Usahihi: VAT kwenye escrow

Nimrod Mkono alitaka tatizo kati ya Tanesco na IPTL lidumu milele ili afaidike. Kumbukeni alichokifanyia BOT kwenye kesi ya Valambhia.

Huyu ndio tatizo, na ni yeyey maswahiba wake ndio wanataka kulisimamisha Taifa bila sababu.

Lakini tatizo kubwa zaidi ni Chikwete.
 
Hadi sasa nikipitia post za watu humu wanaokubali na wanaopinga jibu napata kuwa fedha hizo umma unatakiwa kuhoji kwa maana chimbuko lake ni kutoka kwa wananchi.
 
Mie nasema na ntasema mpaka mwisho,Zitto aliitegemea hii ishu imrudishie kisiasa lakini as aresult ni mpuuzi sana,hata kama ripoti ingekuwa ni sahihi kiasi gani ukianza kuwa bias basi huna tena reputation na hiyo ripoti,yeye pia kahongwa kama wengine na bado ameandaa ripoti kama kukomoa na vijembe vingi ..ameikosea sana kamati kwani kama mwenyekiti naye kala anawezaje akawa msafi wa kuandaa ripoti ya kuwafunga wengine katika ishu hiyo hiyo?
 
Wewe mwizi pia ndio maana unatetea.
 
Naomba kutoa ufafanuzi kidogo

Kama Tanesco hawakupeleka VAT, TRA waibane Tanesco sio IPTL

Kwa mfanyabiashara aliyesajiliwa VAT, anajukumu la kupeleka TRA tofauti kati ya VAT aliyokusanya na VAT aliyolipa au aliyotakiwa kulipa.

Tanesco wakikusanya VAT toka kwetu wanatakiwa wapeleke TRA. Kama katika kufanya biashara yao walilipa gharama zenye VAT ndani yake kama vile capacity charge, wanatakiwa kukokotoa tofauti kati ya waliyopokea na waliyolipa. Kama waliyopokea ni kubwa kuliko waliyolipa, wataipeleka TRA ya juu. Kama waliyopokea ni ndogo kuliko waliyolipa, watatakiwa kuvizia mwezi unaofuata kurecover hiyo deficit kati ya input na output tax. Kwa hiyo kama Tanesco walikuwa wanapata excess ha hawapeleki, wabanwe wao.

Vivyo hivyo na IPTL kama mfanyabiashara mwingine, walitakiwa kila walipopeleka invoice zenye VAT za kuwadai Tanesco, mwisho wa kila mwezi walitakiwa kukokotoa VAT waliyolipia kwenye manunuzi/gharama zao na VAT ya invoice zote walizotoa mwezi husika ikiwa na zile walizopeleka Tanesco. Kama VAT amount ya invoices walizotoa ni kubwa kuliko VAT ya invoices walizolipia gharama, difference walitakiwa wapeleke TRA bila kusubiri eti pesa za Escrow. Kama hawakupeleka, IPTL na TRA wote wawajibishwe. Kama hawakupeleka, na kama TRA walijua, TRA wachinjwe kama hawakuchukua hatua hata ya kukamata mitambo.

Vile vile sikubaliani na wewe kwenye sentensi ifuatayo: Naamini Tanesco walikuwa wanatenga hii pesa baada ya kupokea Tax invoices toka IPTL. Kwa kuwa mnunuaji siyo anayepeleka VAT bali muuzaji (mfanyabiashara, yaani ni IPTL)

Hapa kunielewa. Nilikuwa namaanisha kuwa, Tanesco walikuwa wanapeleka pesa Escrow account baada ya kupokea tax invoice toka IPTL, na hizo zilikuwa na VAT. Tanesco kama mnunuzi, si jukumu lake hapa kuhakikisha VAT ya kwenye invoice zilizoandaliwa na IPTL inalipwa au la. Kama lilivyo jukumu la Tanesco kuwasilisha TRA VAT anayotuchaji sisi kwenye umeme, pia ni jukumu la IPTL kuwasilisha TRA VAT ya kwenye invoices za Tanesco hata kama Tanesco hajalipa au ameweka fedha IPTL.

Itakuwa ni kosa kubwa kwa IPTL na TRA yenyewe kusubiri walipwe fedha za kwenye escrow eti ndio walipe VAT.
Kuna mchangiaji kaongelea suala WITHHOLDING TAX, ambayo ni 5% ya capacity charge before VAT. Hili sasa naliona kuwa tatizo kama halikuzingatiwa haswa na Tanesco wakati wa kupeleka pesa escrow account. Kila walipokuwa wakiandaa malipo ya IPTL invoices na kuhifadhi kwenye escrow account walitakiwa kukata hiyo withholding tax na kuipeleka TRA. Kama hawakufanya hivyo, Tanesco wako liable. Wakati wa kuziiba hizi pesa toka BOT, wezi hawa walitakiwa wacheki na Tanesco kama alikata withholding tax ili kama hakukata, wakate sasa. Kwa wezi hawa alivyo na papara nina wasiwasi kama walicheki na Tanesco.
 

Mh.ukisoma ulivyo andika, ni kama pacha na nilivo andika. Naona zimeunganishwa.

