Us sends 100 combat troops to uganda as advisors

Us sends 100 combat troops to uganda as advisors

Nyie vipi?
Hapo Joseph Konny wana maana ya Yowel Kaguta Mseven, subirini mje muone wanavyo-muadhibu mseven. Mseven ana kila dalili za kuwapa tenda wachina. Pole mseven siku zinatimia kwako.
 
wamarekani na mafuta ni sawa uji na mgonjwa au mgambo na kirungu au dala dala na konda.............

Huyu kony siyo wa jana wala juzi, siku zote yupo.....si chini ya miaka 25....lakini leo eti obama anakuja kumsaka......m7 na waganda kwa ujumla jamaa ananyemelea wese......mtoeni baru ......
 
  • Thanks
Reactions: tz1
kwani Kony hajulikani alipo??
mwaka jana tu hapa alikuwa anaugua na kuwa na shida ya chakula na walikuwa wanafanya negociations na Museveni, Museveni akawa anampa chakula.

Hapo ni PETROL tu hakuna kingine.
Mbona wasipeleke wanajeshi Somalia au border ya kKenya na Somalia??
Au wanawaogopa Alshabab??...........wazee wa Sambusa!!!
 
  • Thanks
Reactions: tz1
Habari wana JF???

Leo asubuhi vyombo vingi vya habari vimezungumzia habari ya Marekani kupeleka majeshi nchini Uganda kwa minajili ya kumtokomeza kabisa Joseph Kony na kundi lake la Lord Resistance Army!

Marekani yenyewe imesema itatumia vifaa vya hali ya juu vya kujua wapi Kony alipo ili ama auawe au akamatwe!

Je tuseme ndiyo mwisho wake umefikia??? Mchezo mwingine unaanza huo tena East Africa baada ya wa Libya kuonekana unaelekea ukingoni!!!

Nawasilisha
Watatumia drones,na Uganda watalipa kwa mikataba ya wese.
 
wamarekani na mafuta ni sawa uji na mgonjwa au mgambo na kirungu au dala dala na konda.............

Huyu kony siyo wa jana wala juzi, siku zote yupo.....si chini ya miaka 25....lakini leo eti obama anakuja kumsaka......m7 na waganda kwa ujumla jamaa ananyemelea wese......mtoeni baru ......
Marekani hawawezi kuachana na mafuta.Ni sawa na mgonjwa mwenye kuhitaji drip halafu unamchomolea.Uchumi wa marekani uliinuliwa na automotive manufacturing/industry.Ndiyo maana sehemu nyingi hawataki kuziendeleza public transportation.Yani wana discourage hayo.Na ikafikia mahali kuwa na gari ni very easy/cheaper,or atleast more people are encouraged to have cars.Shida ni hapo bei ya wese ilipopanda na biashara ya kununua magari ikashuka hence automotive production failure.
Marekani wese likipatikana kwa urahisi basi mambo mengi sana yanakuwa muruwa.
 
Mnanichanganya hapa. Wanawake wakiendelea kubakwa na maelfu wakiendelea kuuwawa mnalalamika. At least US wameonyesha njia ya kusaidia kuliko AU ambayo imekuwa just a big joke kwa waafrika wote
 
MAZZOUT, ESSENCE
miaka yote kumi aliokuwa wapi ndio leo aje kutoa msaada?
 
Mafuta ya Uganda yananukia, Ingawa kweli Konyi amefanya uhalifu mwingi, lakini walikuwa wapi siu zote hizo? !

Una akili sana wewe. Hawa LRA walikuwepo kwa miaka mingi sasa lakini Wababe wa dunia hawakuona umuhimu wa kumwaga wanajeshi wao mpaka baada ya mafuta kupatikana kule Uganda si ajabu hii pia ndio itatumia katika kuweka kituo chao kikubwa cha jeshi Afrika pale Uganda. Hawa jamaa wakiingia mahali ambapo wanaona watafaidika basi huwa hawaondoki kabisa.
 
Where's China?
 
Wamarekani hawana haja ya kuipeleleza uganda. Museveni anawapa siri zote bila wasiwasi, kama ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrica hivi sasa!

mkuu wewe una akili sana.ni kweli lakini ishu kubwa ni mafuta.kama tanzania tuligawa kigamboni sababu ya vyandulia unafikili kuna nini?yaani tumegawa ardhi tupate vyandarua.mababu zetu waliuza zanzibar kwa kipande cha kitambaa.tuna tofauti gani nao?waafrica tumerogwa.roger
 
Kweli, bana. US wako tayari hata kusaidia ujenzi wa miundo mbinu ya "Northern corridor"

Baada ya ujio wa "washauri" tutasikia Al shabaab wamejiingiza Tanzania na washauri hawa watakuja kutushauri jinsi ya kuwashughulikia "magaidi".

Tembelea hii
BBC News - US to send troops to Uganda to help fight LRA rebels

Increased Regional Trade and Integration | USAID East Africa Regional Mission

The Permanent Secretariat of the Transit Transport Coordination Authority of the Northern Corridor

Si umeona juzi juzi tu eti wasomali walitaka kuteka meli Mafia!.Hii ni mipira ya mbali ya Marekani.
Msemaji wa JWTZ alisema hawa jamaa ni jeuri kweli na inaonekana wanaweza wakajiripua na kuhatarisha usalama wa askari wetu.Kama kwamba anazungumza na vizuu.Inawezekanaje wakajiripua wakati tayari wako katika udhibiti wao,kama ni silaha zote wamewanyan'anya.Kama ni kujiripua si wangefanya hivyo wakati wa purukushani za kuwakamata?.Hii ni dalili ya kutumwa na kushindwa kutumika vizuri.
Kumbuka hapa JF tayari kuna thread ya fitna eti maharamia wa kisomali wako kwenye majumba makubwa ya Mbezi.

