Usain Bolt pips Justin Gatlin to win world 100m title

BabuK

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
1,845
329
_85123440_bolt2.jpg


Usain Bolt pipped Justin Gatlin to retain the 100m title at the World Athletics Championships in Beijing.
Bolt had stumbled out of the blocks in winning his semi-final but found a season's best run of 9.79 seconds to win the title for the third time.
 
Justin Gatlin anajitahidi Sana bolt mwenyewe anajua mchuano ulikuwa so wa kitoto
 
Gaitlin kwenye mchuano wa semi final aligonga 9.77s na Bolt alimaliza kwa 9.96 akajiamini atakuwa "mwuuaji wa Bolt" hata hivyo Bolt hujulikana kwa kufanya vizuri akiwa na wapinzani wakali.. Ikatokea.

_85141447_bolt.jpg
 
Pressure zimemuangusha Gatlin,uzoefu wa kutuliza kichwa kwenye matukio muhimu umembeba Bolt.

Gatlin alipiga 9.77 semi final,lakini final anagonga 9.80,huku Bolt akipiga 9.79.Ina maana Gatlin angekirudia kile alichokifanya semi final,Bolt angekuwa anaugulia maumivu saa hizi.

But what happened?Gatlin aliikosea final.Kwa kawaida huyu jamaa huwa anashinda mbio mwanzoni na mwishoni.Mwanzo,huwa na explosive start,na ana acceleration kubwa sana.Mwishoni hujitahidi kutunza speed yake kwa kuminimize deceleration kwa kadri iwezekanavyo.

Bolt yeye mara nyingi ni slow starter,hii ni kutokana na umbile lake kubwa,uzito mkubwa,ila akishafika 60m mark,asiye na mwana aeleke jiwe!

Kwa hiyo ukiweza kumcontain Bolt from 60m to 90m marks,basi una uhakika wa kumshinda.

Sasa final ya juzi Gatlin alikuwa nervous sana,akaharibu silaha yake muhimu ya explosive start,akawa very slow kutoka kwenye blocks.Bolt akabaki na starting yake ile ile,matokeo yake walipofika 50m mark wakawa wapo sawa sawa,na hapo ndipo kosa la Gatlin lilipoonekana.Lile dubwasha likaanza kufunguka hatua zake za hatari,na kuanza kumburuza Gatlin ambaye ni mfupi kuliko Bolt.Baada ya kuona hali ni tete,Gatlin akafanya kosa kubwa zaidi katika riadha,kuiga style ya kukimbia ya mpinzani wake,na yeye akaanza kufungua strides ilhali ni mfupi,badala ya kudumisha style yake ya high frequency cadence(kuchanganya miguu kwa hatua fupi za haraka sana).

Kwa kuzingatia muda mdogo sana waliopishana,yaani 9.79 kwa 9.80,ni wazi hizi minor mistakes ndizo ziliamua final kati ya hawa wawili.Kutokana na uwezo wao mkubwa,ilihitaji kosa dogo sana kuamua mchuano,na Bolt akaibuka mshindi.

Kwa jinsi hali yake ilivyo tete katika siku za hivi karibuni,Bolt amejitahidi sana kugonga 9.79.

Uzoefu wa big occasions umemsaidia.Ulimwengu umefurahia ushindi wa Bolt,ambaye hana kashfa ya doping.Gatlin ni "bad guy" wa track and field,na wadau wa riadha walishukuru kuwa ameshindwa juzi,for the sake of that sport.
 
Usain Bolt is a freak of nature!
yeah!the so called "alpha-actinin skeletal muscle isoform 3(ACTN3)".Utakimbia wee lakini ukikutana na majitu ambayo yamejaaliwa hii kitu(speed gene),utahemea masikioni!Sasa Bolt ni compound ya aina yake;ACTN3 + GIGANTISM uuuuwiii!kweli ni freak of nature!
 
Back
Top Bottom