Usajili kidato cha sita

Usajili kidato cha sita

Messier 31

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2017
Posts
477
Reaction score
1,205
Mimi ni mwanafunzi ambaye kwa sasa ndo naingia kidato cha sita,
Nilipata matatizo wakati narudi shule baada ya hii likizo, nikaibiwa begi ambalo lilikuwa na vitu vifuatavyo
•Cheti cha form iv
•Result slip ya form iv
na vingine.
Lengo la hii thread nilitaka kujua kuwa je naweza nikasajiliwa kidato cha sita bila hivyo vitu hapo juu maana wakati tunakwenda likizo tulitaarifiwa ya kuwa turudi na kitu kimojawapo hapo juu ili kusajiliwa sa sijajua ni kitu gani kinahitajika ndani ya cheti au rusult slip
 
Pole sana. Hapo ni uelewa wa walimu wako wa taakuma....
Kinachotakiwa ukumbuke kiusahihi namna jina lako lilivyoandikwa olevo ba namba yako....
Kwa kumaluzia....nenda ulikosoma olevo huenda wana kopi badu ya namna jina lako lilivyoandikwa. But ondoa wasiwasi
 
NAMBA YA MTIHANI JINA LAKO LA FORM 4 MWAKA WA KUZALIWA
 
Ndiyo mkuu, si ni namba ile niliyoitumia kufanya mtihani kidato cha nne
Ndio.

Hakikisha unawapa majina yako na namba ya mtihani kwa usahihi. (pamoja na mwaka wa kuzaliwa)

Vinginevyo, majina yakija kutofautiana na cheti cha kidato cha sita itakupa shida.

Zungumza nao.

Kwasababu lengo la kuleta cheti cha form four ni kuhakikisha usahihi wa taarifa zako bila kupunguza wala kuongeza chochote.

Mafanikio mema.
 
Nenda Necta kijana huko ndiko suruhisho liliko. Wahi faster. Lakini uwe umeshaandika taarifa polisi na una RB yako. Mwizi wako anaweza kamatwa fasta akikitumia. Siku hizi uhakiki w vyeti uko kila eneo
 
Back
Top Bottom