Usalama barabarani

Usalama barabarani

Bin Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
313
Reaction score
247
Habari zenu wakuu, tunakutana tena kwa awamu nyingine baada ya JF kutoka mapumziko. Kama mada inavyojieleza ni kuhusu usalama barabarani, jeshi la polisi kitengo cha barabarani linafanya kazi kubwa sana lakini bila mafanikio. Tatizo lipo katika njia ya kutatua hili tatizo.

Trafiki wao wameegemea zaidi kulipisha madereva faini na adhabu nyingine wakiamini litakuwa ni suluhisho. Kinacho takiwa ni trafiki watoe elimu ya kutosha kwa madereva na wenye vyombo vya moto. Waweke vituo maalum barabarani kwa ajili ya kutoa elimu bila kumuadhibu dereva.

Mfano kwenda mikoani kuwe na vituo vya elimu kila mpakani mwa mkoa kutoka/ kuingia mkoa mwingine.Hii inaweza kusaidia kama sio kumaliza tatizo. Huwezi kumpa mtu adhabu halafu ndio umpe elimu hawezi kukuelewa maana tayari anahasira , hawezi kukuelewa. Matrafiki wengi barabarani wanajali adhabu zaidi bila kutoa elimu. Hayo ni mawazo yangu kama mdau wa barabarani.
Wengine wanaweza kuchanga mawazo pia
 
Bora umeipost huju jamii forums! Thubutu kuipost Facebook o instagram upewe kesi ya uchochezi
 
Mh waziri wa mambo ya ndani hawezi kuisoma hii. Ila nadhani ni wazo zuri kama angeliisoma. Lakini, mapato yatapungua. Aangalie kama Mbeya fine zimepungua ajue, RTO ndo alikuwa anazi "bemenda"
 
Tatizo kitengo cha usalama barabarani kinajisifu kukusanya mapato mengi wakati hilo ni tatizo kubwa sana kwa usalama. Faini za usalama barabarani zinatokana na makosa ya vyombo vya usafiri au uzembe wa madereva, sasa unapokuwa na makusanyo mengi ujue usalama barabarani nao ni mdogo, kwani kuna uwezekano vyombo vilivyopo barabarani havistahili kuwepo au madereva waliopo hawajui sheria za barabarani. Askari wajipange kutoa elimu zaidi kuliko faini watafanikiwa.
 
Uzi mzuri.ila saivi tupo kule tunacomment kwenye nyuzi za ngono kwanza kama kawaida yetu wa TZ
 
Usalama barabarani ni jukumu la wote
 
Ukaguzi wa vyombo vya usafiri, leseni za madereva na barabara ni muhimu pia. Zoezi liwe endelevu. Lisisubiri ajali zitokee alafu wahusika waanze kufanya kazi kama inavyotokea kipindi hiki.
 
Kwa kweli inabidi turudi kwenye elimu ya mara kwa mara kwa watumiaji wa barabara hasa madereva.
 
Leo jamaa alikuwa anavuka barabara kwa miguu wakati taa haijawaka akapigwa 30 hapohapo kwa uzembe
 
tatizo si tz tu, traffic kote duniani wanatoa 'ticket penalt' kwa madreva wasiofuata usalama barabarani inayolipwa traffic office,hivyo hili haliepukiki! Tatizo kubwa kwa maoni yangu, pamoja na mengine uwepo wa mashimo (potholes) barabarani ni moja ya sababu kuu za ajali mbaya sana barabarani, maana dreva aliye highway 120/hr - 160km/hr kama SGR afu ghafla anakutana na pothole ambalo kulikanyaga kwake inamaanisha rim kupinda kama sio kuvunjika kabisa ni rahisi sana kuhama njia na kugongana uso kwa uso na magari! Wito kwa wanaohusika na kufanya 'repair' barabara zetu, wawe wepesi kuzipa mashimo hayo mara tu yanapotokea!
Tatizo jingine kubwa ni kutokuwa serious na mafunzo ya udereva hasa kwa kuwa na utitiri wa vyuo visivyokidhi ubora wa kufundisha madereva wenye weledi! Kwa hiyo usishangae kuona madreva wengi hawana ufahamu wa kutosha juu ya lama nyingi muhimu za barabarani na hata njia bora ya uendeshaji wa kujilinda (defensive driving) badala yake by default wanaendesha kwa ubabe/shamblizi (offensive driving)!
leseni nyingi wengine zinawakuta home, wala hawajawi hata kufika kwenye mafunzo ya udereva husika, wanafunzwa nyumbani na watu wasiokuwa na weledi wa udereva! Kwa hiyo usishangae mtu akakugonga barabarani na akakuraumu kuwa ww ndio mwenye makosa hata kama kosa ni lake...maana hajui sheria za barabarani.
ukitaka kujua hili, madereva waliowengi hawawezi endesha kwa kujiamini wakienda nje ya Tz!
Niishie hapo kwanza!

Habari zenu wakuu, tunakutana tena kwa awamu nyingine baada ya JF kutoka mapumziko. Kama mada inavyojieleza ni kuhusu usalama barabarani, jeshi la polisi kitengo cha barabarani linafanya kazi kubwa sana lakini bila mafanikio. Tatizo lipo katika njia ya kutatua hili tatizo.

Trafiki wao wameegemea zaidi kulipisha madereva faini na adhabu nyingine wakiamini litakuwa ni suluhisho. Kinacho takiwa ni trafiki watoe elimu ya kutosha kwa madereva na wenye vyombo vya moto. Waweke vituo maalum barabarani kwa ajili ya kutoa elimu bila kumuadhibu dereva.

Mfano kwenda mikoani kuwe na vituo vya elimu kila mpakani mwa mkoa kutoka/ kuingia mkoa mwingine.Hii inaweza kusaidia kama sio kumaliza tatizo. Huwezi kumpa mtu adhabu halafu ndio umpe elimu hawezi kukuelewa maana tayari anahasira , hawezi kukuelewa. Matrafiki wengi barabarani wanajali adhabu zaidi bila kutoa elimu. Hayo ni mawazo yangu kama mdau wa barabarani.
Wengine wanaweza kuchanga mawazo pia
atizo
 
Back
Top Bottom