Hakikisha una bank statement inayoonyesha flow ya hela nzuri kwa muda mrefu na bank letter inayokutambulisha kama mteja wa muda mrefu usiye na matatizo, hizi bank documents ni muhimu ziwe za nguvu.
Pia itasaidia ukiwa na document zinazoonyesha kwamba una strong ties na nyumbani (kama una barua ya muajiri inayoonyesha unakwenda kusoma na unatakiwa kurudi kufanya kazi baada ya kumaliza masomo, kama una nyumba, mke, shamba na vitu vingine vya kuonyesha chances za kuishia Marekani ni ndogo) ili kuowaondoa na wasiwasi wa kurudi kwako, unaweza kuongezea vingine lakini hizi ni muhimu kabisa.
Ma councillor wa ubalozini wanakuwa assessed ka jinsi gani wao wanaweza kuwa asses waomba visa, na kwa mujibu wa vyanzo vya uhamiaji wao (hii ilikuwa mara baada ya 9/11) councillors wanaowapa watu wengi wasiorudi/ wanaoondoka shuke bila kufuata mpango visa wanaonekana hawajafanya kazi zao vizuri.Ndiyo maana siku hizi uhamiaji unafuatilia mpaka attendance ya foreigners vyuoni.