Usalama wa Raia - Mashuleni napo sio salama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usalama wa Raia - Mashuleni napo sio salama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Morani75, Oct 29, 2008.

 1. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele wana Jamvi wenzangu..... Nimesoma hii kitu hapa chini kwenye Nipashe la leo kwa kweli imenishtua kidogo..... Kwa ufahamu wangu ni kwamba wengi wetu tutasema hii ni "Isolated incidence" lakini je, tuiachie hapo?? Watoto wetu mashuleni watakuwa salama?


  Mwanafunzi awashambulia wenzake kwa kisu darasani

  2008-10-29 12:32:58
  Na Boniface Luhanga


  Wanafunzi wanne pamoja na mwalimu wao wa Shule ya Sekondari St. Peter`s iliyoko Kimara, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wamejeruhiwa vibaya baada ya mwanafunzi mmoja wa shule hiyo kuibuka ghafla darasani na kuwashambulia kwa kisu.

  Tukio hilo la kusikitisha, lilitokea jana saa 2:45 asubuhi baada ya mwanafunzi huyo, Aaron Mbando, anayesoma kidato cha tatu shuleni hapo, kuinuka ghafla darasani na kuchomoa kisu mfukoni mwake na kuanza kuwachoma visu wanafunzi wenzake pamoja na mwalimu wao aliyekuwa akifundisha somo la Jiografia kwa wakati huo.

  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Leticia James, aliwataja wanafunzi waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Eva Daza, Siwatu Abdallah, Esther Soter, Anzuruni Anzuruni pamoja na mwalimu Peter Salema.

  Mwalimu James alifafanua kuwa, wanafunzi Eva na Siwatu, walijeruhiwa vibaya kichwani, mgongoni, miguuni na mikononi.

  Alisema majeruhi hao wote wa kidato cha tatu, walipelekwa katika zahanati ya serikali ya Kimara na kupewa huduma ya kwanza ikiwemo kushonwa nyuzi kadhaa kwenye majeraha ambapo Eva na Siwatu, baadaye walikimbizwa hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.

  Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kimara, Dk. Regina Elias, alithibitisha kuwapokea majeruhi hao na kueleza kwamba, wawili kati yao walipata majeraha makubwa.

  ``Wawili kati yao, wamepata majeraha makubwa ambapo mmoja amechomwa kisu kichwani na kimezama sana na kusababisha atokwe damu nyingi...kwa zahanati hii, hatuwezi kudhibiti hali hiyo na ndiyo maana tumeshauri pamoja na mwenzake, wapelekwe Mwananyamala kwa matibabu zaidi,`` alifafanua.

  Nipashe ilishuhudia gari dogo lenye namba za usajili T 148 AJA likiwabeba majeruhi hao kuwapeleka hospitali ya Mwananyamala.

  Akisimulia mkasa huo, mwanafunzi aliyenusurika kujeruhiwa, Mary Patrick wa kidato cha tatu, alisema wakiwa darasani wakifundishwa somo la Jiografia na mwalimu Salema, ghafla mwanafunzi mwenzao Aaron, alisimama na kumchoma kisu Eva aliyekuwa ameketi karibu naye.

  Alisema tukio hilo liliwashtua wanafunzi wote ambapo mwalimu wao, Salema alijaribu kumfuata kwa lengo la kumdhibiti, lakini naye pia alichomwa kisu kichwani.

  ``Ndipo wanafunzi wote pamoja na mwalimu, tukaanza kusukumana mlangoni kila mmoja akijaribu kukimbia kuokoa maisha yake,`` alisema.

  Alisema wakati wakisukumana mlangoni, ndipo mwanafunzi huyo Aaron, alipopata nafasi kuwachoma visu kila mwanafunzi aliyefanikiwa kumfikia.

  ``Kulikuwa na kelele zisizokuwa za kawaida, hali iliyowashtua walimu na wanafunzi waliokuwa kwenye madarasa mengine ambao walifika eneo la tukio kutaka kufahamu kulikoni,`` alifafanua.

