Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,916
Hizi si habari ngeni hata kidogo! Hizi si habari mpya hata kidogo! Kinahozifanya ziwe mpya na ngeni ni kule kusemwa rasmi hadharani na kiongozi wa upinzani kwenye jukwaa la kisiasa la mkutano wa hadhara..! Kiongozi hasimu wa chama tawala
Tukiondoa uvivu wa kufikiri na ukengeufu wa kutunza kumbukumbu tunaweza kujikumbusha yale masaa 72 yote yaliyojiri na kuvuja kabla ya kutangaziwa tanzia ya mwendazake...
Hayo masaa 72 sawa na siku 3 yalikuwa ni hitimisho tu ya minong'ono ya takribani wiki nzima
Tuhuma za benki kuu kuporwa mabilioni
Tuhuma za hazina kukombwa mabilioni
Tuhuma za kukutwa chumba chenye mabilioni nyumbani Chato kwa mwendazake!
Kuna watu walitajwa kwa majina kabisa kwamba ndio walikuwa viongozi kwenye hayo mambo.. Hawa wote wapo na bado wako hai, na karibia wote wakiwa na madaraka makubwa tuu
Swali: Usalama kazini?
Utendaji kazi wa hiki kitengo ni tofauti kabisa na utendaji kazi wa vitengo vingine vya serikali.. Ambavyo kwa sehemu kubwa hutoa mrejesho kwa jamii ama huishirikisha jamii ya yale yaliyojiri.. Japo si yote bali yanayofaa kuifikia jamii kwa utaratibu rasmi
Hakuna jambo linalofanyika popote duniani bila usalama wa nchi husika kuwa na taarifa nalo.. Jukumu kubwa na la msingi la usalama si kwenda front bali ni kupeleka taarifa kwa vitengo husika!
Kuna mazingira ambayo kama kuna mushkeli kidogo wa jambo fulani na kitengo husika kikashindwa kwa sababu zozote zile kulifanyia kazi kwa wakati.. Taarifa hizo huvujishwa kwa jamii kwa namna ya kipekee mno!
Usalama ndio huendesha taifa kupitia serikali na vitengo vyake vingine.. Ni usalama ndio huamua jambo liwe ama lisiwe na kwa sababu gani ama kwa wakati gani!
Kupunguza urefu wa mada ni kwamba
Mikutano ya kisiasa isingewezekana bila usalama kuridhia
Mikataba mibovu isingevuja bila usalama kuridhia
Watu wasiojulikana.....,..!
Kuna tuhuma zikisemwa rasmi hadharani kwenye jukwaa la kisiasa mbele ya mkutano mkubwa wa hadhara..
Hilo si bahati mbaya
Hilo si kuropoka
Hilo si kutafuta kiki
Hilo si la uongo wala la kusingizia...!
Yapo ya kuropoka na kusiibana kwenye majukwaa ya siasa za majitaka lakini yasiyo sensitive kabisa! Na yapo ya kutamkwa hadharani huku mtamkaji akitambua wazi kwamba ana wajibu wa kutakiwa kuthibitisha itakapohitajika kufanya hivyo kisheria...!
Kama haya ya huko Chato yameanza kusemwa rasmi hadharani basi tambua kuna mziki mnene unakuja! Lakini huo mziki mnene unaweza kuzimika ghafla bin vuu kama lile limkataba likifutuliwa mbali tena kwa kauli moja tuu..!
Wazalendo wako kazini kwa maslahi mapana ya Taifa teule la Tanganyika huru...!
Sent using Jamii Forums mobile app