US-Russia wakubaliana mpango wa kusitisha mapigano Syria

Maswala

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
560
225
USA na Warusi wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano ndani ya Syria baina ya makundi hasimu isipokuwa kwa makundi Daesh (IS/ISIS), Al-Nusra na mengine yaliyoorodheshwa na UN kama makundi ya kigaidi.

Makubaliano hayo yanaanza kutekelezwa 27 Feb, 2016 saa 00:00. Wahusika watalazimika kukubaliana kwa kusaini kabla ya 26 Feb. Wasiokubaliana maanake wataendelea kutwanga mabovu, huku waliosaini wakiunganisha nguvu zao kupigana na Daesh.

Mkakati unakuja siku chache baada ya Rais Barack Mobama wa Marekani akiwa amekiri "kiana" kushindwa maswaiba wake wapinzani wa serikali ya Syria inayosaidiwa na Warusi.

Obama alisema mapigo ya Urusi ni makali na wapinzani hawataweza kustahimili, hivyo ni bora kupatikana na suluhu ya kisiasa badala ya kijeshi, sawa na msimamo wa toka mwanzo Rais putin wa Urusi.

Kwa upande mwingine, Uturuki anaweza kuwa na wakati mgumu kwani kwa utaratibu huu, agenda yake ya kuvamia na kuwadhibit Wakurdi itakuwa imedhoofishwa kabisa.

Soruces; France 24 TV, rt.com, sputniknews.com.
 
Yaani USA wamefyata mkia. Wakati Warusi wakianza mashambulizi ya anga, walimbeza sana kuwa "nguvu za soda".

Imebi wapinzani wa Assad na Wamagharibi wote kubadili msimamo wao wa awali wa kutaka Rais huyo wa Syria kuachia ngazi.
 
Na wewe kwa upeo wako kabisa unakubali mzozo wa Syria utamalizwa na maneno ya Putin na Obama kwenye simu?....hahah asee mnachekesha kweli
 
Na wewe kwa upeo wako kabisa unakubali mzozo wa Syria utamalizwa na maneno ya Putin na Obama kwenye simu?....hahah asee mnachekesha kweli
Yes! Kwa sababu hawa ndo waanzilishi na wadhamini wakuu. Ikiwa wao wameridhia, naamini inawezekana!
 
da! yani baada ya kukombolew maeneo muhimu ndo vita vinaisha,bora hata Isis wanazibiti jangwa kuliko awa syria rebels maan kila kona wamezunguk ktk maeneo wanayoyazibit hata kupata misaad inakuwa kazi kubw san
 
Eneo dogo liloko chini ya himaya ya Serikali ndo lenye watu wengi inasemekana zaidi ya 80+. Na hii ndo sababu kubwa USA na washirika wake hawakupenda kusikia uchaguzi, wanajua jamaa lazima ashinde!
 
Na wewe kwa upeo wako kabisa unakubali mzozo wa Syria utamalizwa na maneno ya Putin na Obama kwenye simu?....hahah asee mnachekesha kweli
haya mataifa makubwa yanachezea Uhuru wa mataifa madogo Mimi sitegemei usitishaji wa vita kwa njia hiyo ya kuwasiliana na kukubaliana kati ya Putin na Obama. Ingawa ndiyo waamuzi wa masuala ya dunia. UN haiwezi fanya kitu kama haya mataifa hayakubali.
 
Yes! Kwa sababu hawa ndo waanzilishi na wadhamini wakuu. Ikiwa wao wameridhia, naamini inawezekana!
Aaa wapii...mzozo wa syria utamalizwa na wa syria wenyewe tuu..na si hawa sjui ma super power wanaokaa vikao kila sku visio na tija...
Na hii sio mara ya kwanza wao kupiga soga kwe simu,na bado mapigan yanaendelea tuu had leo..syria kwa sasa ishakuwa magofu tupu..kila sku madege ya russia na ya magharib yanazid kubomoa majengo syria...mwisho wa hii vita ni syria kubaki mashimo tuu bas...kama russia angelitaka kusaidia,angeingilia mapema wakat us walipoanza ku bomb syria,sio anakuja loo late na videge vyake wakan nchi ishakuwa magofu....
Wote hawa ni ma mbwa tu no body cares kuusu dhaman ya maisha ya watu wa syria tena...
 
Back
Top Bottom