Usafiri wa bus mbezi_morogoro rd | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafiri wa bus mbezi_morogoro rd

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mfwakwa, Jun 1, 2010.

 1. m

  mfwakwa Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: May 31, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimeshangazwa na usafiri wa mbezi. Nilikuwa nasafiri kutoka posta mpya kuelekea mbezi kwa msuguli, nilishangaa nilipofika kituo cha posta majira ya saa 11.30 nilikuta watu wamefurika sana; bahati nzuri akatokea abiri mmoja akanishauri nihame nikapandie bus kituo cha akiba then nirudi posta halafu mbezi; nilikubali nikaondoka naye hadi akiba; pale pia kulikuwa na abiria wengi sana; nikaamua kupanda bus ya ubungo inayoingia kwanza posta; nililipa 250/= then posta nikalipa tena 250/= hadi ubungo. nilipofika ubungo nilishangaa zaidi bus nyigi zinazoanzia ubungo zinaishia kimara. ok niliingia kwenye bus ya ubungo-msata nilitoa 1000 nikamweleze konda naelekea mbezi; alifoka na kuniambia gari ya shamba hii ila inaenda kulala inaisha kimara; nikamwambia well kama itaendelea nitaendelea kama itaishia kimara sawa, alichukua 250/= tulipofika kimara pale napo watu walikuwa wengi sana alifika pale akashusha watu wote then akaaza safari upya uzuri na mimi nilifanikiwa kuingia nikalipa tena 250/ kutoka pale ile gari ilienda hadi mbezi tuliposhuka akachukua tena watu pale kuelekea kibamba kwa 200/ SAFARI KUTOKA POSTA HADI KIBAMBA 250AKIBA+250UBUNGO+250KIMARA+250MBEZI+200KIBAMBA=1200/= anayepand bus ni mshahara wa kima cha chini; KWELI ATAFIKA?:confused2:
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maisha bora kwa kila mtanzania ndo hayo Mfwakwa..........................
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nakushauri ununue tuktuk tu utapunguza gharama hizo ukiweka full tank wese unasahau.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,170
  Trophy Points: 280
  Tanzania yenye neema ni hii ya kikwete
   
 5. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kweli kasi mpya, Mtu wa Kima cha chini aweze wapi maisha haya bila kuwa na cha pembeni? Hata hiyo pikipiki yenyewe inahitaji mafuta ambayo kwa sasa yamesimama kwenye 1700 ukitumia lita mbili kwa siku, ni sawa na lita 44 kwa siku 22 za kazi ona sasa mshahara usivyotosha. TUCTA fanyeni mabo hapo hapajatulia.
   
 6. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,464
  Likes Received: 1,401
  Trophy Points: 280
  hali ya usafiri kwa dar es salaam kwa ujumla ni mbaya
   
 7. m

  mfwakwa Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: May 31, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Fidel, kima cha chini 150,000 tukutuku ni more than 3m litanunulika?
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Na kaburi aandae; weye unajua jinsi tukutuku ilivyo risk hapo mjini!
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mabasi yaendayo kasi, mwaka kesho yatapunguza kero za dala dala
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  mfwakwa,

  hayo maisha mbona tumeyazoea sasa :

  Kutoka Posta hadi Mbagala Rangi Tatu - unapanda mabasi manne (250 x 4)
  Kutoka Posta hadi Bunju - Magari matatu (au Mawili kama utapanda ya Bagamoyo = 300 +1600)
  Kutoka Posta hadi Gongo la Mboto - Magari manne au matano (250 x 4/5)
  Kutoka Posta hadi Tabata (Mawenzi/Chang'ombe/Kinyerezi/Segerea) - Magari manne (250 x 4)

  List inaendelea

  Hayo maeneo niliyokutajia ni "one-way" kwahiyo ukitaka kupata gharama halisi zidisha mara mbili kwa siku mara idadi ya tegemezi (dependants)!
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Itabidi tusubiri 2018 ili mshahara uopande kama alivyosema mkulu
   
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...kuna mengi yanayochangia katika hili lakini nadhani kubwa ni hili la kumruhusu kila mwenye basi lake kuwa msafirishaji wa abiria jijini. Mwanzisha thread amesema kuwa 'Kondakta akafoka', hii ni kutokana na hili ninalolisema. Usafirishaji wa jiji kama la Dar ulitakiwa ume ni Kampuni rasmi kwa Mfano UDA, kama watu wasingeihomola. Ingesaidia sana kupunguza matatizo ya Wahuni wanaokatisha ruti na wafanyakazi wasiokuwa na adabu kwa watu wanaowapa kula yao! kibaya zaidi ni kuwa hao hao wenye mamlaka ya kuondoa uozo huu ndio hao haowenye kumiliki hayo mabasi yanayokatisha ruti. Ni a vicious circle. Poor We!
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahaha!kumbe mfwaka unakaa mbezi eeh!?
  sasa tukutane pale SUN-SET jioni ya ijumaa tuyajadili haya matatizo huku tukizitiririsha
   
 14. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tatizo la usafiri wa Tz hasa Dar ni biashara huru iliyokaa mfumo wa kiholela mnoo
   
Loading...