USAID imeondoka - Nini Kifanyike Sasa

USAID imeondoka - Nini Kifanyike Sasa

Amba Samedi

Senior Member
Joined
Apr 5, 2024
Posts
193
Reaction score
326
Habari wanaJF,
Niko Mzumbe, katika sehemu moja hapa. Usiku usiku nlikuwa najaribu kuweka mambo sawa. Nilipanga mengi, ila nimejikuta nazima moto. Inshallah ntaendelea kesho.

USAID imeondoka rasmi katika utendaji wake wa miaka mingi. Na nchi za Africa zitahisi maumivu makubwa kwa kuwa ndo ilikuwa chombo tegemezi kwa asilimia kubwa.

Nnapoandika haya, nimemaliza project ya website na mobile app ya shirika moja hapa nchini. Developer wao wa zamani aliwachaji 7m na akafanya kazi moja ya kishkaji. Nimetumia chini ya nusu ya hapo nikawapa kitu kizuri mno. Sio kwamba gharama zangu ni za ovyo, bali nlikuwa naokoa jahazi kwa plan fulani ya kesho na keshokutwa.

Kilichonigusa ni kuwa USAID walikuwa wakitegemeza shirika hili kwa 80%, na kuondoka kwao ni pigo kubwa kwa utendaji. Kabla ya hapa, walikuwa na shida ya mishahara. Leo sasa, najaribu kufikiria tutafanyaje. Dada yangu anayefanya kazi pale alipokuja na machozi akiomba msaada kufufua app (ambayo ilipaswa kuongezewa pia functionality), nilimwelewa. Nikatumia njia rahisi na sasa wanakwenda.

Lakini swali linabaki palepale, nini kifanyike? Vipi kuhusu waliotegemea NGO hizi kwa kazi na ajira? Familia zao? Miradi yao? Makanisa.

Hapa nna kitabu chenye title Dead Aid: Why Aid is not working and how there is a better way for Africa (Msaada Uliokufa: Kwa nini Msaada sio tija, na njia bora kwa ajili ya bara la Africa). Limeandikwa na mwenzetu kutoka Nigeria (Dambisa Moyo).

Ntawapa feedback na fikra mbadala cha kufanya ili kuskuma gurudumu.

Na, ili kuonyesha kuwa njia mbadala inahitajika, ntawaambia how nitaapply hii kwenye NGO ninazozishauri moja kwa moja.

Tuonane upande wa pili.

Good night for now,

Signed,
Amba Jnr.
 
Usibiri ya IRAN,Kiduku,china wanakuja na misaada kama hiyo
 
Hatuna namna watoto waende kujisaidia vichakani
 
Mtajuwa hamjui opportunities com and go so keep create
 
Back
Top Bottom