Hata msimu uliopita Simba ilikuwa na kikosi kizuri kabisa kilichokuwa na uwezo wa kubeba ubingwa wa ligi kuu Bara.
Pamoja na kikosi kuwa kizuri kulikuwa na matatizo makubwa matatu tu yaliyoiponza Simba
1. Kikosi kilikuwa chembamba yaani walioko uwanjani hawana mbadala wa uhakika
2. Kilikuwa hakijawa pamoja kwa muda wa kutosha
3. Hakikuwa na benchi la ufundi imara lililotulia. Kila siku sarakasi mpya
Swali kubwa je hadi sasa viongozi wa Simba wanajua tatizo la msingi la timu au wamezidiwa na pressure ya mashabiki?
Ni ngumu kujua kama kweli wanaelewa tatizo la msingi la Simba maana inaelekea wanataka kufanya makosa yaleyale.
Hawana kocha mkuu hadi sasa, wanasajili wachezaji wengi wapya na kutaka kuacha wengi wa zamani.