Usafi wa jiji:Wananchi kukimbizana na mgambo kila kona ya Dar es salaam

more88

JF-Expert Member
Apr 9, 2016
447
412
Takribani wiki moja sasa mgambo wa jiji wamekuwa wakikagua usafi maeneo mbalimbali ya jiji lakini zoezi hili sasa linaenda kuwa kero kwa wananchi maana wanatoza fine kubwa sana ya sh 50,000 na hali ya sasa ya wananchi kwa kweli ni kiasi kikubwa sana kwa walala hoi! Biashara nyingi sana zimefungwa kwa watu kuogopa mgamboo wa jiji,, nimekaa sehemu naona wananchi wamebebwa kwenye bajaji kupelekwa serikali za kata kulipia fine,
Vipi zoezi hili katika maeneo mengine wadau ??
 
Sijajua maana ya usafi. Vitu vimepangwa barabarani kama bidhaa. Huo si uchafu? Kwani neno uchafu una maana gani? labda tuanzie hapo. kama maana ya uchafu ni kitu kutokuwa ktk mahala pake basi jiji lote ni chafu. sasa watamtoza nani faini wamwache nani?
 
Weka mazingira yako salama hutasumbuliwa.Ukweli wewe ukienda Moshi - Kilimanjaro watakuweka ndani
 
Ili Dar iwe safi waondolewe machinga na wafanyabiashara kando ya barabara afu ziwekwe bins za taka
 
Back
Top Bottom