Nchi haijengwi kwa njia moja sasa unaposema "nipe mfano wa nchi iliyojengwa namna hii dunini" inakuwa una simplify a complex array into a simple construct.
La kama unaongelea nchi kujengwa kwa namna hii pamoja na nyingine, hakuna nchi ambayo haijajengwa kwa namna hii. Hata vuguvugu la uhuru Afrika lilichochewa sana na askari waliorudi safari baada ya kupigana vita vya pili vya dunia. Angalia superpowers zote na jinsi zilivyorise. Kuanzia Wagiriki na Wamisri waliosafiri baharini mpaka Warumi, Waingereza na Wamarekani. Sababu moja kubwa iliyofanya Europe itawale Africa, na si Africa kutawala Europe ni kwamba watu wa Europe walitoka kwao kuja kutafuta maisha Africa, bado hatujajifunza tu kwamba "Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu"?
Swala hapa si mimi kukupa mfano wa nchi iliyojengwa namna hii, bali wewe kunipa mfano wa nchi ambayo haijajengwa namna hii, kama ipo.
Isolationism does not work.The Chinese tried it and despite being far more advanced technologically at an earlier stage before Europe, this same isolationism coupled with an utopia of "China is the centre of civilization, therefore the Chinese do not need to go out" is what stagnated Chinese development for hundreds if not thousands of years.
Yaani wewe hoja zako zina ma logical fallacies mpaka nashindwa sijui nianzie wapi kukujibu. Wewe umefikiaje hizo conclusions ulizoandika? Kusafiri nje ya nchi na kuona maendeleo ya duniani siyo lazima uhamie huko uende kuwa mtumwa wao. Unaweza kwenda kuyaona na ukarudi kujenga kwako.
Logical fallacy ninayoiona hapa ni kufikiri kwamba kwa kuwa kusafiri nje ya nchi na kuona maendeleo ya dunia siyo lazima uhamie huko uende kuwa "mtumwa wao" na unaweza kwenda kuyaona na kurudi kujenga nchi yako, it follows kwamba huwezi kujenga uchumi wa nchi yako ukiwa nje ya nchi.
Non Sequitur. The premise and the conclusion are not connected.
Yaani unataka kufanya kama nchi nzima na watu wote ni homogeneous, wakati kuna watu tofauti, wenye uwezo na karama tofauti katika stages tofauti za maisha yao.
Zaidi ya hapo naweza kukwambia narudi nchini, nipo katika process ya kuona maendeleo ya nje. Utasema nini?
Kwamba unaweza kujenga nchi yako kutoka ndani ya nchi hakumaanishi kwamba huwezi kujenga nchi kutoka nje ya nchi, ndiyo maana nikasisitiza the complementary nature of these two sets.
Kati yangu ninayesema unaweza kuchangia uchumi wa nchi kutoka popote, na wewe unayesema kwamba kwa kuwa unaweza kwenda nje na kurudi nyumbani kujenga nchi yako, huwezi kujenga nchi kutoka nje, nani ana logical fallacies sasa?
Acheni medieval smallmindedness hizo za kujifungia chumbani unaogopa kupambana na wenzako katika dunia ya leo.
Kama unaendekeza uzalendo sana tutakutaka usitumie maandishi ya kigeni, usitumie internet iliyoanzishwa na wageni, rudi huko ukavumbue kila kitu mwenyewe tukujue wewe mzalendo kweli.
Otherwise utakuwa mnafiki tu na uzalendo nusunusu.
Above all, concept nzima ya "nchi" kwa watu wenye upeo inaanguka, unajitia uzalendo mkubwa na kukataa "utumwa" wa hawa wageni kwa kukumbatia hii concept ya "nchi" bila kujua kwamba kukumbatia hii concept ya "nchi" kama ilivyo sasa ni utumwa mkubwa sana uliowekwa na hawa wageni, kwa sababu hii concept nzima ya "nchi" tumeletewa na wageni hawa hawa.
Kati ya mimi ninayekataa hii concept kunifunga, na wewe unayekubali minyororo ya mikataba ya wageni ikufunge katika mipaka ambayo hata si ya asili, nani anakuwa mtumwa sasa?
Kusafiri nje ya nchi na kuona maendeleo ya duniani siyo lazima uhamie huko uende kuwa mtumwa wao.
Acha kuukana uraia wa nchi yako. Njaa itakuua.
