Usahihi: VAT kwenye escrow

Tukubaliane kwamba ni mali ya UMA kivipi wakati nimehitimisha kwa kusema sio mali ya UMA. Hoja ya VAT kwenye swala la ESCROW imelazimishwa bila sababu za msingi, na ndio maana nasema sababu zilizopelekea hilo zikijakujilikana kuna watu wanaweza kupondwa mawe mpaka wafe.

Labda uniambie kwamba, TRA waliielekeza BOT au TANESCO wasiilipe IPTL sababu IPTL wanadaiwa pesa nyingi sana na TRA walizozikusanya toka Tanesco alafu hawajaziwasilisha TRA.

Sheria za kodi, zinaipa mamlaka TRA kunyakua mali na pesa za mdaiwa wa kodi kokote inakoweza kuzifikia, kwa sababu hawakufanya hivyo ni wazi hawakuwa na issue na IPTL,
 
Nimeupenda uchambuzi wako. Nakubaliana no isipokuwa nadhani kuna makosa machache umefanya, labda sikuelewa vizuri nieleweshe zaidi.

Kama Tanesco hawakupeleka VAT, TRA waibane Tanesco sio IPTL

Nadhani hapa umechanganya mambo. Unazungumzia umeme unaouzwa na Tanesco au umeme unaouzwa na IPTL? Swala lililopo ni umeme unaouzwa na IPTL, Tanesco akiwa mnunuzi.

Kama unazungumzia umeme unaouzwa na IPTL basi kwa msimamo huo, kama Tanesco watakuja kwako kununua nguzo za umeme, na wewe ukawacharge VAT kama utashindwa kuwasilisha hivyo VAT basi wadaiwe Tanesco. Nikija mimi kununua mbao kwako ukanicharge VAT lakini ukashindwa kuwasilisha basi ni mimi wa kudaiwa? Wataniona wapi? Kuna wangapi wanaokuja kununua vitu kwako kwa siku moja - itakuwa rahii kuwafuatilia?

Vile vile sikubaliani na wewe kwenye sentensi ifuatayo: Naamini Tanesco walikuwa wanatenga hii pesa baada ya kupokea Tax invoices toka IPTL. Kwa kuwa mnunuaji siyo anayepeleka VAT bali muuzaji(mfanyabiashara, yaani ni IPTL)

Nakubaliana na wewe hapa:
basi hakuna tatizo lolote kulipa IPTL pesa yote bila kupunguza kodi yeyote, laba ka TRA waliiagiza Tanesco kuwa wakara wa kuikusanyia kodi zote za IPTL, vinginevyo hakuna kosa.

Hakuna fedha za umma kwenye escrow, IPTL kama ni wakala wa kodi basi kodi itatolewa full stop.
Sijakuelewa mkuu! Tanesco wanasema walikuwa wanalipa pesa escrow pamoja na VAT component yake. Kwa hivyo unasema hiyo VAT sio ya umma? IPTL ana uhalali gani wa kukusanya VAT na kuitumia katika matumizi yake?
 
Mgogoro ulitatuliwa kwa taratibu walizojiwekewa kwenye kikao kunduchi beach hoteli. wewe unapaswa kuwauliza Tanesco, kama walikuwa hawakubaliani na invoices ni kwa nini walikuwa wanapeleka hela escrow, Upumbavu wao uko hapo tu.

muda wote walikuwa wanalalamika na kuomba pesa serikali za kujiendesha lakini wanakwenda kuweka pesa in deposit bot, hizo ni akili au matope? wao hawakuwa na accounts za kuweka hizo pesa? au walikuwa na excess liquidity?
 
Naomba kuuliza kama pesa za VAT ni mali ni mali ya nani .TRA ni executive agency ya wizara ya fedha .Wizara ni sehemu ya serikali.Serikali ni sehemu ya umma.Kama sio mali ya umma na kama taasis inaweza kwenda kudai tu basi kwa hasara aliyosababisha Mh Mramba miaka ile aachiwe tu halafu TRA ikaidai allex Stewarts hizo hela B 11.7 yaishe na mzee wa watu aendelee na Precision air na ubunge wake
 
Sijakuelewa mkuu! Tanesco wanasema walikuwa wanalipa pesa escrow pamoja na VAT component yake. Kwa hivyo unasema hiyo VAT sio ya umma? IPTL ana uhalali gani wa kukusanya VAT na kuitumia katika matumizi yake?

