Usanii wa TCRA na mfumo wa Digitali.

Usanii wa TCRA na mfumo wa Digitali.

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
552
*Kwa muda sasa Wananchi wa tanzania wamehimizwa kwa kiasi kikubwa sana na mamlaka ya mawasiliano(TCRA) wachukue hatua ya kununua ving'amuzi kwa ajili ya kuhamia mfumo wa Digitali.

*Tarehe 31/12/2012 saa sita usiku ilikuwa ni siku rasmi ya kuzimwa mitambo ya Analogia kupisha mfumo mpya wa Digitali.
Lakini yaliyotokea na yanayoendelea kutokea ni usanii mkubwa.

*Maafisa wa TCRA wamekuwa wakizunguka nchi nzima wakiwapa watu hadithi tamu(njozi?) inayoitwa Digitali, yaani wakisema huu ni mfumo NAFUU(Cheap and Easy), UBORA(Picha na sauti), MPANA(Large Coverage and Multi Channels)
Lakini badala yake wananchi wengi wameshuhudia mambo ya tofauti kabisa, kwa mfano
1/GHARAMA KUBWA(Ununuzi wa Ving'amuzi na gharama zingine za malipo)

2/UHAFIFU(Upatikanaji wa picha na sauti umekuwa na matatizo mpaka kufikia ulazima wa kutumia antenna tena)

3/UFINYU(Bado sehemu chache sana ndio zinazoweza kupata hayo matangazo, na kuna local channel nyingi sana ambazo haziko hewani tena!!)

*Kuna sarakasi nyingi sana ambazo TCRA inaendelea kuzifanya sasa, kwa mfano mpango wa kuzima mitambo ya Analogia ulikuwa wa nchi nzima kwa wakati mmoja ila sasa ni kwa awamu tena umeanzia Dar pekee(Majaribio?) kwanini?
 
Mara nyingi mwanzo huwa ni mgumu lkn mwisho wa siku tutazoea na kusahau matatizo yote. Nawaunga mkono tcra tena nataka wahamie na kwenye simu haraka iwezekanavyo.
 
Mkuu huu sio mwanzo bali ni mwendelezo, kumbuka mfumo wa Digitali ulianza toka mwaka 2010, lakini hali bado ni mbaya sana.

Tutazoea kitu gani? Gharama kubwa? Uhafifu wa matangazo? Uduni wa matangazo?
 
kichoongelewa ni garama kubwa na huduma mbovu,tofauti hali halisi hatuitaji mazoea,je unaweza kula sumu na ukasema nitazoeya?
 
TCRA wameleta chaos!
Hili ni pigo jipya kwa watawala.

Digitali ya kweli ni 2015 ....CDM(Digital)
CCM(Analogy)
 
Whether kwa kujua au kutojua, digital migration has enhanced digital divide kwani ni watanzania wachache sana ambao wataweza afford kununua ving'amuzi, let alone afford extra costs za umeme to power ving'amuzi; unless serikali ije na some sort of of subsidy kwa wananchi wasio na uwezo au itengeneze mazingira yenye ushindani mkali zaidi ili bei ya ving'amuzi iwe chini, otherwise the majority wont enjoy digital justice, watakuwa ni watu wa kuhadithiwa tu bungeni kumejadiliwa nini n.k;

Licha ya umuhimu wa digital migration, bila ya uangalifu, suala hili litakuwa politicized na kupewa tafsiri kwamba ni mpango wa serikali to control media kwa umma; kwa vile sehemu kubwa ya umma ni illiterate na pia kwa vile serikali haikufanya awareness raising ya kutosha kama kwa mfano wenzetu wa Kenya, sehemu kubwa ya umma utakubaliana na hoja nyingi za kisiasa katika hili;
 
*Kwa muda sasa Wananchi wa tanzania wamehimizwa kwa kiasi kikubwa sana na mamlaka ya mawasiliano(TCRA) wachukue hatua ya kununua ving'amuzi kwa ajili ya kuhamia mfumo wa Digitali.

*Tarehe 31/12/2012 saa sita usiku ilikuwa ni siku rasmi ya kuzimwa mitambo ya Analogia kupisha mfumo mpya wa Digitali.
Lakini yaliyotokea na yanayoendelea kutokea ni usanii mkubwa.

*Maafisa wa TCRA wamekuwa wakizunguka nchi nzima wakiwapa watu hadithi tamu(njozi?) inayoitwa Digitali, yaani wakisema huu ni mfumo NAFUU(Cheap and Easy), UBORA(Picha na sauti), MPANA(Large Coverage and Multi Channels)
Lakini badala yake wananchi wengi wameshuhudia mambo ya tofauti kabisa, kwa mfano
1/GHARAMA KUBWA(Ununuzi wa Ving'amuzi na gharama zingine za malipo)

2/UHAFIFU(Upatikanaji wa picha na sauti umekuwa na matatizo mpaka kufikia ulazima wa kutumia antenna tena)

3/UFINYU(Bado sehemu chache sana ndio zinazoweza kupata hayo matangazo, na kuna local channel nyingi sana ambazo haziko hewani tena!!)