Tuwasaidie hawa watu wajikite kwenye namna zilivyotolewa BOT kabla ya kuisha kwa mzozo wa wa capacity charge ambao ndio chanzo cha kufungua account ya escrow. Tuking'ang'ana na kuwa ni za umma au sio za umma, kuna kodi au hakuna kodi hatufika tunakotarajia kufika maana hakuna kodi ya VAT ndani yake. Hat withholding tax, Tanesco walitakiwa wawe wamekata kabla ya kuzipeleka Escrow account
 

Asante. Hivyo ndivyo ninavyoelewa mimi.
 

Tatizo sasa hivi hili suala limechukuliwa kisiasa. Kila mtu ni mjuzi mradi tu anajua kupiga kelele sana na kutoa matusi makubwa makubwa. Nionavyo mimi ni rahisi kabisa kuujua ukweli wa nini kilitakiwa kufanyika na hakikufanyika. Makabrasha na sheria zote zinazohusu nini kilitakiwa kifanyike na hakikufanyika vipo.

Kuna watu wanafikiri kuwa Rugemalira na IPTL walitakiwa asilipwe kitu chochote ijapokuwa pesa zile ziliwekwa Escrow Account kwa ajili yao.
 

wewe ngoja nikuache tuh,

maana mara unasema hakuna sehemu tanesco walipofungua kesi mahakamani na tena hapo hapo unasema kesi iliyofunguliwa baina ya tanesco na iptl ni ya kiwango cha uwekezaji sasa ngoja nikuache tu uende zako,

unakanusha kile unachokisema,

sasa nakuuliza,kama kweli unakiri na kukubali kwamba ipo kesi ya msingi mahakamani na bado haijamalizika hao waliokaa kunduchi kuidhinisha pesa itoke walitoa kwa amri ya nani??

then tanesco sio ndiyo ambao walikaa huko kunduchi,hujui unachokiongea,,,

waliokaa huko kunduchi ni hao jamaa zako kina muhongo unaowatetea.
 
asante kwa taarifa mkuu na taarifa yako imepokelewa.
 

Usilazimishe mambo, haijawahi kuwapo kesi ya capacity charge, au unadhani watu wakipelekana mahakani basi ni kila tofauti zao zinazungumziwa huko.

sasa kama akina muhongo wanahusika na utawala wa tanesco, hautaki wakae vikao, mnataka shirika liongozwe vipi sasa?
 

Tumia akili wewe.

Hakuna mwenye tatzo na iptl kuhusu energy charge,

Tanesco na Iptl hawana shida kuhusu energy charges,thats why hadi leo wanauziana umeme huo kwa mkataba mwingine mpya kabisa ambao walishaaingia,

Tanesco sio wajinga watumie kitu bila kukilipia,

Ishu ni capacity charges na ndiyo kesi kubwa hii.

Ngoma nguumu hii,

JAMAA ZAKO UNAWATETEA WANA KESI YA KUJIBU KWA WANANCHI,

NOWAY OUT,

MNALO HILI SAFARI HII,MMEKULA PESA YA UMEME LAZIMA IWAPIGE SHOTIII
 
Okoanchi CAG alikuwa sahihi. ESCROW haiqualify kuwa asset kwenye financial statements za TANESCO.Kitu ambacho CAG alifanya 2012 ni sahihi. NOTE DISCLOSURE.kwa sababu kuweka escrow kwenye asset position siyo sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kubwa ni kwanini fedha km ni za halali zigawanywe km chakula wakati wa njaa tajili gani duniani anfanya hivyo?
 
Ndugu Okoachi uchambuzi wako mzuri sana, Hiyo kodi ya TRA ni ya nani? Uliandika vizuri kuwa IPTL ni wakala wa TRA kukusanya VAT kutokana na malipo ya capacity charge, miaka yote hiyo kama hawa kufanya hesabu na VAT ina penalt, huoni huyo TRA(umma) anadai pesa nyingi? Ufafanuzi please!
 
Okoanchi CAG alikuwa sahihi. ESCROW haiqualify kuwa asset kwenye financial statements za TANESCO.Kitu ambacho CAG alifanya 2012 ni sahihi. NOTE DISCLOSURE.kwa sababu kuweka escrow kwenye asset position siyo sahihi.

Ndugu yangu Kanga. Kunapokuwa na mijitu mijizi inayotegea matundu ya kudokolea kama viongozi wetu hawa, tuwe makini maana hutumia tafsiri nyepesi kuiba.

Tanseco walikuwa wanajua wanadaiwa na IPTL na hili deni wakalitambua kwenye vitabu vyao vya mahesabu kama LIABILITY. Deni hili linatokana na capacity charge ya umeme waliopokea.

Kutenga pesa kwa ajili yakulipa baadaye wakati hujui exactly utalipa ngapi (provision)lazima iwe disclosed vizuri. Nimeambiwa ilionyeshwa kama CONTINGENT LIABILITY. JE wakati wa kutoa pesa, najua waliCREDIT Bank/cash, DEBIT entry ilikwenda wapi?

Lakini
 
Samahani kwa kuchelewa kujibu.Ni kweli huyo UMMA yaani TRA anadai hela nyingi sana. Naomba ujue haidai ESCROW Anamdai IPTL. Pesa ilipokuwa BOT iliwekwa ili kusubiri deni lijulikane na ndipo lilipwe na kama IPTL alikuwa anazisubiri ili akalipie malimbikizo ya kodi, basi angefanya hivyo mara baada ya kulipwa.TRA kama walitambua kuwa wanadai walikuwa na nafasi ya kuiambia BOT kuwa wazuie hizo pesa.TRA nao wana kesi ya kuujibu umma, kwa nini hawakukusanya pesa ya kodi in time?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…