Usafiri binafsi kwenda mtwara toka Dar

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,658
13,485
Waungwana nauliza kama naweza kwenda na usafiri binafsi Dar to Mtwara. Napenda kusafiri usiku vipi usalama wake utakuwaje kwani kulikuwa na matukio ya kibiti ambayo sifahamu yaliishaje
 
Kwa kutokea Dar Kibiti mbona unapita mapema sana wakati magari bado yapo kibao njiani, au unamaanisha usiku wa sa ngapi.
 
Hamna shida hata kidogo kusafiri usiku labda swali lako limekosa maelezo yanayojitosheleza.
Kwanza safari yako unategemea kutoka Dar kuanzia muda gani?
Je utatumia gari ya aina gani?
Je ni mara yako ya kwanza kwenda mtwara?

Kuhusu usalama hali ni shwari sana mimi mwenyewe huwa naenda masasi muda wowote ninaojisikia na sijawahi kupata matatizo ya usalama
 
Gari ndogo nataka kuondoka jioni saa 10 jioni
 
Muda wowote tu ondoka hata saa 12 jioni usisahau energy drink chupa 2,maana ujue hapo, Lindi saa 9 alfajir mtwara utaingia asubuhi Jua limetoka. Kuwa mwangalifu kuna mashimo ya ghafla barabarani
Bara Bara ni nzuri hasa baada ya kulimaliza daraja la mkapa nyamwage hadi somanga barabara ina kiwango kizuri kuliko barabara yeyote ile Tanzania hii
 
Km hujaondoka pitia mbagara pale utampata binti wa kimakonde ukamwage uno Mnazimmoja huo muda mzuri sana maana tochi zinasumbua kuanzia Nangurukuru mpaka Lindi wanajificha polini.Usalama ni mkubwa kuwa makini na vijana wa Dangote tu wanakula sana mmea
 
Unasafiri lini na upo na gari aina gani kama unatumia tyre low profile uwe tu makini barabara ina shimo sana kila km 20 lazima ukutane na lori za dangote na zile zinazobeba ufuta zina mwanga mkali sana so watchout
 
Ok,nasafiri na rav4...kilometer mbaya ni za kipande gani
 
Back
Top Bottom