Ukiambiwa leo kwamba IPTL inaidai TRA pesa za VAT, utajisikiaje?
 
TANESCO KASAJILIWA.
Si tu ni mnunuzi mkubwa bali pia ni muuzaji mkubwa wa Umeme.Alitakiwa a-withold tax na kupeleka TRA

Sheria ya VAT inasemaje? Nijuavyo mimi kua sheria kadhaa za kodi zinazomtaka mlipaji "to withhod tax payable", mojawapo ni ya PAYE. Kama hakuna sheria kama hiyo kwenye swala la VAT lisitupotezee muda wetu. Tujifunze kuona sheria kama zilivyo.
 
Kuna madhara ya watu kuwa wataalamu wa vitu wasivyovijua......

VAT inakatwa katika jumla kuu ya malipo. Tanesco wangewezaje kujua VAT kama bado hawakuwa na hakika ya kiwango cha pesa walichotakiwa kulipa IPTL? Kumbuka kodi ni ''percentage ya total amount'' na wala sio flat rate!!!
Kwa kifupi hata kama TANESCO wangelipa shilingi 10 kwa IPTL ndani yake ipo kodi ya V.A.T

Jambo la pili, kwa kuruhusu pesa kutoka ina maana kuwa TANESCO wanakubaliana na kiwango cha capacity charge walichotozwa na wanachotozwa, kwa hiyo wameamua kesi wenyewe kwa hasara yao.

Bado huoni kuwa hapo kuna hujuma imefanyika?

Ninachoweza kusema ni kuwa huitaji kuwa vyama vya upinzani kuona hili. Hii ganji iliyotoka ni faida ambayo iptl wameipata kwa kutoza capacity charge kubwa.
Hela ya biashara inapogawiwa kama gawio la faida kwa wanahisa wenye akili lazima wahoji?
 
Upo sahihi kabisa, kuwa ndani ya ile pesa iliyokuwa ndani ya Escrow account, kulikuwa na VAT iliyolipwa na TANESCO. VAT ile ni pesa ya serikali, ni pesa umma. Na hiyo ilifafanuliwa vizuri sana kwenye PAC ripoti.

Uko huru.

Ngoja niendelee na shughuri zangu.
 
Mkuu SMU. kuna madhara ya watu kuwa wataalamu wa vitu wasivyovijua......

VAT inakatwa katika jumla kuu ya malipo. Tanesco wangewezaje kujua VAT kama bado hawakuwa na hakika ya kiwango cha pesa walichotakiwa kulipa IPTL? Kumbuka kodi ni ''percentage ya total amount'' na wala sio flat rate!!!
Kwa kifupi hata kama TANESCO wangelipa shilingi 10 kwa IPTL ndani yake ipo kodi ya V.A.T

Jambo la pili, kwa kuruhusu pesa kutoka ina maana kuwa TANESCO wanakubaliana na kiwango cha capacity charge walichotozwa na wanachotozwa, kwa hiyo wameamua kesi wenyewe kwa hasara yao.

Bado haoni kuwa hapo kuna hujuma imefanyika?

Ninachoweza kusema ni kuwa huitaji kuwa vyama vya upinzani kuona hili. Hii ganji iliyotoka ni faida ambayo iptl wameipata kwa kutoza capacity charge kubwa.
Hela ya biashara inapogawiwa kama gawio la faida kwa wanahisa wenye akili lazima wahoji?

Nimekuelewa, ndio sababu sikutaka kuendelea mpaka kwanza tukubaliana kuwa ni za umma ama siyo za umma. Je unakubali kuwa IPTL katika transaction hii alikuwa ni wakala wa kukusanya VAT kutoka Tanessco?

