USD 600 million zilizokopwa na JK zimefanya shughuli gani za maendeleo?

Nov 5, 2013
16
2
Magufuli: " Karibu miezi sita sasa imepita (tangu bajeti ya 2015/2016 ipitishwe) hakuna fedha yoyote ya maendeleo iliyoenda kwenye wizara yoyote. Fedha yote tulikuwa tunaitumia kwa ajili ya mishahara na vitu vingine."

Balozi Sefue atueleze fedha zile za Mkopo USD 600 Mil tangu mwaka 2012/2013 hadi mwaka huu wa fedha 2015/2016 zimeenda kufanya shughuli gani ya maendeleo kama alivyowahi kusema?

Watanzania tumuulize Balozi Sefue ambaye ni kiongozi mwanamizi katika serikali ya JK na sasa Magufuli atupe majibu yanayoeleweka juu ya fedha hizo?

Akina Mheshimiwa Zitto na wanasiasa wengine mliokuwepo katika bunge lilopita, tupeni majibu ya fedha zile na shughuli gani ya maendeleo iliyofanywa?

Magufuli " Mwezi huu (Dec) ndio zimetolewa Bil 120 kwa ajili ya shughuli za maendeleo lakini kwa miazi yote tangu bajeti ipitishwa ilikuwa haijatoka hata senti tano." Tumuulize Rais, maendelo hayo ni yepi haswa?

Tumuulize JK "Mzee wa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!" ilikuwaje tangu mwezi wa Saba hadi anakabidhi nchi Nov hajafanya lolote la maendeleo kwa mwaka huu wa fedha?
 
Hayo maswali magumu sana kujibiwa mkuu.... ile bajeti pale bungeni inaonekana ilikuwa kiini macho... mkosamali aliisha wauliza mantiki ya bunge la bajeti kama hamna pesa.... ccm ni ileile....
 
Hiyo pesa imejenga nyumba za nyumba ndogo za michepuko, kununua magoli mikono Kipindi cha kampeni
 
Ajabu hata zitto alipokuwa anahojiwa na DW-SWAHILI Naye aliuliza je pesa hiyo kweli ilienda serikalini? JK anajua na Kitilya anajua! Zitto ulikuwa PAC tunataka ujijibu!
 
Haya maswali yatakuja kuibua mengi mpaka watu wataona Bandari na TRA kumbe ulikuwa mchezo wa kitoto tuu. Ndio maana nimejiuliza sana kwa nini Chenge aliita ile dola milioni moja ya Kule Uingereza vijisenti? Tena kwa msisitizo na bila hofu?
Nikuwa alikuwa anajua watu wanapesa kiasi gani za wizi na ufisadi.
 
Si ajabu 75% ya hiyo pesa imeliwa na mambweha na mpaka muda huu hawajafuta midomo.
 
Pamoja na udhaifu wake mkubwa, Speaker alianza kuliona hilo hadi akaunda kamati ya bunge ya budget. Undwaji wake ulikuwa na figisufigisu baada ya kumteua "Mtemi" Chenge kuwa mwenyekiti badala ya kuwaachia wajumbe wachague mwenyekiti wao kama ilivyo kawaida.

Kenya kwa sasa wana tatizo kama hilo. Wamekopa mabiilion (Eurobond) lakini inaelekea wajanja wametafuna billion 140 za Kenya.

Ni vyema tukajua hizo US Dollar 600m zilifanya nini kama sio kugharimia safari za Kikwete.
 
ulijuaje hajafanya chochote? hizo barabara zilizokuwa zikiendelea kujengwa na miradi mingine unafikiri ilikuwa nini? hukuona miradi mbalimbali mfano ya maji ikiwa kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji?

Magufuli: " Karibu miezi sita sasa imepita (tangu bajeti ya 2015/2016 ipitishwe) hakuna fedha yoyote ya maendeleo iliyoenda kwenye wizara yoyote. Fedha yote tulikuwa tunaitumia kwa ajili ya mishahara na vitu vingine."

Balozi Sefue atueleze fedha zile za Mkopo USD 600 Mil tangu mwaka 2012/2013 hadi mwaka huu wa fedha 2015/2016 zimeenda kufanya shughuli gani ya maendeleo kama alivyowahi kusema?

Watanzania tumuulize Balozi Sefue ambaye ni kiongozi mwanamizi katika serikali ya JK na sasa Magufuli atupe majibu yanayoeleweka juu ya fedha hizo?

Akina Mheshimiwa Zitto na wanasiasa wengine mliokuwepo katika bunge lilopita, tupeni majibu ya fedha zile na shughuli gani ya maendeleo iliyofanywa?

Magufuli " Mwezi huu (Dec) ndio zimetolewa Bil 120 kwa ajili ya shughuli za maendeleo lakini kwa miazi yote tangu bajeti ipitishwa ilikuwa haijatoka hata senti tano." Tumuulize Rais, maendelo hayo ni yepi haswa?

Tumuulize JK "Mzee wa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!" ilikuwaje tangu mwezi wa Saba hadi anakabidhi nchi Nov hajafanya lolote la maendeleo kwa mwaka huu wa fedha?
 
Hizo watu wakianza kuzipiga hata kabla hazijafika Bongo, sio ajabu ni miongoni mwa yale mabilioni Zitto alikuwa anapigia kelele
 
Shamba la bibi hili tuokoe eee magufuli situtakuombea tu watanxania tupo nyuma yako
 
Back
Top Bottom