Usalama wa mitandao ni sawa na Matumizi mazuri ya mitandao?

gkutta

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
273
168
Tunapomsikia mtu akisema Usalama wa mitandao/Matumizi mzuri ya mitandao...tumeshawahi kujiuliza huyu mtu ana lengo na nia gani kwa jamii??....Kwanza kabla mtu yeyote hajaanza kutuhubiria kuhusu Usalama wa Mitandao akihusisha na Lugha laini ya matumizi MAZURI ya mitandao tunaomba watupe tfsiri halisi kikatiba na kisheria juu ya hayo maneno!!!
 
kichwa changu kimejaa maji a.k.a kichwa maji, sijakusoma bado, nitasoma comments za wenzangu nipate concept
 
Tunapomsikia mtu akisema Usalama wa mitandao/Matumizi mzuri ya mitandao...tumeshawahi kujiuliza huyu mtu ana lengo na nia gani kwa jamii??....Kwanza kabla mtu yeyote hajaanza kutuhubiria kuhusu Usalama wa Mitandao akihusisha na Lugha laini ya matumizi MAZURI ya mitandao tunaomba watupe tfsiri halisi kikatiba na kisheria juu ya hayo maneno!!!

Mkuu labda anamaanisha mitandao iwe sehemu nzuri ya kupashana habari,kuwasiliana,kufanya biashara na sio kuchafuana, utapeli, kuitumia kwa uchochezi n.k
 
Maana ya kutochafuana ni kkuzuia haki ya raia kukosoa serikali kwa uhuru wake kikatiba kisiasa na kisheria??...kupashana habari za sifa zisizo na kichwa wala miguu kusifia pangaboi hata kama tunajua ni kosa kubwa kiuchumi na kiuzalendo kwa walipakodi wasio na maji salama vijijini?
 
Aisee, mkuu ni haki yako kukosoa serikali..ila je unaikosoa kwa hoja gani zenye mashiko?? Serikali isiyotaka kukosolewa itakuwa sio sikivu...Ni lazima serikali ikosolewe no matter what
 
Back
Top Bottom