  Alisema hadi wanafanikiwa kutoka nje ya darasa, mwanafunzi huyo alikuwa tayari amewajeruhi wanafunzi wanne pamoja na mwalimu.

  Hata hivyo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Leticia James, alisema wiki kadhaa zilizopita, mwanafunzi huyo aliyewajeruhi wenzake, hakuhudhuria shuleni.

  Alisema baadaye, alirejea shuleni ambapo mzazi wake alidai kwamba, mtoto wake alikuwa ametoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha.

  Mwalimu Mkuu Msaidizi huyo aliongeza kuwa, mzazi wa mwanafunzi huyo pia alidai kuwa, mtoto wake alikuwa akikabiliwa na matatizo ya akili.

  Hata hivyo, alisema tangu aliporejea shuleni hapo takriban wiki moja, hakuonyesha dalili zozote za kuumwa hadi jana alipofanya kitendo hicho.

  James alisema uongozi wa shule, haukuweza kufahamu mara moja namna mwanafunzi huyo alivyoweza kuingia na kisu darasani na kwamba kwa kawaida, hawana utaratibu wa kuwakagua wanafunzi mifukoni mwao kama wanaingia madarasani na vitu vya hatari zikiwemo silaha.

  Mwanafunzi aliyefanya unyama huo, pia alijeruhiwa vibaya kichwani na ilidaiwa kwamba alijichoma mwenyewe kwa kisu baada ya kuwajeruhi wenzake.

  Hata hivyo, mwanafunzi huyo alikamatwa na kufikishwa kituo Kidogo cha Polisi Kimara na baadaye kuchukuliwa kwa gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 1412 na kupelekwa kituo cha Polisi Magomeni.

  Ilidaiwa kuwa, ilikuwa ni kazi kubwa hadi kufanikiwa kumkamata mwanafunzi huyo kutokana na kuwa na kisu mkononi.

  Na alipohifadhiwa katika kituo kidogo cha polisi Kimara, mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele huku akigonga gonga mlango kwa nguvu akitaka afunguliwe atoke.

  Hili ni tukio la pili linalofanana na hilo la jana kutokea ambapo zaidi ya mwezi mmoja uliopita, mgonjwa mmoja wa akili, aliwashambulia wagonjwa wenzake katika wodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwaua wawili huku wengine watano wakijeruhiwa vibaya.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  HATARI sana hiyo, tumeanza kuwa kama kwa wenzetu wanakochapana risasi mashuleni.اللهawape nafuu ya haraka waliomahututi na kuwaponya wote pamoja na waliojeruhiwa kidogo.
   
 3. M

  Mundu JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nadhani utaratibu wa kuanza kukaguana ufanyike mashuleni pia hasa shule za sekondari. kwani wanafunzi wengi hutumia madawa ya kulevya, hivyo kuna uwezekano wa kuleta madhara makubwa kwa wengine na wao wenyewe.

  Hili la Kimara liwe ni la kutufungua Macho. lets act now.
   
 4. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  heshima mbele wakuu.... Kumbe sio madarasani/mashuleni tu ambapo wanafunzi wanakuwa exposed kwenye majanga yanayotishia usalama wao, kumbe hata mitaani wakitoka/kwenda shule..... Hii nimeona kwenye gazeti la Nipashe na swali kubwa ninalojiuliza ni:
  1. Je, kwa nini kusiwe na utaratibu wa walimu/wazazi kutumia muda mchachje katika ratiba zao nyingi kuongelea mambo yanayohusu mahusiano na watoto wa kika manake inaelekea huyu jamaa labda alishafanya advances to the lady!
  2. Apart from kuzungumzia kuwa watu waache kufanya mapenzi na wanafunzi, mbona inaelekea hakuna hatua yoyote inayochukuliwa zaidi ya watu kupiga kelele kwenye hotuba??

  Mungu Ibariki Tanzania na watu wake na atuondolee balaa hili amablo limekuwa linakua kwa kasi kubwa sana hapa nchini!!