*Kuna sarakasi nyingi sana ambazo TCRA inaendelea kuzifanya sasa, kwa mfano mpango wa kuzima mitambo ya Analogia ulikuwa wa nchi nzima kwa wakati mmoja ila sasa ni kwa awamu tena umeanzia Dar pekee(Majaribio?) kwanini?

vema basi usanii wenyewe uvutie, wanaonesha sanaa ndooogo hata mazoezi hawajafanya...aibu
 
Whether kwa kujua au kutojua, digital migration has enhanced digital divide kwani ni watanzania wachache sana ambao wataweza afford kununua ving'amuzi, let alone afford extra costs za umeme to power ving'amuzi; unless serikali ije na some sort of of subsidy kwa wananchi wasio na uwezo au itengeneze mazingira yenye ushindani mkali zaidi ili bei ya ving'amuzi iwe chini, otherwise the majority wont enjoy digital justice, watakuwa ni watu wa kuhadithiwa tu bungeni kumejadiliwa nini n.k;

Licha ya umuhimu wa digital migration, bila ya uangalifu, suala hili litakuwa politicized na kupewa tafsiri kwamba ni mpango wa serikali to control media kwa umma; kwa vile sehemu kubwa ya umma ni illiterate na pia kwa vile serikali haikufanya awareness raising ya kutosha kama kwa mfano wenzetu wa Kenya, sehemu kubwa ya umma utakubaliana na hoja nyingi za kisiasa katika hili;
bado naona ni kosa jingine la ccm.yaani tumekurupukia sera bila kuangalia mazingira,elimu,uchumi wa wananchi wetu ambao wengi ni wakulima.

Digitali kwa manufaa ya nani?
 
kichoongelewa ni garama kubwa na huduma mbovu,tofauti hali halisi hatuitaji mazoea,je unaweza kula sumu na ukasema nitazoeya?
 
Hili swala analogy to digital migration ni aibu kubwa kwa serikali. inaonekana hata masuala ya kawaida kabisa hawawezi. Baadae utasikia tumejaribu, tumeweza! kila siku kujaribu
 
Jamani, swala la digital halikwepeki, ni swala la mda tu. analogy is an old tech na hakuna sababu ya kuing'ang'ania. dunia yote inaenda huko na sisi ni lazima tuende huko.

ila kinachonikera mimi ni kwanini TCRA hawawapi waTz correct information badala yake wanakuwa mawakala wa star times?hii inanikera sana ... setelite dishes are cheaper than all these rubish star times na am sure kwa kila anayeweza nunua TV anaweza nunua ungo wake akapata free TVs zaidi ya channel hamsini mbalimbali.

TCRA wanafumbafumba hapa na kuwapikia debe star times ni nini hiki?
 
*Kwa muda sasa Wananchi wa tanzania wamehimizwa kwa kiasi kikubwa sana na mamlaka ya mawasiliano(TCRA) wachukue hatua ya kununua ving'amuzi kwa ajili ya kuhamia mfumo wa Digitali.

*Tarehe 31/12/2012 saa sita usiku ilikuwa ni siku rasmi ya kuzimwa mitambo ya Analogia kupisha mfumo mpya wa Digitali.
Lakini yaliyotokea na yanayoendelea kutokea ni usanii mkubwa.
Mkuu hapa ungetufafanulia usanii upo wapi? mikoa iliotajwa analogia si imezimwa au?
*Maafisa wa TCRA wamekuwa wakizunguka nchi nzima wakiwapa watu hadithi tamu(njozi?) inayoitwa Digitali, yaani wakisema huu ni mfumo NAFUU(Cheap and Easy), UBORA(Picha na sauti), MPANA(Large Coverage and Multi Channels)
Lakini badala yake wananchi wengi wameshuhudia mambo ya tofauti kabisa, kwa mfano
1/GHARAMA KUBWA(Ununuzi wa Ving'amuzi na gharama zingine za malipo)

2/UHAFIFU(Upatikanaji wa picha na sauti umekuwa na matatizo mpaka kufikia ulazima wa kutumia antenna tena)