Labda uniambie kwamba, TRA waliielekeza BOT au TANESCO wasiilipe IPTL sababu IPTL wanadaiwa pesa nyingi sana na TRA walizozikusanya toka Tanesco alafu hawajaziwasilisha TRA.
Yes, soma report ya CAG/PAC. Kwa ushauri wa AG, BOT an wengine waliohusika kuzitoa pesa hizo walikataa kutii matakwa ya TRA. Walivunja sheria ya VAT (soma sura 32 yote ya Cap 148).

Sheria za kodi, zinaipa mamlaka TRA kunyakua mali na pesa za mdaiwa wa kodi kokote inakoweza kuzifikia, kwa sababu hawakufanya hivyo ni wazi hawakuwa na issue na IPTL,
Waliomba BOT wazuie kodi hiyo kabla ya kullipwa IPTL lakini AG kinyume na sheria akakaidi/akaisamehe.
 
Sikubaliani na wewe labda uniambie kuwa katika kila invoice waliyokuwa wanawapelekea TANESCO kila mwezi hamkuwepo swala la VAT. Kama kulikuwepo na VAT, basi kiasi hicho cha pesa siyo mali ya IPTL bali cha serikali (TRA). Nashangaa kwa nini hadi leo hii TRA hawajadai pesa zao kutoka IPTL na kuchkua hatua inayotakiwa kama wanavyofanya kwa kampuni zozote zile.
 
= ghilba
= yanajulikana
= wakala

Hayo uliyosema ni sawa na si sawa, Jee, unawea kutuonesha invoice zilizotumika tuone kama zina VAT?

Kuna uwezekano TANESCO walisema wako VAT exempted kwenye mradi huu na wakapeleka pesa bila VAT, uwezekano huo upo kwa kuwa huu mradi mkataba wa IPTL ulianza kabla ya sheria ya VAT.

Lazima kuna technicalities na hilo si tatizo kubwa kwani mitambo ipo, TRA ipo, Mikataba ipo, IPTL hawajalipwa pesa zote wanazodai, ni jambo la kukaa chini TRA na wakala wake na kulitatua. Si jambo la kusema pesa zilizowekwa escrow ni za umma. Hapana, hayo yalikuwa malipo rasmi ya huduma waliyopewa TANESCO na hizo pesa ni za IPTL.
 
sasa kama unajua Tanesco walipaswa kudai kodi IPTL kwa nini unasema zile pesa ni za UMA? Kumbuka ukisema ni za UMA unamaanisha kwamba hazikupaswa kulipwa kwa IPTL.

Msiongelee mambo ya hela kinadharia nadharia, ndio maana tunakuwa masikini. Hela ni Hela. Hela iliyopaswa kwenda IPTL hata kama kuna VAT ni hela ya IPTL.

Wewe unalazimisha eti ni za uma kwa sababu tu neno VAT linatajwa nazo?
 
Ukiambiwa leo kwamba IPTL inaidai TRA pesa za VAT, utajisikiaje?
Nitataka kujua ni kwa vipi? Najua zipo sababu za kampuni kuwa kwenye VAT refund position. Kama zipo na zinaeleweka sina tatizo. Lakini VAT refund najua inao utaratibu wake na katika huo utaratibu ni lazima madai hayo yathibitishwe na CPA-PP.
 
Unapoteza muda wako huyo Sangarara ana lake jambo sio wa kutokuelewa.
 
I agree with you.
siwezi kuonyesha kama invoice zilikuwa na VAT, labda Mkurugenzi wa TRA asaidie sababu ndo aliwaambia PAC kwamba kuna VAT humo, mi najidili taarifa iliyo mezani.

Huo usahihisho wako wa rugha, nitauhakiki kwenye kamusi nikirudi nyumbani reo jioni.

Tatizo langu ni moja tu.
Lugemalila alikuwa amechanganyikiwa hadi kuanza kutapanya mipesa mingi kiasi kile namna hile?
 
Nitataka kujua ni kwa vipi? Najua zipo sababu za kampuni kuwa kwenye VAT refund position. Kama zipo na zinaeleweka sina tatizo. Lakini VAT refund najua inao utaratibu wake na katika huo utaratibu ni lazima madai hayo yathibitishwe na CPA-PP.

with all this understanding, what makes you think those funds were public funds? peer pressure?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…