Usajili namba za simu-umakini zero!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Awali nilizani zoezi la kusajili namba za simu ni kitu serious ambacho kingehitaji watu (wasajili) makini kumbe sivyo! Nimesajili namba 3, za tigo 2 na voda moja. Tigo ya kwanza ingawaje nimesajili zamani kabisa kabla ya foleni, lakini jana naulizia taarifa zangu naambiwa namba yangu haijasajiliwa na hivyo nitume upya jina na namba ya fomu!! Nikafanya hivyo jana, na leo nilipoulizia taarifa hizo,nikapewa jibu lile lile-kwamba sijasajiliwa!!!!! Nilipohitaji taarifa za namba nyingine ya hao hao tigo ambayo nimeisajili majuzi; nikajibiwa nimesajiliwa. Hata hivyo, taarifa nilizotumiwa (jina na namba) ni tofauti kabisa!!!! Kwa maana nyingine, kwa upande wangu ingawaje nimejisajili lakini zoezi hilo lime-fail kwa 100% !!!! Nilihitaji taarifa kutoka Vodacom, wao waliishia tu kusema nimesajiliwa vizuri kabisa lakini bila kunitumia taarifa zangu ambazo ningezihakiki!!!! Sina hakika, labda wasajili wa Vodacom hawakosei!!!!! The question follows, TCRA washasema kwamba wasiosajiliwa namba zao zitafungwa; sasa kwanini mtu kama mimi nifungiwe kwa uzembe wa service provider?! On the otherhand, ile namba ambayo taarifa zake sio sahii,endapo nitaitumia ndivyo isivyo, sio ataingia matatani mtu ambae wao ndie wameandika habari zake wakati sio?! Sasa nini maana ya zoezi zima hili?! Ni nani wa kulaumiwa? Ingawaje zoezi hili linaonekana muhimu lakini hata wasajili tulionao huku uswahilini wala hawaonekani kama ni watu makini!!! USHAURI KWA TCRA; wala msiharakie kufungia namba za watu kabla uhakiki haujafanyika!!!
 
Mkuu acha tu, mi nilisajili namba yangu ya tigo toka August last year leo naulizia naambiwa sijasajiliwa au kama nimesajili nitume tena namba ya fomu ya usajili! Fomu yenyewe sijui nilipoweka! Hawa jamaa kweli hawako makini, muda wote huo bado hawajaweka kumbu kumbu kwenye mtandao wao!?
 
At Tigo, we pride ourselves in customer care. Our call centre caters to the needs of all service ranges. We have you covered 24/7 hours a day with our call centre staff ready to assist you with any queries you may have.



bullet_verde.gif
Contact Information:
bullet_rosa.gif
MIC Tanzania LTD
HEAD QUARTERS
P.O.Box 2929
Lugoda Street, Dar es salaam,
Tanzania.
Phone: 0713 123 103
Fax +255 22 2120474
dot_clear.gif
dot_clear.gif
bullet_rosa.gif
For more information
Dial 0713 800 800 or 100
dot_clear.gif
dot_clear.gif
photo_customer.jpg

Tigo ni matepeli wa kubwa, kwenye hizo contact zao ni namba mmoja tu ina fanya kazi hiyo ya kulipia kidogo ya 800 800.
Namba ya customer care 100 ukipiga unaambiwa umekosea namba, mtandao mkubwa kama huu hauna e-mail address kwajili ya wateja wao?
 
yani hakuna kero kama hawa watu wa mitandao,sijui wanafanya kazi gani
hawako makini na kumbukumbu,sasa computer/server za nini?!!ivi kwa akili kidogo tu hivi unaweza tunza mikaratasi ile uloandikisha??basi wawe wanasema hatutunzi kumbukumbu ktk computer zetu so mtu ujue unafanyeje!! ovyo kabisa
nyambafff!!
 
Mkuu acha tu, mi nilisajili namba yangu ya tigo toka August last year leo naulizia naambiwa sijasajiliwa au kama nimesajili nitume tena namba ya fomu ya usajili! Fomu yenyewe sijui nilipoweka! Hawa jamaa kweli hawako makini, muda wote huo bado hawajaweka kumbu kumbu kwenye mtandao wao!?


Mkuu, uwe na fomu au usiwe na fomu yote sawa tu!!! Mie bahati fomu zote ninazo lakini hata nilipotuma jina na namba ya fomu bado nilipoouliza 30 hours later niliambiwa sijasajiliwa na kwamba nitume namba ya fomu na jina wakati nilishafanya hivyo!!! Hawa Voda ndo wananitisha zaidi wanaosema wamenisajili kwa usahihi bila ya kunitumia taarifa zangu ili nizithibitishe!!!! Usisahau, namba moja ya tigo wamenisajili lakini taarifa zilizopo si zangu!!!
 
sasa sisi tulioko nje tumeumia manake nilisajili mwaka jana na sijafuatialia tena. Potelea mbali wakinifungia!
 
Niliuliza zain, ikawa sahihi; ila nilipojaribu mara ya pili, nikaletewa taarifa tofauti kabisaa (Now I'm confused), no luck yet with Tigo na Voda. Only God knows ni kitu gani Watanzania tunafanya japo 95% sahihi...:pray:
 
hizi namba kama zinasajiliwa hovyo hovyo bila umakini wowote au kuakikisha kwamba mtu anatoa information za kweli basi huko mbeleni kutakuwa na hatari mtu kupewa kesi sio yake.
 
Kosa kubwa lilikuwa kuandikisha watu kwenye makaratasi in thew first place, kwenye kuhamisha data rahisi sana kuchemsha, wangefanya kwa kompyuta tangu mwanzo. Na mahakamani sijui itakuwaje, kama system iko ovyo sidhani kama ushahidi utakubalika mahakamani.
 
mimi nasubili hiyo date ifike; alafu ka-simu kangu kasifanye kazi; kwani nilisha kwenda kuuliza wakaniambia nimesajiriwa. Inabidi wanasheria wajiandae kwani malalamiko yatakuwa mengi.
 
Back
Top Bottom