Asanteni sana wote kwa maelezo hayo. Baada ya SaidSabke kuniambia ni wimbo wa Bongo Flava, nikaenda YouTube na nikaweza kuuangalia. Ni wimbo mzuri. Asanteni sana, maana kwa wengine ambao hatupo nyumbani, misemo mingi inatupita. Wakati uliopita kulikuwa na forum ya Tanzanet ambapo kulikuwa kunawekwa misemo mipya. Hii ilitufanya wengi tuwe 'uptodate' na mabadiliko ya lugha.