USAHIHI: Kilichotokea kati ya Juliana Shonza na Wabunge wa Upinzani kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma

una uhakika kama kweli wewe Juliana, mbona nasikia ulimtukana yule mama anayeweza kukuzaa mbunge wa chadema? ukiheshimu watu na wewe utaheshimiwa, wapange mkakati wa kukudhuru wewe ni nani, mbona wapinzani mnawaona maadui jamani, na wao ni binadamu kama wewe, kumbuka cheo ni dhamana, hapo umeteuliwa je ungechaguliwa na wanachi ungekuwaje, unajiita unbreakable, haya mama, ila mark ur tongue, mie sijawahi sikia hata siku 1 watu wakashughulika na wewe, kuna agenda ya wao na wewe imejificha, lakini muda utasema wacha tusubiri,
Nimekuja kusahihisha kile ulichokisikia, siwezi kuanza kutukana watu bila sababu za msingi, mimi sio kichaa. Na kuhusu heshima hilo ndilo vazi langu.

Ingefaa zaidi kuwauliza waliopanga njama hizo, wangekusaidia kujua kwanini wamepanga kunidhuru lakini jambo lingine la ziada nitakalokukumbusha ni kuwa, hapo zamani za kale aliwahi kukamatwa mtu na sumu akitakiwa kumwekea Zitto.
 
Na nyie wanyiha kwa maneno na kupenda kuonekana, nakushauri tu kuwa siasa ni kama upepo hujui kesho yake usijaribu kushindana na wenzio we ulijuaje adhabu haikutosha? Mi naona ulikuwa unataka kumkomoa Halima
Lazima kuna kitu nyuma ya pazia
 
Wanajamvi,
Kwa muda sasa nimekuwa kimya sana kuchangia na kushiriki mijadala mbalimbali inayoendelea kwenye jamvi letu hii ni kutokana na majukumu yanayonikabili ikiwemo kazi pamoja na shule. Nalazimika kurudi tena jukwaani kutolea ufafanuzi wa kile kilichotokea jana katika viwanja vya bunge kwani nimepokea simu nyingi na ujumbe mbalimbali, na kwa maelezo yao nimegundua kuwa upo upotoshaji mkubwa wa kilichotokea na kinachoendelea. Katika hali kama hiyo busara yangu ikaniongoza kuja kulitolea ufafanuzi.

Mtakumbuka kuwa siku ya jumatatu ya tarehe 5 June, 2017 Bunge liliazimia kumsimamisha Mbunge Halima Mdee kwa kipindi cha Mwaka mmoja, na azimio hili lilitokana kwa kiasi kikubwa na hoja yangu ya kutaka Mhe Halima aongezewe adhabu ambayo mara ya kwanza ilikuwa ni ndogo na isiyofanana na aina ya makosa aliyoyafanya. Kitendo iko kiliwaghadhibisha wabunge na viongozi wa CHADEMA, hivyo wakakutana mjini Dodoma na kupanga mikakati ya kunidhuru. Kama kawaida nikapata taarifa hizo mapema sana hata kabla ya kikao chao hakijaisha nami nikachukua hatua ya kwenda kuripoti katika vyombo vinavyohusika na Ulinzi na Usalama wa raia kuwa upo mkakati wa aina hiyo, hatua hiyo iliwafanya washindwe kufanikisha mkakati wao. Hivyo tangu hapo wakawa wanafikiria mbinu nyingine za kutaka kunishughulikia.

Kilichotokea jana ni matokea ya kufeli kwa mipango yao ya kidhalimu dhidi yangu, jana walidhihirisha wazi wazi kilichomo ndani ya vifua vyao juu yangu. Jana, nimeshambuliwa, kwa mara nyingine tena nimetukanwa na kudhalilishwa tena ndani ya viwanja vya bunge.