3/UFINYU(Bado sehemu chache sana ndio zinazoweza kupata hayo matangazo, na kuna local channel nyingi sana ambazo haziko hewani tena!!)
*Swala la gharama nadhani elf 9 kwa mwezi wamejitahidi sana maana mfumo huu si bure kama analogia na pia ving'amuzi havitolewi bure jamani wala si kazi ya TCRA kupanga bei,.....ni swala la muda tu bei sokoni itabalance tu...kumbua mobile zilipoanza kuingia
*Swala la ubora wa sauti na picha kiukweli huwezi kabisa kulinganisha na analogia ukiondoa kasoro ndogo ndogo za matangazo kukata kata kutokana na ugeni wa mfumo
*Swala la large coverage and multi channel pia si usanii, hapa inapaswa kujua kuna ving'amuzi vya fta vinapokea kwenye minara kwa antena na pia kuna ving'amuzi vinapokea kwa setelaiti unavyoweza kuona ukiwa popote pale nchini na channel ni nyingi ingawa zinaweza zisiwe za kukuvutia
*Swala la antena halimaanishi hii ni analogi au digitali
*Swala la local channel kutokuwa hewani ni wao kujiunga na warusha matangazo tu, maana TCRA wametoa mwongozo stations 5 ambazo ni itv eat startv tbc na channel 10 ni lazima zionyeshwe kwenye ving'amuzi vyote tena bure kabisa na ndio maana ukienda zuku,startimes na ting unazikuta
stations zingine zitachagua zenyewe king'amuzi cha kujiunga kwa makubaliano ya kibiashara
*Swala la kuzima analogia nchi nzima kwa wakati mmoja isingewezekana na hii ni kutokana na uwezo mdogo wa mashirka yetu ya utangazaji kutransform to dijitali tanzania nzima. sipati picha kama wangezima kote maana ingekuwa ni vilo balaa

tunapaswa kujua kwamba swala la kuhamia dijitali ni makubaliano ya lazima ya kidunia na TCRA ni msimamizi tu wa kutoa maelekezo kwa wenye vyombo vya habari kutekeleza takwa hili...lakini sasa gharama zote za kuhamia dijitali ni mzigo wa wenye mashirika ya utangazaji na hapa sasa ndio ugumu unapoingia
maana wao wapo kibiashara zaidi, wao ndio wanaonunua hiyo mitambo sio TCRA na wao ndio wanaiendesha na si TCRA. sasa wakati mwingine huwezi kuwaforce sana na ndio maana wanaenda kwa awamu kujali maslahi ya wananchi pia

Ni swala la muda tu kila kitu kitakuwa sawa kama ilivyokuwa kwenye mitandao ya simu tulipokuwa tunauziwa 500 kwa dk hata ukiongea sekunde lakini sasa kwa sh 400 unaongea dk 15, sms 100 na mb 50
 
mkuu unaishi Tz kweli?
 
Ndugu yangu unakataa nini na unakubali nini?
Narudia kusema kuna Usanii mkubwa sana unaofanywa na TCRA na mfumo wa digitali.

*Hakuna anaepinga kwamba Digitali ni mfumo wa kisasa na dunia nzima itatakiwa iwe imehamia huko kufikia mwaka 2015.

*Hebu fafanua baadhi ya haya mambo hapa chini kama sio usanii wa TCRA kupitia hadithi tamu wanazowapa wananchi, kwa mfano;
1/Mwisho wa mitambo ya analogia ni tarehe 31/12/2012 kisha mitambo yote itazimwa NCHI NZIMA!!(Sarakasi ikabadilishwa tarehe 29/12/2012 na kuwa Dar pekee!!!)

2/Mfumo wa digitali utahitaji kutumia king'amuzi na ANTENNA HAZITAHITAJIKA TENA!!(Hadithi ikabadilika na kuwa baadhi ya maeneo itahitaji kutumia Antenna!!)

3/Mfumo mpya wa digitali utakuwa ni mfumo NAFUU SANA(Cheap and Easy), BORA ZAIDI(Sound and Picture), MPANA ZAIDI(Large coverage, Multi channels)!!

4/Local Channel zote zitakuwepo kwenye ving'amuzi vyote tena hata PASIPO KULIPIA!!!(Sarakasi ikabadilishwa mwezi November na kuwa ni Local channel tano tu!!!)

*Ndugu yangu unaona shilingi Elfu tisa kwa mwezi ni ndogo sana? Uko Tanzania kweli? Unasema baada ya muda itashuka, are you sure? je haiwezi kupanda zaidi?
Hapo bado hujanunua king'amuzi(Tsh 39000/= hichi ni chini zaidi) na Antenna(Tsh30000/= katika baadhi ya maeneo) na bado hautapata local channels zote ambazo zilikuwa zinapatikana kwenye mfumo wa analogia. Kumbuka analogia ilikuwa ni mfumo wa Bure kabisa.
 
kichoongelewa ni garama kubwa na huduma mbovu,tofauti hali halisi hatuitaji mazoea,je unaweza kula sumu na ukasema nitazoeya?

Daima siku zote kila kunapotokea mabadiliko lazima kuna watakaoathirika. Hii ni survival for the fitest! Naamini huko tunakoelekea gharama zitapungua kutokana na ushindani wa biashara hivyo wale ambao hawana uwezo wa kulipia kwa sasa wataweza baadaye.
 
Tusonge mbele na watakaokwamisha wanyooshwe
 
Back
Top Bottom