Usafi wa Mazingira ya Jiji la Dar.

Usafi wa Mazingira ya Jiji la Dar.

Common man

Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
15
Reaction score
0
Ni nani anapaswa kulaumiwa kuhusu uchafu ulivyozagaa katika Jiji? Hivi karibuni nilisafiri na kuingia katika Jiji hili ambalo wengi wanasema ndilo sura halisi ya Tanzania. Kwanza nikiri kuwa nililazimika kununua karanga kwa machinga/mchuuzi. Aliniwekea kweye kifungashio chake. Mara baada ya kula karanga nilikuwa natarajia niikute mahali pakutupa taka ili nitupe kile kifungashio cha ajabu sikupata mahali rasmi pa kutupa.
Kama kweli kuna haja ya kuweka mazingira ya jiji safi basi mbona hakuna sehemu maalum za kutupa taka? Hivi viongozi wa ngazi zote hawawezi kufikiri na kulitatua tatizo hili? Jiji linanuka, linachafua sifa ya nchi.
 
Ndo hivo bana,linanuka kweli ila kila anae kuja na kusikia harufu mbaya haondoki na wala hasafishi!

Utazoea tu na maisha yanasonga
 
Ndo hivo bana,linanuka kweli ila kila anae kuja na kusikia harufu mbaya haondoki na wala hasafishi!

Utazoea tu na maisha yanasonga
Nionavyo mimi tatizo ni utamaduni. Hata Meya wa Jiji amekulia huko vijijini. Ameishi na mifugo ndani ya nyumba. Uwanja wote nje umejaa mavi na mikojo ya mifugo. Akifika mjini huo uchafu hawezi kuuona kwa sababu hali ya mjini ni mara kumi bora ya ile aliyoiacha huko bush kwao. Kuna Msemo "unaweza kumtoa Mmasai porini lakini huwezi kutoa pori ndani ya Mmasai". Hata huko sehemu za wazito utakuta mtu anakaa kwenye jumba kubwa, ndani ni kama uko New York au London. Ukitoka nje ya uzio tu ni kama uko Manzese. Barabara ya kufika kwenye hekalu ni kama kichochoro cha ng'ombe. Na mheshimiwa haoni shida. Kwa hiyo mimi nasema Dar si chafu ila wanaoishi Dar ndiyo wachafu.
 
Back
Top Bottom