Nimesikitishwa na vijana waliotumwa kuja kunishambulia, hawakuja kwa bahati mbaya bali ni sehemu ya maelekezo waliyopewa, nao kama kawaida bila kufikiria athari ya maelekezo hayo wakaamua kuyatekeleza na kuja kunishambulia na kunidhalilisha, tena wengi ni wabunge Vijana ambao mimi siku zote nimekuwa nikiwaheshimu na kuwafanya wenzangu, nikiamini kuwa Viongozi Vijana tuna mzigo mzito mabegani mwetu wa kuongoza kizazi cha leo na kesho, na ili tufike mbali hatuna budi tutembee na kizazi chetu na tushirikiane baina yetu. Inasikitisha kuona Vijana kwa mara nyingine tena wanakubali kutumwa kumshughulikia kijana mwenzao. Taarifa kuwa nimeshambuliwa na watu wazima hazina ukweli wowote, ni vijana waliotumwa.

Naomba niwakumbushe jambo moja, miaka 5 iliyopita nikiwa na umri wa miaka 25 tu nilikuwa na UJASIRI wa kupambana na aliyewatuma jana, i dare to stand against ur so praised DEMIGOD, and i made my way out victoriously.

Naandika historia yangu kwa mkono wangu, U should always be alarmed and alerted mkitumwa kushughulika na mimi, i have never been soft in my life, go easy on urself. Wapo wanaoitengeneza historia, kuna wanaoiandika na wapo wanaoitazama historia ikitengenezwa na kuandikwa.,mmeamua kuendelea kubaki watazamaji.

Ingefaa zaidi kushughulika na Chama chenu kuliko kushughulika na JULIANA, i am just UNBREAKABLE.

Pambana dada hakuna wakukubabaisha!!
 
Dada yangu na wanachama mwenzangu maisha ni tofauti na unavyofikiria ukiwa kama kijana weka akiba Maneno na jeuri kumbuka pasipo upinzani usungejulikana kama ulivyo upata Ubunge wa kuteuliwa hukutegemea. Nakupa wazo moja tuu hivi Nape ni mtu kuonekana hana maana ndani ya chama wewe na Nape nani zaidi ktk siasa za Nchi hii basi jitahidi kutojijengea maadui. Mwangalie ndugu yangu February anavyojitahidi kuyabadilisha maneno aliyewahi kuyasema na sasa anayakanusha lakini hayakanushiki uhuru wa habari ni wa muhimu ndo maana na ww umekuja kujitetea huku
 
Kwani hatukuona taarifa ya habari unakuja hapa na braa braaa,halafu una kipi cha ziada labda kwa mfano KIKUBWA cha watu kukupangia njama, au ww una nidhamu ipi nzuri,umeandika ujinga mtupu tulidhani utaweka na picha ama clip kidogo ili tuone nani mkosaji kati ya wale walotaka kukushambulia na ww, halafu hivi waweza pigwa tu bila kosa,nyie mafisiemu hamjitambui kabisaaaaa
 
Unaona ulivyojidhalilisha?
Picha hazidanganyi hizo...
498f948871a871c39b12e477463c83fb.jpg

7b19da0a3c0a0bcff7e8f643a983e637.jpg

2897343b75632c4a336ed32bf4209efc.jpg

0f26c90b22f1e95a48acae1b374a3bd7.jpg

827492a6d3daa6a8c7d12273705a21c7.jpg
 
Dada yangu na wanachama mwenzangu maisha ni tofauti na unavyofikiria ukiwa kama kijana weka akiba Maneno na jeuri kumbuka pasipo upinzani usungejulikana kama ulivyo upata Ubunge wa kuteuliwa hukutegemea. Nakupa wazo moja tuu hivi Nape ni mtu kuonekana hana maana ndani ya chama wewe na Nape nani zaidi ktk siasa za Nchi hii basi jitahidi kutojijengea maadui. Mwangalie ndugu yangu February anavyojitahidi kuyabadilisha maneno aliyewahi kuyasema na sasa anayakanusha lakini hayakanushiki uhuru wa habari ni wa muhimu ndo maana na ww umekuja kujitetea huku
Awashukuru sana David Silinde na Joseph Mbilinyi Sugu walifanya ajulikane , naona kama anasahau alipotoka ila ndo kawaida yetu watz tunasahau mapema mno. Namshauri ajikite katika kutatua matatizo ya watu wa Songwe na siyo kupenda siasa za majitaka hizo
 
Back
Top Bottom