Bin Chuma75
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 1,002
- 1,092
Napenda kushare nanyi jambo moja ambalo ninauzoefu nalo sana, ndugu zangu wenye magari madogo hasa private kwa sasa epukeni safari za usiku kutokana na mabasi kuruhusiwa kutembea masaa 24.
Kutakusaidia kuepukana na ajali zisizo za lazima. Iwapo ukikutana na basi akikuletea upande wako kidogo tu ni rahisi kujiingiza uso kwa uso au kwenda nje mazima, sababu ni vigumu kuchagua pa kupita kwa ghafla maana macho yako yanaishia mwisho wa taa zako tu.
Ninauzoefu wa barabarani kwa magari yote (mabasi, malori, gari dogo) zote hizi nimeendesha kwa miaka mingi ndani na nje ya nchi. Hivyo nimeona nitoe ushauri kidogo kwa wenzangu tunaopenda safari za usiku.