Acha kuukana uraia wa nchi yako. Njaa itakuua.
Nani amekufunga wewe?
Nimekwambia watu wanaenda na kurudi.
Nilichokuuliza wewe unipe mfano wa nchi iliyojengwa kwa mantiki unayoongelea.
Mifano uliyotoa hai support hoja zako, usilazimishe.
Huja ni convince bado
kwamba brain drain ina faida kwetu.
Wewe jamaa kiazi kweli wewe. Unajua maana ya utumwa wewe?
Hivi mtu anayefanya kazi Airtel au Clouds FM ana tofauti gani na mtu anayefanya kazi Verizon Wireless au hhgregg?
Hakuna aliyenifunga, ndiyo maana last week nilikuwa bongo.
Huhitaji kuniambia hili, mwenyewe naenda na kurudi.
Nimekujibu nchi zote hujengwa kutoka ndani na nje, swali si nchi gani imejengwa kwa namna hii, ni nchi gani haijajengwa namna hii.Nimekuuliza hujajibu.
Unayelazimisha ni wewe unayeitaja mifano bila kuichambua na kuonyesha ni kwa vipi hai support hoja zangu. Kutaja kitu kijumla jumla bila maelezo ndiko kulazimisha kwenyewe.
Kama unafikiri niko hapa kuku convince wewe no wonder unafikiri isolationism ndiyo jibu la matatizo yetu.
Wewe unachoita "brain drain" wengine wataita "soldiers advancing behind enemy lines", "businesspeople breaking new grounds" and "knowledge workers looking for greener pastures".
Wewe kama una karama ya kubaki nyumbani hukatazwi, lakini usiwaseme wenye karama ya kuchangia uchumi kutoka nje.
Uchumi wenyewe mdogo, hata tukisema turudi wote utaweza kutu absorb? Au mnataka mambo ya uzalendo wa utopia?
Kama hao watu wa nchi tajiri wamejaa Africa wanatafuta ma deal, kwa nini sisi Waafrica tujifungie kwetu kwa sababu sentimental zisizo na mshiko katika dunia ya leo?
Halafu hujanijibu kuhusu kutumia maandishi ya kikwetu na internet ya kikwetu ili tujue kweli wewe mzalendo pure.Huu unafiki wa uzalendo nusunusu unakuwa exposed very easily hapa.
Wa Airtel anasukuma gurudumu la maendeleo la nchi yake. Analipa kodi, anatumia pesa zake hapa hapa na ananufaisha wabongo wenzake. Huyo wa Verizon anatumikia wazungu mpaka akizeeka.
Bado nasubiri mifano ya nchi zilizojengwa na mantiki unazoziongelea. Kama hakuna basi kwa nini unataka na sisi tufanye hayo mambo? Yaani eti tuwe brain drained halafu tutapata maendeleo. Mimi sijaona hayo mambo bado.
Unaweza kuomba uraia baada ya kuwa na hiyo Green card kwa miaka mitano!.
Huyu hapa hata hajajua jinsi uchumi wa dunia ulivyojichanganya kama maji kwenye ndoo, bado anafikiri chumi zimetenganishwa na mipaka ya nchi.
Labda nikuulize kwanza.Hiyo Airtel ni kampuni ya wapi?
Kama hujui anzia hapa chini.
Bharti Airtel - Wikipedia, the free encyclopedia
Kuna mtu anaweza ku argue kwamba huyu anayefanya kazi verizon anachukua hela za Wamarekani na kuzirudisha Tanzania kama remmittances, na huyu anayefanya kazi Airtel anatumika kuchukua hela za Watanzania na kuzipeleka India.
These things are not as simple as you are trying to make them be.
Kama unajua kusoma utaona nimekwambia nchi zote zimejengwa kwa support kutoka ndani na nje yazo, na nimekupa challenge ya kutaja nchi ambayo haijajengwa kwa kutoka nje.
But I suspect moja ya matatizo hapa ni fact kwamba hujui kusoma.
Mimi siyo wajibu wangu ku prove au ku support hoja zako dhaifu. Wewe ndiyo uliyoleta hoja kwa hiyo lazima uwe tayari kutoa ushahidi kama ukiulizwa. Halafu unaniuliza mimi nitaje nchi ambayo haijajengwa. Unataka mimi ni prove negative kitu ambacho katika logic hakipo.