Uwezekano wa wale wasomali waliokamatwa ni kuwa ni wakimbizi tu wa njaa ambao mimi naelewa wanasafiri kwa wingi bahari ya hindi kuelekea Afrika Kusini na Msumbiji.JWTZ nao wanajuwa hivyo waliamua kushika kikundi fulani ili watekeleze agizo lenye lengo la mbali.
 
Last edited by a moderator:
Where's China?

Unajua China bado hawawezi kushindana na US inapokuja suala la kutafuta soko, sababu ni kama zifuatazo :
  • China bado nchi inayoendelea, ambayo licha ya kuwa serikali yake ni tajiri sana, lakini wananchi wengi ni masikini, hivyo bado inachangamoto kubwa sana.
  • China inatumia sana nguvu ya uchumi wake kuweka influence duniani, lakini US wanatumia Uchumi na nguvu ya kijeshi, Mf. wataahidi ushikiriano katika mambo ya kiulinzi na kiintelejensia.
  • China bado haiwezi kukabiliana na changamoto za kiusalama duniani kutokana na Jeshi lake kutokusambaa nje ya mipaka yake,(ukiachana na meli chache walizotuma kukabili maharamia wa Kisomali)
  • Viongozi wengi wa kiafrika ni walafi, wanamadhambi mengi waliyoyafanya, ikiwamo kuhujumu uchumi, hivyo kama wakiingia dili na US wanaweza kulindwa pale mambo yatakapoharibika.
China wanafanya dili nyingi sana na nchi zingine zinazoendelea ambazo viongozi wake wanaakili mf nchi za Latin America, baadhi ya nchi za Asia.
Lakini bado wanajitahidi kulichukua soko la Africa.
 
Mr. Kony now it's your turn to face the wrath of the AntiChrist. Licha ya kuwa "msemaji wa Mungu" sasa Kony upo hatarini kulipuliwa na kereng'ende (drones) za wamarekani. Jasho litakutoka. Umeyataka mwenyewe. Sikuonei huruma!
Kama we ni askari kanzu kweli unajua maana ya askari kanzu.unachofikiria sicho.
Mkuu jaribu kuangali USA ni polisi wa ulimwengu,UN ni yao.Kazi kwako kuna vitu vingi vya kutafuta kwenye google na Jf ndo tunapo elimishana.
 
kwani Kony hajulikani alipo??
mwaka jana tu hapa alikuwa anaugua na kuwa na shida ya chakula na walikuwa wanafanya negociations na Museveni, Museveni akawa anampa chakula.

Hapo ni PETROL tu hakuna kingine.
Mbona wasipeleke wanajeshi Somalia au border ya kKenya na Somalia??
Au wanawaogopa Alshabab??...........wazee wa Sambusa!!!
Nakubaliana na wewe .
Jiulize kwa nini wako Pakistan ili wawe jirani na afganstan.
Kwa nini afganstani ni kuwa jirani na warusi.
Walifanikiwa kuvunja umoja wa urusii kwa nia ya kuweza kutumia nchi mpya zitakazo undwa baada ya ku vunja
Umoja wa nchi za kirasha kama wanavyo tumia Poland sasa hivi kuweka mitambo yao ya kujikinga kama wakishambuliwa na warusi.
Na sasa wamethubutu na wamefanikiwa north Afrika na sasa wanaenda Uganda na wakifika hapo E Afrika iko chini yao na hapo waennda kusini nia yao kubwa ni mugabe na baada ya hapo swazi na afrika ya kusini na wote tutakuwa vibaraka wa USA.
 
Kama we ni askari kanzu kweli unajua maana ya askari kanzu.unachofikiria sicho.
Mkuu jaribu kuangali USA ni polisi wa ulimwengu,UN ni yao.Kazi kwako kuna vitu vingi vya kutafuta kwenye google na Jf ndo tunapo elimishana.
Wewe ni nani unaefikiria kilicho?
 
Nakubaliana na wewe .
Jiulize kwa nini wako Pakistan ili wawe jirani na afganstan.
Kwa nini afganstani ni kuwa jirani na warusi.
Walifanikiwa kuvunja umoja wa urusii kwa nia ya kuweza kutumia nchi mpya zitakazo undwa baada ya ku vunja
Umoja wa nchi za kirasha kama wanavyo tumia Poland sasa hivi kuweka mitambo yao ya kujikinga kama wakishambuliwa na warusi.
Na sasa wamethubutu na wamefanikiwa north Afrika na sasa wanaenda Uganda na wakifika hapo E Afrika iko chini yao na hapo waennda kusini nia yao kubwa ni mugabe na baada ya hapo swazi na afrika ya kusini na wote tutakuwa vibaraka wa USA.
Acha kudanganya watu. Usifikirie sote humu ni zao la shule za kata. Uchambuzi wako hauna mashiko!
 
Back
Top Bottom