Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,943
- 1,015
Wanasiasa wamekaa kimyaa… watendaji kimya… POLISI wako usingizini.
Kutokana na kile kilichotokea kwa wanachuo wa IFM waishio Kigamboni na yale yaliyokwisha kutokea wanachuo wa Mwalimu Nyerere Memorial Academy, DUCE, UDSM, St. John-Dodoma, Tumaini University (DSM Campus), MUCE, Saint Augustine na wenzao wa CUHAS(formerly BUCHS) . Ni meshawishika kuliandikia hili ili tuone namana njema ya kutoka hapa mahali tiulipo ambapo si salama kwenda kule tukutakako ambako ni salama.
Kama wanajamii karibu tulijadili jambo kama tataizo linaloliangamiza taifa letu kwa kuathiri rasilimali watu tarajiwa, na jamii kwa upande wa pili.
Sababu ya uwepo wa Hostel
Kutokana na kuongezeka kwa udahili katika vyuo vingi hapa nchi ambao hauzingatii uwepo wa Hostel za vyuo husika, na ukipata shinikizo kubwa la uhitaji wa vijana wa kitanzania kupata elimu, ilipelekea wanafunzi wanaodahiliwa kutafuta vyumba vya kupanga vilivyo karibu na vyuo husika.
Binafsi bado hadi sasa siafiki kuwa tusiwadahili wanafunzi, kisa serikali haikujenga hostel za kutosha katika chuo husika. Nafikiri wakati ujenzi wa hosteli ukiwa unaendelea, basi wawepo wanachuo watakao patatfursa ya kusoma lakini wakiwa wanatokea ‘mtaani'.
Tatizo la kukosekana kwa hosteli za kutosha lilianza kujionyesha kwa kiasi kikubwa katikati mwishoni mwa miaka ya 1990, kwaupande wa UDSM. Hiki ndicho kilikuwa kiini cha ujenzi wa Hosteli za Mabibo. Kabla ya hapo itakumbukwa kuwa kuwa kulikuwa na wimbi kubwa la wanachuo kupanga Ubungo-Msewe, Kijitonyama, Survey, Mwenge, n.k.
Wanafunzi walipanga chumba kimoja watatu, wanne, watano,.. kwa kadiri wao walivyoona inafaa katika kundi lao.
Taratibu watu walianza kuzibadilisha nyumba zao kutoka kupangisha wanachi wa kawaida, waliamua kuwapangisha wanachuo tu (Nakumbuka kuna nyumba ukienda mwezi wa Mei kutaka kupanga wanakwambia wanafunzi wamekwisha book kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo, na hela wametoa).
Mwendelezo wake ukawa ni kwa wamiliki wa nyumba zilizo karibu na vyuo kuanza kuzikarabati nyumba zao na kuzigeuza hosteli. Awala zilikuwa ni nyumba za kuishi familia, lakini sasa baada ya kuweka vitu kadhaa na kufanyiwa matengenezo zimekuwa hosteli. Wanachuo hawapangishwi kwa chumba tena bali kwa kitanda. Mfano, mwanzoni chumba kililipiwa 20,000/= kwa mwezi lakini sasa kitanda kinalipiwa 15,000/= kwa mwezi. Kama chumba kinakaa vitanda vya ghorofa vitatu, mwenye nyumba atapata 90,000/= kwa mwezi. Mtu anapata super-profit kutoka 20,000/= kwenda 90,000/= kwa mwezi.
Hosteli zilivyo na zilipo
Osteli nyingi ni nyumba za kuishi familia. Hazijajengwa kwa kufuata vigezo rasmi vya kuwa hosteli iwe na vyumba vya ukubwa gani, ikae na vitanda na fanicha nyingine ngapi kwa wnafunzi wangapi, eneo wazi la nje liwe na ukubwa gani, tahadhari za majanga ya moto zimechukuliwaje, n.k. Nyingi ya hosteli hizi hazina uzio na hata zile zenye uzio hazina ulinzi wa mali na maisha ya wanachuo.
Hosteli hizi zipo katika maeneo ya makazi ya watu si katika yale maeneo yaiyotengwa kwa huduma za jamii kwa sababu nyingi zinamilikiwa na watu binafsi na kama nilivyoandika awali zilikuwa ni nyumba kwa matumizi ya kuishi familia. Zimetengeneza muingiliano wa wazi kati ya wanachuo na wanamtaa.
Athari za hostel hizi kwa wenyeji
Japo kuna faida kubwa sana ya kifaedha kwa wale wanaofanya biashara karibu na hosteli hizo kutokana na ama kuuza biashara zao au huduma, lakini pia yapo malalamiko dhidi ya wanaoishi katika hosteli hizo.
