Regnatus Cletus
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,114
- 958
Nimeshawishika kupachika bandiko hili baada ya upotoshaji unaofanywa na mwanajamvi mwenzetu ndugu Barbarosa.
Kama mdau wa sheria, nimeumizwa, na nikapata msukumo wa dhati wa kuliweka jambo hili sawia ili kuzuia udanganyifu wa makusudi.
SHERIA YA ARDHI YA MWAKA 1999, YAANI THE LAND ACT ; KIFUNGU CHA NNE (1) KINASEMA, " ALL LAND IN TANZANIA SHALL CONTINUE TO BE PUBLIC LAND AND REMAIN VESTED IN THE PRESIDENT AS TRUSTEE FOR AND ON BEHALF OF ALL CITIZENS OF TANZANIA.
Kwa lugha ya Kiswahili ni kuwa, "Ardhi yote ya Tanzania itabaki kuwa ardhi ya Umma, na itakabidhiwa kwa Rais kama msimamizi kwa niaba ya watanzania wote.
HIVYO, si kweli kama asemavyo Barbarosa kuwa Ardhi ya Tanzania ni mali ya Rais, na sisi ni wapangaji wake. Rais ni msimamizi wa ardhi yetu watanzania.
KIFUNGU CHA 3 CHA LAND ACQUISITION ACT, YA MWAKA 1967, Kinampa mamlaka Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuichukua ardhi kwa matumizi ya umma.
Na matumizi hayo ya umma yamebainishwa kwa viwango vinavyodhibiti tafsiri yake (it is strictly construed)..... Yaani kuwa matumizi hayo ya umma sharti yawe, aidha kwa shughuli za kiserikali, shughuli za kitaifa, miradi, kilimo, viwanda, biashara, usimikaji wa miundo mbinu, na uchimbaji wa madini.
MATUMIZI YA UMMA SIO TU KWA MATAKWA AU UTASHI BINAFSI KAMA ANAVYOTUELEZA BARBAROSA. MATUMIZI YA UMMA YAMEBAINISHWA KATIKA UTARATIBU WAKE.
IBARA YA 24 (2) YA KATIBA YA JAMUHURI YA TANZANIA INASEMA, "IT SHALL BE UNLAWFUL FOR ANY PERSON TO BE DEPRIVED OF HIS PROPERTY FOR THE PURPOSES OF NATIONALIZATION OR ANY OTHER PURPOSES WITHOUT THE AUTHORITY OF LAW WHICH MAKES PROVISION FOR FAIR AND ADEQUATE COMPENSATION.
Yaani kwa Kiswahili , " ITAKUWA NI KINYUME NA SHERIA, KWA MTU YEYOTE KUNYANG'ANYWA MALI YAKE KWA MALENGO YA UTAIFISHAJI AU MALENGO MENGINE YOYOTE BILA MAMLAKA YA KISHERIA YANAYOWEZESHA FIDIA TOSHELEZI NA YA HAKI".
KIFUNGU CHA 11 CHA "LAND ACQUISITION ACT" YA 1967, KINAMTAKA RAIS AU WAZIRI WA ARDHI KULIPA FIDIA KWA WOTE WALIOCHUKULIWA ARDHI ZAO KWA AJILI YA MATUMIZI YA UMMA. FIDIA HIYO LAZIMA IWE FIDIA TOSHELEZI NA YA HAKI. WATU HAO WANAWEZA KUFIDIWA FEDHA TASLIMU AU KWA KUPATIWA VIPANDE VINGINE VYA ARDHI.
NDUGU WANAJAMVI, TUSIPOTOSHWE NA WATU WACHACHE WENYE MALENGO NA NIA OVU.