  Mwanafunzi auawa kwa kukataa kufanya mapenzi

  2008-11-02 12:49:22
  Na Sammy Kisika, PST Sumbawanga


  Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari Kanoge wilayani Mpanda, mkoani Rukwa amekufa baada ya kuchomwa kisu mgongoni na mwanaume mmoja aliyekataa kufanya naye mapenzi.
  Taarifa zilizotolewa na kuthibitishwa na jeshi la polisi wilayani Mpanda, zimemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Grace Mgawanyu (23), ambaye alichomwa kisu na Bakisi Buruga (28) ambaye naye alijiua muda mfupi baada ya kutenda unyama huo.

  Taarifa zimeeleza kuwa siku ya tukio Oktoba 29, Grace alikuwa akitokea shule akiwa amepakizwa kwenye baiskeli na rafiki yake wa kike wakiwa wanaelekea nyumbani, wakiwa njiani, walikutana na mwanaume huyo waliyempita kwa kasi lakini alirusha kisu na kumchoma mwanafunzi huyo mgongoni kisha kudondoka chini huku akitokwa na damu nyingi.

  Baada ya kudondoka chini mwanaume huyo alimfuata mwanafunzi huyo na kumshambulia tena kwa kumchoma kisu katika mikono huku akimweleza kuwa mwisho wa maringo yake ulikuwa umefika, na atajutia kumkataa kushirikiana naye kimapenzi.

  Shambulio hilo lilimfanya mwanafunzi aliyembeba Grace katika baiskeli kuanza kupiga kelele zilizowakusanya wanafunzi wengine waliokuwa katika masafara wa kurudi makwao, hatimaye walianza kumfukuza Buruga aliyekuwa akitokomea porini.

  Akiwa amekimbia umbali mrefu ili hali wanafunzi hao wakizidi kumkimbiza Buruga alisimama huku akitweta na kusema kuwa ni bora afe kuliko kutiwa mikononi mwa wanafunzi hao au polisi, ndipo alipochomoa kisu chake na kujichoma mwenyewe tumboni kwa kujichana katikati ya tumbo akitenganisha sehemu ya tumbo na mbavu na hatimaye alidondoka chini na kufa papo hapo.

  Wakiwa wanashuhudia kwa karibu muuaji huyo akijiua mwenyewe, wanafunzi hao wa shule ya Sekondari Kanoge waliondoka hadi sehemu alipochomwa kisu mwenzao na kumkuta akigalagala chini kwa maumivu ambapo walitoa taarifa kituo cha polisi waliokwenda kumchukua na kumkimbiza hospitali ya wilaya ya Mpanda wakiwa na maiti ya Buruga.

  Habari zilieleza kuwa mwanafunzi huyo alifariki dunia akiwa njiani akikimbizwa hospitalini kupata matibabu.

  Uchunguzi wa polisi wilayani Mpanda ulibaini kuwa awali baada ya kumkataa mwanaume huyo Grace alitumiwa ujumbe kupitia kwa rafiki wa Buruga ukimwarifu kuwa akae chonjo kwani hakukubaliana na maamuzi ya kukataliwa licha kubembelezwa kwa muda mrefu hivyo aliahidi kumfanyia kitu kibaya katika maisha yake.

  Hata hivyo, polisi walisema walishangazwa na mwanafunzi huyo kutotoa taarifa katika vyombo vya usalama licha ya kupokea vitisho hivyo kutoka kwa mwanaume huyo.

  SOURCE: Nipashe
   
 5. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Lakini wakuu mi bado nina wasiwasi na mazingira ya tukio zima ukianzia kutoweka kwa huyo kijana kwao kwa muda usiojulikana na sijui mzazi wake baada ya kuona kijana amerudi alichukua initiative gani angalau kuzungumza nae kujua kilichosababisha atoweke kwao, alikuwa wapi kwa muda wote huo na ikibidi afatilie huko alikokuwa mtoto wake....Wengine wanafichwa kwenye vijiwe vya bangi tu....wakitoka huko matokeo yake ndio wanakuwa hivyo....
   
Loading...