Usawa wa kijinsia ni ajenda ya kitapeli

NYAMUHANZI

Senior Member
Apr 7, 2017
187
388
Habari waheshimiwa!

Hapo mwanzo kulianza kuwa na harakati za haki sawa, binafsi nilikubaliana nazo maana kulikuwa na baadhi ya wanawake wanadhulumiwa haki zao kutokana na sheria kandamizi zilizokuwepo wakati huo. Wanaharakati walipambana na hatimae sheria kandamizi zikaondolewa na zinaendelea kuondolewa kila zinapobainika (maana ni jambo endelevu).

Sasa baadhi ya wanaharakati wakaona ili wasikose kazi za kufanya wakaamua kuanzisha ajenda za usawa wa kijinsia. Binafsi mimi naona hii ajenda ya usawa wa kijinsia imekaa kitapeli maana msingi wa tofauti kati ya Mwanaume na Mwanamke ni maumbile yetu hasa upande wa viungo vya uzazi.

Mtoto wa kike hawezi kuwa na hisia za kumpa mtu mimba na Mtoto wa kiume hawezi kuwa na hisia za kushika ujauzito labda awe kichwani hazimtoshi, hivyo basi naamini haitakaa itokee sisi wote kuwa sawa kijinsia maana Mungu aliyetuumba kwa jinsia tofauti kwa kila kiumbe hakuwa mjinga bali alitaka tuendelee kuzaliana na kupanga maisha kwa kutumia akili alizotupa sasa ikiwa sisi tunataka kuwa sawa kijinsia ina maanisha tusizaliane wala kutegemeana.

Hayo ni maoni yangu, karibuni kwa michango ya mawazo.
 
Back
Top Bottom