Wakuu habari za wakati?
Leo mchana nilibahatika kufuatilia tukio la kuuaga mwili wa G.G. Kariuki, aliyepata kuwa waziri wa Ardhi na Makazi nchini Kenya, nikapatwa na mshangao kuona Rais Kipenzi cha Wakenya na Afrika Mashariki kwa ujumla akiwa huru kabisa bila kusimamiwa na magruned kwa nyuma au pembeni yake. Nikabaki najiuliza au kwenye misiba walinzi hawaruhusiwi au Usalama wa Kenya uko vizuri kuliko wa hapa kwetu? Kwa nini Rais kwetu akiwa anatoa neno lazima asimamiwe na walinzi nyuma yake na pembeni yake? Ina maana sisi nchi yetu siyo salama ki vile? Juzi tulishuhdia maaskari waliosheheni silaha nzito za kivita alivyotinga kwenye uwanja wa Nyamagana kushuhudia mpira wa ndondo cup wakiwa mbele na nyuma huku vidole vikiwe kwenye trigger kabisa tayari kwa lolote! Je,, hizi ni sifaaaa au kitu gani! Sijamwelewa Uhuru kwa kweli!!