Kwa uchache:
Ndoa: Mahusiano ya kindoa yamekuwa yakiharibiwa na uwepo wa wanachuo kutokana na tabia mbaya ya baadhi yao; kwa wale wa kike kutoka na waume za watu hivyo yule wa nyumbani kuonekana nyanya mbovu, wale wa kiume kutoka na wake ama wachumba za watu na kusababisha kuongezeka kwa ‘inferiority complex' kwa vidume. Kwa majirani, wako wanawake wanaotaka kuonekana wanavaa kama wanavyuo ilhali kipato ama umri wao haulingani na wanavyuo, matokeo yake wamekuwa wakiwashinikiza wenzi wao kufanya yale yaliyo juu ya uwezo wao…vurugu na mikwaruzano kuzidi.
Mahusiano mabovu: Kutokana na namna wanachuo wanavyoishi na inferiority complex zilizojengeka, hakuna mahusian mazuri kati ya wanachuo na wenyeji-majirani. Wako wanaosema wanacuo wanajidai sana, hawasalimii, wanajiona sana na kadha wa kadha. Matokeo yake watu wanafikia kiwango cha kusema, "aa bwana, mi wanachuo wakivamiwa au kupata matatizo siwasaidii…labda fulani nitamsaidia (wanamtaja mwanachuo ambaye wanamahusiano naye mazuri)"
Ikumbukwe kuwa namna ambavyo wanachuo wanaishi chuoni ambapo si lazima kumsalimia kila mtu ama kumtambua kwa namna moja au nyingine (vyuoni ni maisha ya kawaida); mtaani sivyo wanavyotaka watu waishi. Ipo ile namna ya kutambuana na hata kusalimiana au kushirikiana. It is like remaining Maasai and working in executive office with ‘lubega'.
Hostel ni shabaha (target) nzuri kwa vibaka
Kutokana na ujinga wa wanavyuo kuji-show-off na kutokuwa na maarifa ya risk reduction from being attacked with robbers, wamejikuta wanatembea na vitu vya thamani waziwazi ama kuonyeshana/kutumia katika vibaraza na penu za majengo ya hosteli. Matokeo yake vibaka wanajua …aaah! Pale wanavitu hivi na hivi…tukiwavamia tutapata kwa kiasi hiki..wanaanza kupanga mipango ya kuwavamia ama wakiwa njiani kwenda/kurudi toka chuoni au usiku wakiwa wamelala.
Usalama wa mali na maisha yao
Matokeo yake ni kuwa, usalama wao unakuwa mdogo sana, si katika mali zao tu bali pia hata katika viungo na maisha yao. Wamekuwa wakiporwa sana vitu mbalimbali kuanzia saa, simu, laptop, heleni, mikufu,viatu, nguo, n.k. Kana kwamba haitoshi wamekuwa wakipigwa, kukabwa, na kujeruhiwa kwa kiasi kikubwa na kwa wasichana wamekuwa wakibakwa.
Haya mambo yanapokuwa yanatokea, yamekuwa yakifumbiwa macho kama si kupuuzwa kwa sababu ni ya ‘mpito' na pengine wanaopata na matatizo hayo hawana uhusiano wakindugu nasi.
Ni wakati sasa, kwa Jeshi la POLISI kuzichukulia kwa uzito kila taarifa ya matukio ya uhalifu dhidi ya wanavyuo.
Wananchi tusiwatenge ama kuwa na kinyongo na wanachuo, tafadhali tuwasaidie wanapokuwa katika shida ama hata kwa mawazo wasipokuwa na shida. Hatujui hawa watu watakuwa ni kinani katika Tanzania ya kesho. Tunapowazira tunawapoteza. Tunapowaacha waumizwe wanapovamia tunazidi kupunguza rasilimali watu bora kwa namna moja au nyingine.
Wasibweteke kuishi katika chumba bila silaha ya jadi ya kujihami na kujua namna ya kuitumia. Uzoefu umeonyesha wanavamia kama kuku, hawajui kujihami kwasababu hawana silaha.

- Polisi wafanye nini?
Ni wakati sasa, kwa Jeshi la POLISI kuzichukulia kwa uzito kila taarifa ya matukio ya uhalifu dhidi ya wanavyuo.
- Wamiliki wafanye nini?
- Wanachi wafanye nini?
Wananchi tusiwatenge ama kuwa na kinyongo na wanachuo, tafadhali tuwasaidie wanapokuwa katika shida ama hata kwa mawazo wasipokuwa na shida. Hatujui hawa watu watakuwa ni kinani katika Tanzania ya kesho. Tunapowazira tunawapoteza. Tunapowaacha waumizwe wanapovamia tunazidi kupunguza rasilimali watu bora kwa namna moja au nyingine.
- Wanachuo wafanye nini?
Wasibweteke kuishi katika chumba bila silaha ya jadi ya kujihami na kujua namna ya kuitumia. Uzoefu umeonyesha wanavamia kama kuku, hawajui kujihami kwasababu hawana silaha.
- Wazazi/walezi wafanye nini?