miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,821
- 48,976
Habari zenu wana MMU,
Mimi nadhani hakuna mapenzi yenye furaha na amani kama kuwa na mwenza mmoja wa kuaminiana, lakini tunavyokuwa na wapenzi zaidi ya mmoja yani mtu unaishi kwa mateso na shida tu kama:
Sasa najiuliza matesio ni mengi kuliko starehe kwa nini tunataka kuwa na maisha ya tabu na shida na mateso mengi kuliko raha. Mimi kwa mtazamo wangu naona embu jaribu kuwa na mmoja kwanza uone raha yake yani ila hakikisheni mnapendana sana
Niwatakie maandalizi mema ya sikuku ya idd

- Kuwa na wasi wasi muda wote
- Hasira za mara kwa mara hasa ukikutana na maswali "ulikuwa wapi?" unaongea na nani? Unachati na nani? unaweza kasirika mpaka ukataka kufa wakati majibu yapo wazi na simple.
- Huna uhuru na simu yako.
- na unakuwa mlinzi wa simu badala ya simu ya kuicontrol wewe simu ina kucotrol wewe.
- Kukosa amani
- Kukosa uhuru wa hisia za mwenzio. yani ukimkuta mwenzio kanuna unaanza kuogopa
- Kuishi maisha ya hisia na kujilinda zaidi.