end of the day itampa nguvu kufanya mambo makubwa Zaidi, hasa kwa young generation.

Ni mtazamo tu, je wewe mwana jamvi una maoni gani kuhusu hilo? Elezea hasira zako humu nasi tupate kusikia mawazo
 
Back
Top Bottom