Usafiri bora na wa kisasa kwenda Arusha

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,650
3,662
wadau naulizia usafiri bora na wakisasa wa bus wa kwenda Arusha,liwe kama modern coast express au shabby line vip. ndani kuwe na wi-fi socket charger na tv kama kuna bus muundo huo nijuze
 
Panda al hushoom au ndekule basi yapo safi sana pia lipo lingine laitwa mwanamara aka ngoreme bus
 
Kitu kimoja usifanye usipande mabasi yanayoondoka kuanzia saa tatu asubuhi,yote Ni mabovu
Yanasanya njia nzima daladala nyuma,badala ya kutumia saa Saba kufika yanatumia saa kumi.
Hasa ukisikia wahudumu wake wanaongea au kuwa na lafudhi ya Kipare jua ndio yenyewe
 
Mkuu nimepiga safar nying za kwenda a town,nilijuta simu nilipokata ticket ya bus a nilodhan litakuwa luxury nikapandishwa bus b safar ya Saa kum na mbil asubuh nkafikishwa a town SA tatu kasoro 9t,tangu Usiku hiyo nipo making na haya mabus,jaribu kupanda Kilimanjaro nadhan wako vizur,wako on time
 
Kilimanjaro ni ya kawaida sana hawana charging systeam, no AC , kampuni yenye mabasi yenye AC zinazo funguliwa kuanzia Dar hadi Arusha ni DAR EXPRESS ila sio DAR EXPRESS zote, Tahmeed hili ni jipya kabisa la Dar to Arusha na lipo Dar to Nairobi ila Dar express hazina charging systeam. Mengine yote full usanii AC inawashwa mara izimwe. Ila kuhusu huduma za ndani za kugawa soda na maji na biscut mabasi karibia yote yanafanana hakuna utofauti,
 
Au panda modern cost la Dar to Nairobi hilo ni full luxury au Tahmeed la Dar to Nairobi.
 
Nachukia sana mabasi yanayopiga muziki au kuonyesha movie hovyohovyo...Kwa hilo tu niliwapenda Kilimanjaro.

Zaidi ya hapo naona yote huduma zinafanana
 
Kilimanjaro za kawaida sana sijaona utofauti wao, labda kwamba hayana wapiga Debe ila kwa huduma n za kawaida sana Maji na soda na keki labda ndo vinavutia watu. Halafu mabasi karibia yote Customer Care mi tatizo kubwa sana, ukichunguza wale wa hudumu wote utakuta wana uhusiano wa karibu sana na wamiliki wa mabasi either mjomba, baba mdogo, babu, shemeji, jirani, baba wa ubatizo, shangazi na kazalika. hivyo unakuta ni full kiburi lugha mbaya kwa wateja.
 
Kamata fastjet kata ticket miezi 4 kabla ya safari utaipata kwa bei rahisi.
 
wadau naulizia usafiri bora na wakisasa wa bus wa kwenda Arusha,liwe kama modern coast express au shabby line vip. ndani kuwe na wi-fi socket charger na tv kama kuna bus muundo huo nijuze

Jaribu MV Spice Islander Mkuu.
 
wadau naulizia usafiri bora na wakisasa wa bus wa kwenda Arusha,liwe kama modern coast express au shabby line vip. ndani kuwe na wi-fi socket charger na tv kama kuna bus muundo huo nijuze
Chukua boda boda
 
Back
Top Bottom