Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,554
Shirikisho la soka Barani Ulaya limeshikilia msimamo wake wa kutoiruhusu nchi ya Urusi kushiriki michuano ya kufuzu UERO mwaka 2024.
Huu ni mwendelezo wa vikwazo kwa nchi hiyo kufuatia kufanya uvamizi wa kijeshi kwenye nchi ya Ukraine.
Hadi sasa, vilabu vya soka nchini humo vimezuiwa pia kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Kwa mujibu wa UEFA, nchi hiyo haitashiriki kwenye droo ya makundi ya kufuzu kwa fainali za EURO inayotazamiwa kufanyika Octoba 9, 2022 mjini Frankfurt.
Independent
Acha waongeze ukubwa wa nchi yao kwanza🏃Tutai miss timu yao nzuri kwenye michuano hii
Watu wa Magharibi na US ndiyo wanatawala mifumo ya Dunia tunayoishi leo.Urusi alijipima nguvu na mabeberu ona sasa wanamla mande kila sehemu.
Atacheza na China na Iran?Putin anzisha EURO yako !!
Uganda na India.Atacheza na China na Iran?
ndio hivyo,mkubwa mkubwa tu.Hivi marekani na washirika wake waliokua nyuma yake kuivamia iraq mpaka kuuawa kwa saddam na civilians kwa ujumla, na isitoshe wakaivamia na libya, je! walichukuliwa hatua gani? Je, mataifa hayo yalizuiwa kushiriki mashindano yoyote duniani kama wafanyavyo kwa URUSI?
Israel dhidi ya Palestina(Uvamizi+Mauwaji ya civilians kwenye ardhi yao), je! Alishawahi kuchukuliwa hatua ama kuzuiwa kushiriki mashindano yoyote duniani??
Ni jambo la mbolea,mvamizi ,mhalifu lazima atengwe hata kama wanamichezo wataumia.Serikali zetu zinakatazwa kuingilia soka, ila wenye dunia wameutumia huo mchezo kuziadhibu timu na wanamichezo wa Urusi ambao hawahusiki na maamuzi ya kisiasa ya viongozi wao.
Huu ni undumilakuwili.