R Mbuna
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,295
- 5,458
SALAMU ZENU WAKUU.
Leo nimepatwa na hasira sana kwa hii huduma mbovu inayotolewa na shirika letu la reli Tanzania (TRL) kwenda mikoa ya Bara. Nilikata tiketi ya kwenda Kigoma kwa daraja la pili kulala( second class sleeping) kwa bei yao ya ofa ya shilingi elfu 60/= wiki moja kabla .
Leo ndio ilikuwa siku ya safari sasa cha kusikikitisha na kama sio kuaibisha ni pale tuliwasili stesheni ya gari moshi karibu na makao makuu ya polisi wenyewe wanapaita central Dar es salaam kwa wakati tuliopangiwa kwenye tikiti husika tulipoambiwa kuwa safari leo haitokuwepo mpaka hapo kesho kwa sababu kuna ajali imetokea maeneo ya Mikese/Kingolwira.
Hivyo kwa sababu hiyo safari imeghairishwa mpaka kesho na wakasema kuwa hawana huduma ya choo kwa pale hivyo wasafiri wote wanashauriwa warudi nyumbani kwao waje kesho muda ule ule kwa ajili ya safari.
Kilichonigusa hapa ni hiki kitendo cha wahusika kutojali kuwa kuna baadhi ya wasafiri wanatokea mbali eidha ni visiwani huko Zanzibar au maeno ya mbali hapa hapa Dar es salaam. Hivyo basi wao wawapa majibu rahisi ya kuwaambia warudi kwao waje kesho bila kujali kama hawa watu bajeti yao ya safari itaharibika kwa sababu kwa mtu wa kutoka visiwani lazima ataenda kulala hotelini tu leo bila kupenda.
Naomba tu serikali iwe inaangalia na inakuwa na mbadala kwa dharura kama hizi zinapotokea ili watu wasiumie sana kwenye gharama ambazo hawakujiandaa nazo kwa wakati huo.
Siku njema wakuu.