Hivi Yanga mbona wanateseka sana na Usajili wa Simba? Wao si ndio walianza kwa mbwembwe mara Balinya, mara Mnamibia mara Lamine Moro mara Mavugo n.k. huku wakibeza kuwa "MO" kagoma kutoa mzigo wa usajili. Sasa kelele za nini tulieni dawa iingie na mpeni haraka Gadiel dau analotaka ili asiondoke au mzigo ndio umeshakata? Halafu muwe na kumbukumbu mwaka juzi mlisema Simba inasajili wazee wakina Boco. Mwaka jana tena mkarudia kusema hivyo hivyo kwa Kagere. Na mara zote Simba kaibuka kuwa bingwa. Mwaka huu tena mmeanza kwa Wabrazili kuwa wazee.
Kwa mtizamo wangu naona tusubiri ligi ianze na kwa kuwa mpira unachezwa uwanjani tena hadharani mbivu na mbichi zitaonekana. Wapo waliosajiliwa Simba watafanya vizuri na wapo watakaochemsha na hata Yanga itakuwa hivyo hivyo ndio hali ya kawaida kwenye mpira na anayeufahamu mpira hawezi kushangaa hili hata Ulaya wachezaji wakubwa limeshawakuta mfano Di Maria, Mateja Kezman, Shevechenko, n.k. Hivi ni kipi bora kuwa na timu ya vijana ambayo haichukui ubingwa au kuwa na timu ya wazee inayochukuwa ubingwa?
Vile lazima mashabiki wajue kuna wavulana na wanaume. Kwenye mpira ukitaka matokeo ya miaka mingi ijayo tumia wavulana na ukitaka matokeo ya muda mfupi tumia wanaume. Simba iliwahi kujaribu kuwatumia wavulana kutafuta ubingwa miaka ya nyuma wakati wakina Mkude, Ndemla, Ajib, Seseme, Edo Christopher, Manyika Jr, n.k lakini walishindwa kwani wakati huo Yanga ilikuwa na wanaume hasa na ndio maana ya sajili zinazofanyika sasa kwa Simba kusajili wachezaji hao mnaowaita wazee.
Pia kwa taarifa tu mashabiki wengi hawajashtukia sajili za sasa za Simba kuwa wameenda mbele zaidi kwa kusajili wachezaji wengi pamoja na uwezo wao pia wameangalia miili mikubwa ili kupambana kwenye champion league hivyo timu za ligi kuu zijipange. Simba inaenda kucheza soka la nguvu hasa si mchezo.
Ila watani zetu Yanga wabishi kuanzia kwenye usajili ila misemo huwa inaisha pale ligi inapokuwa inaenda ukingoni. Hivi kuna anayejua anikumbushe ule msemo wa kila mtu ashinde mechi zake mwisho wa ligi tufanya mahesabu ya pointi tujue nani bingwa uliisha lini?